• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 11-Aprilii 17)

    (GMT+08:00) 2020-04-17 17:15:06

    China yapitisha majaribio ya chanjo mbili za corona, mchakato wa muda mrefu kuepukwa

    Wakati wanasayansi wakichuana kutafuta kinga ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, serikali ya China imeruhusu majaribio mawili zaidi ya chanjo ya kudhibiti ugonjwa huo uliogeuka janga duniani.

    Jumatatu, mamlaka ya serikali ya chakula na dawa, iliidhinisha chanjo moja iliyotengenezwa na kampuni ya Sinovac Biotech ambayo imesajiliwa katika soko la Nasdaq na makao yake makuu ni Beijing.

    Chanjo nyingine inayotengenezwa na Taasisi ya Bidhaa za Kibaiolojia ya Wuhan pamoja na Taasisi ya Virolojia ya Wuhan, iliidhinishwa Jumapili. China iliidhinisha majaribio ya kwanza kwa chanjo iliyotengenezwa na Kituo cha Sayansi ya Tiba cha Kijeshi pamoja na kampuni ya CanSino Bio ya Hong Kong Machi 16.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako