• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Jinsi gani wachina wanavyojitahidi kulinda faida ya wateja
    Katika nchi nyingi za Afrika kumekuwa na malalamiko kuhusu bidhaa za China, kuna wale wanaosema kuna bidhaa nyingi feki kutoka China, baadhi ya watu wamekuwa hata wakilalamikia baadhi ya huduma zinazotolewa na makampuni ya China kuwa ni hafifu, kwa kuwa wahusika wanaangalia faida zaidi kuliko ubora wa huduma. Leo basi tunaangalia ni jinsi gani wachina wanavyojitahidi kukabiliana na tatizo hii.
    • Changamoto ya usalama barabarani
    Beijing, Shanghai na Guangzhou ni miji mikubwa zaidi hapa China. Sio kama tu miji hii ina maendeleo makubwa kiuchumi, na idadi kubwa ya watu, bali pia ina idadi kubwa sana ya magari. Leo tunawaeleza jinsi miji hii inavyokabiliana na changamoto ya usalama barabarani.
    • Mafanikio na changamoto ya kupambana na umaskini nchini China
    China imepata maendeleo zaidi katika kupunguza idadi ya watu maskini, tutaangalia hali ikoje katika sehemu za mijini na kulinganisha kidogo na hali katika sehemu nyingine.
    • Mambo yaliyojadiliwa sana mwaka jana na wana mtandao na watu wengine kwenye jamii ya China
    Mwisho mwa mwaka jana neno "Tu Hao" liliienea kwenye mtandao wa internet hapa China. Neno hilo kwa kweli lina maana mbaya, lakini naweza kusema, ni kutokana na watu kupata utajiri kwanza, lakini kuendelea kuwa na mawazo ya zamani au kuwa na mawazo ya "kishamba". Mwezi Septemba neno hilo lilitajwa sana na watu hapa China, baada ya kuona kuwa kuna wimbi kubwa la watu kutumia pesa ovyo, kwa kuwa tu wana pesa bila hata kujali wanatumia vipi pesa hizo.
    • Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China
    Mara nyingi katika kipindi hiki huwa tunazungumzia mambo ya kijamii, lakini leo nimeona tuzungumzie kidogo mambo ya kisiasa, kwa kuwa kuna jambo moja ambao ni geni kabisa, ambalo nimeona ni vizuri nikawafahamisha wasikilizaji ili muwe na uelewa zaidi kuhusu siasa za China, na jinsi watu wanavyoshiriki kutoa maoni na mapendekezo yao kwa serikali yao.
    • Mambo kuhusu Wachina
    Kumekuwa na imani potofu kuhusu mambo ya kijamii hapa China, kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa hapa China watu wote wanafanana na wengine wanaona majina ya mume na mke yanafanana wanafikia hata kusema hapa China, ndugu wanaoana. Ukweli wa mambo hayo unakuwaje?
    • Lugha ya Kiingereza
    Ukiwa hapa China moja kati ya mambo yanayoweza kukufanya uifurahie China, ni kuonana na mwenyeji ambaye mnaweza kuongea naye na kuelewana. Ni vizuri sana kama unajua Kichina, lakini kwa kuwa Kichina ni lugha ngeni sana kwa wageni, si mbaya kama ukikutana na Mchina anayeweza kuongea lugha unayoweza kuongea.
    • Mji wa Guangzhou
    Guangzhou ni mji unaofahamika sana kwa watu wengi kutoka Afrika Mashariki, hasa wafanyabiashara. Ni changamoto gani wanazokumbana nazo, na wafanye nini ili wao na wafanyabiashara wengine wnaokuja China waweze kufanya kazi zao na biashara bila matatizo?
    • Maisha ya Waafrika mjini Guangzhou
    Mji wa Guangzhou ambao baadhi ya Waafrika wanauita "gwanzuu" unafahamika kwa Waafrika wengi kutokana na kuvutia wafanyabiashara wengi, na kutokana na bidhaa nyingi zinazotengenezwa mjini humo kuuzwa katika nchi za Afrika.
    • Siku ya kupanda miti
    Tarehe 12 Machi wiki ni siku ya kupanda miti nchini China, kila inapofika siku hii watu katika sehemu mbalimbali hapa China huwa wanashirikishwa katika harakati za kupanda miti. Harakati hizi ni sehemu ya mpango wa kupambana na hali ya jangwa na kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwaka 2050, eneo la ardhi la China lililofunikwa na mmisitu linafikia asilimia 28.
    • Siku ya wanawake
    Leo ni siku ya wanawake. Vijana wengi huwa wanauliza kina dada Wachina wakoje? Wana tofauti gani na kina dada kaitka sehemu nyingine duniani? Je wana changamoto gani na wanakabiliana vipi na changamoto hizo?
    • Maisha ya wastaafu nchini China
    Utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa Wachina wengi waliostaafu wanafurahia maisha ya kustaafu, na wale ambao wanakaribia kustaafu wanapanga vizuri bajeti zao ili waweze kutumia pesa zao vizuri baada ya kustaafu. Karibu wastaafu wote hapa China wanapokea fedha za malipo ya uzeeni, japo si nyingi sana, fedha hizo zinaweza kukidhi mahitaji yao ya kimsingi.
    • Michezo yanayofanywa na Wachina katika majira ya baridi
    Majira ya baridi bado yanaendelea hapa China. Katika kipindi hiki watu hapa China wanafanya michezo ya ujasiri, ambayo baadhi ya watu wanaona inaimarisha mwili na wengine wanaikosoa na kuitaja kuwa ni michezo yenye hatari kwa afya zao.
    • Shule za msingi zafunguliwa
    Hapa China wanafunzi walikuwa katika likizo ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, ambapo walipewa mapumziko ya mwezi mmoja. Sasa wanafunzi hao wamerudi shule na kuanza muhula wa pili wa masomo, na wazazi wanatakiwa kujipanga kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto wao kudamka kwenda shule na kukabiliana na muhula mpya wa masomo.
    • Sikukuu ya taa
    Sikukuu ya taa huwa inakuwepo siku ya 15 ya mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya China, ambayo inaashiria kwisha kwa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ya China. Hapa Beijing kulikuwa na shamrashamra za sikukuu ya taa, na watu huwa wanakula vyakula maalum katika sikukuu hiyo, yaani "Tangyuan" au "Yuanxiao".
    • Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China
    Kila mwaka baada ya watu wa sehemu nyingine duniani kusherehekea sikukuu za Krismas na mwaka mpya, Wachina huwa wanaanza kufanya maandalizi ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi. Hii ni sikukuu kubwa kabisa kwa Wachina kama ilivyo Krismas kwa Wakristo na Idd el Fitr kwa Waislamu.
    • Hospitali nchini China
    Baadhi ya Waafrika wana maswali kuhusu hospitali na matibabu hapa China zikoje, na baadhi wamekuwa na picha isiyo sahihi wakidhani ni sawa na vibanda vinavyouza dawa za mitishamba ya Kichina vinavyoonekana katika miji mbalimbali kama nchini Tanzania au Kenya.
    • Likizo ya majira ya baridi
    Ikiwa ndio tuko mwanzo mwa mwaka, hapa Beijing kwa sasa tuko katikati ya majira ya baridi na siku chache zijazo wanafunzi wataanza mapumziko ya majira ya baridi. Baada ya wanafunzi kufanya mitihani ya muhula wa kwanza unaoanza mwezi Septemba na kuishia mwezi Januari, inamaanisha kuwa likizo inaanza.
    • Sikukuu ya mwaka mpya
    Sikukuu ya mwaka mpya imekaribia, itaanza wiki ijayo. Huu ni mwaka mpya ambao umezoeleka karibu kila mahali duniani, kwa kuwa shughuli nyingi za kimataifa kama mikutano au mipango ya shughuli za kidiplomasia za kimataifa zinafanyika kwa mujibu wa kalenda ya kimataifa. Hapa China licha ya siku hiyo ya mwaka mpya, pia kuna mwaka mpya mwingine.
    • Sikukuu ya Krismasi
    Ndiyo hivyo tunamaliza mwaka, na kila inapofika mwishoni mwa mwaka kunakuwa sikukuu mbili kubwa, moja ni sikukuu ya Krismasi na nyingine ni sikukuu ya mwaka mpya.
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako