• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 18-Julai 24)

    (GMT+08:00) 2020-07-24 17:08:53

    China yalaani Marekani kwa kuitaka kufunga ubalozi wake mdogo mjini Houston

    Wiki hii serikali ya Rais Donald Trump imeishangaza ulimwengu kwa kuendelea na sera yake ya kuiandama China kwa kutoa muda wa saa 72 kufunga konseli kuu ya China mjini Houston, kwa kisingizio cha "kulinda taarifa binafsi za wamarekani na kulinda haki za ubunifu za wamarekani".

    China imeilaani Marekani kwa kuitaka kufunga ubalozi mdogo wake mjini Houston.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin alhamisi jijini Beijing alisema China inailaani vikali Marekani kwa kuitaka ifunge ubalozi mdogo wake mjini Houston.

    Alisema hatua hiyo ni uchochezi wa upande mmoja wa Marekani dhidi ya China, na kukiuka sheria ya kimataifa na kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa, na mkataba wa mambo ya konseli kuu kati ya China na Marekani, na kuharibu uhusiano kati ya China na Marekani kwa makusudi.

    China inalaani vikali hatua hiyo ya Marekani, na kuitaka kufuta mara moja uamuzi husika wa makosa, ama sivyo China itatoa majibu yake ya haki na ya lazima.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako