• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 11-Aprilii 17)

    (GMT+08:00) 2020-04-17 17:15:06

    Kenya yamwomboleza mwandishi stadi

    Biwi la simanzi limetanda nchini Kenya kufuatia taarifa za kifo cha ghafla cha mwandishi, mwalimu na mwanahabari maarufu, Prof Ken Walibora

    Taarifa za kifo cha Walibora, 56, ambaye aliwahi kuwa mwanahahari wa kampuni ya habari ya Nation Media Group (NMG), zilijulikana na kuthibitishwa asubuhi ya Jumatano, siku tano baada ya kufariki kwake Ijumaa iliyopita.

    Hadi kifo chake, Prof Walibora alikuwa mchangiaji mkuu wa makala ya Lugha, Fasihi na Elimu katika gazeti la Taifa Leo na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Riara, Nairobi.

    Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi katika eneo la Nairobi, Bw Philip Ndolo, Prof Walibora aligongwa na matatu kwenye barabara ya Landhies, Nairobi Ijumaa ya Aprili 10, 2020.

    Msomi huyo ambaye anafahamika mno kwa kitabu chake cha 'Siku Njema' alitoweka wiki iliyopita, na tangu wakati huo, alikuwa akitafutwa na familia, marafiki, jamaa na baadhi ya wafanyakazi wenzake bila ya mafanikio.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako