• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 18-Julai 24)

    (GMT+08:00) 2020-07-24 17:08:53

    Nimonia isiyojulikana nchini Kazakhstan huenda inatokana na maabara ya viumbe ya Marekani

    Hivi karibuni nimonia isiyojulikana imelipuka nchini Kazakhstan, na kusababisha vifo vya watu wengi. Maabara ya utafiti wa viumbe ya Marekani nchini humo yamefuatiliwa sana na watu kutokana na uwezekano wake wa kusababisha ugonjwa huo mkali.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ya Kazakhstan, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, idadi ya maambukizi ya nimonia hiyo ilifikia 98,546, na katika mwezi Juni, watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo wamezidi 600 nchini humo, ambapo kiwango hiki cha vifo ni juu zaidi kuliko COVID-19. Baadhi ya watu wanaamini kuwa sababu ya nimonia hiyo ni virusi kutoka maabara ya utafiti wa viumbe yaliyojengwa na Marekani nchini humo.

    Maabara hiyo iliyoko mjini Almaty ilianzishwa mwaka 2010 na serikali ya Marekani kwa madhumuni ya utafiti wa kisayansi na kuhifadhi virusi vikali. Kazakhstan inayopakana na China na Russia inachukuliwa na Marekani kama ni sehemu bora ya kujaribu silaha za viumbe, kwani virusi vinaweza kuenea nchini China na Russia kwa kasi kwa makusudi au kutokana na ajali.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako