• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 18-Julai 24)

    (GMT+08:00) 2020-07-24 17:08:53

    Waziri Mkuu wa Ethiopia apongeza kuanza kujazwa maji kwa bwawa la GERD

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amepongeza kuanza kujazwa maji kwenye bwana kubwa la Ethiopia la GERD, na kusema bwawa hilo litaanza kuzalisha umeme mwaka kesho.

    Bwana Ahmed amesema hayo siku chache baada ya Misri na Sudan kusema kumekuwa na maendeleo kwenye mazungumzo kati ya pande tatu kuhusu bwawa hilo lenye thamani ya dola bilioni 4.6.

    Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Misri na Sudan kuhusu nia ya Ethiopia kujaza maji kwenye bwawa hilo na kusema itahatarisha maslahi ya watu wake, lakini Waziri mkuu amesema hatua ja kwanza ya kujaza maji kwenye bwawa hilo inatokana na mvua kubwa, na haijaathiri upande wowote.

    Bwawa hilo linatarajiwa kuanza kuzalisha umeme kikamilifu mwaka 2023.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako