• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 11-Aprilii 17)

    (GMT+08:00) 2020-04-17 17:15:06

    Jamaa amdanganya Waziri Ummy ana Corona, akamatwa na Polisi

    Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia, Mussa Jackson Kisinza (25) Mkazi wa Kijiji cha Mwakitolyo II kwa kutoa taarifa ya uongo baada ya kumpigia simu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuwa ana ugonjwa wa Corona.

    Kamanda wa polisi mkoani huko, ACP Debora Magiligimba amesema kuwa baada ya taarifa hiyo timu ya madaktari inayotoa huduma eneo la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini katika kukabiliana na Covid 19, ilifika ili kutoa huduma kwa mtu huyo ambaye alizima simu yake na kuchangia timu hiyo kushindwa kumpata hali iliyozua taharuki.

    Kikosi kazi cha makosa ya kimtandao cha jeshi hilo kilifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa kisha kufikishwa kwenye zahanati ya kijiji hicho baada ya vipimo vya awali vilibaini mtuhumiwa kutokuwa na dalili za ugonjwa huo.

    Baada ya mtu huyo kuhojiwa amekiri kutoa taarifa hizo kisha kuharibu simu yake kwa kuivunjavunja ili kukwepa mkono wa dola.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako