• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 11-Aprilii 17)

    (GMT+08:00) 2020-04-17 17:15:06

    Wanaofadhili WHO, na athari za Trump kulinyima ufadhili shirika hilo.

    Wingu la hofu limetanda kuhusu hatma ya shirika la afya duniani WHO kufuatia uamuzi uliochukuliwa na rais Donald Trump wa Marekani

    Rais Donald Trump Jumanne aliagiza kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani katika Shirika la Afya Duniani wakati linakabiliana na janga la virusi vya corona lililokumba ulimwengu.

    Rais wa Marekani amesema kwamba hatua hiyo itatekelezwa huku ikipitia tena jukumu la Shirika hilo wakati ambapo limeshindwa kusimamia uendeshaji wa shughuli za kukabliana na ugonjwa wa covid-19, pamoja na madai ya kutosema ukweli kuhusu maambukizi hayo.

    Lakini Je WHO imekuwa ikifadhiliwa vipi?

    Ufadhili wa lazima na wakujitolea

    Shirika hilo liliundwa 1948 kama sehemu ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, likilenga kuendeleza afya bora, kuhakikisha dunia inakuwa salama na kuhudumia wale walio katika hatari zaidi."

    Taasisi hiyo, ambayo makao yake makuu ni Geneva (Uswizi), ilikuwa na bajeti ya karibia dola bilioni 5.6 kwa kipindi cha miaka miwili 2018-2019, na vyanzo vyake ni viwili tofauti.

    Kwanza, kuna pesa ambazo ni lazima zitolewe na nchi washirika 194.

    Kila nchi inatakiwa kulipa kiwango fulani kulingana na Umoja wa Mataifa kupitia mfumo ambao ni vigumu kuelezeka kwasababu unazingatia utajiri wa nchi na idadi ya watu.

    Ni pesa ambayo kwa msingi huwa inasimamia mishahara na utawala wa shirika hilo. Mwaka 2018-2019, ufadhili huo ulijumuisha karibia dola milioni 950 za Marekani.

    Pili ni ufadhili wa kujitolea unaowezesha nchi na maeneo kuahidi pesa watakazochangia kwa maswala maalum, kama vile chanjo ya ugonjwa wa polio, afya ya wanawake au ukabilianaji na matumizi ya tumbaku.

    Mwaka 2018-2019, fedha hizo zilikuwa karibia dola bilioni 4.3.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako