• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 11-Aprilii 17)

    (GMT+08:00) 2020-04-17 17:15:06

    Uhispania: Maelfu waanza kurejea kazini

    Mapema wiki hii, maelfu ya watu nchini Uhispania walianza kuruhusiwa kurejea kazini, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuibuka kwa mlipuko wa virusi vya corona, ambapo serikali iliweka marufuku ya kufanyika shughuli za kawaida.

    Jumatatu ya Pasaka kwa taifa hilo haikuwa siku ya kitaifa ya mapunziko kwa raia badala yake waliruhusiwa kuondoka majumbani mwao, ikiwa hatua ya taratibu ya kuindoa marufuku iliyodumu tangu mwezi uliopita.

    Kwa mujibu wa makadirio ya vyombo vya habari, takribani watu 300,000 walirejea makazini mjini Madrid. Kabla ya hatua hiyo, watu ambao ajira zao zilionekana kuwa na ulazima kufanyika waliruhusiwa kufanya kazi. Katika kipindi kigumu nchini Uhispania kulirekodiwa hadi maambukizi 8,000 kwa siku.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako