• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Usalama wa kuendesha magari barabarani
    China inasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, lakini idadi kubwa ya watu pia ina maana kuwa kama watu wana uwezo wa kiuchumi basi idadi ya magari itakuwa kubwa. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, kwa wastani kila familia 100 zina magari 25, na katika miji mikubwa idadi hiyo ni kubwa zaidi. Kwa hiyo hali ya msongamano wa magari barabarani inaongezeka siku hadi siku.
    • Ugatuzi kama hatua ya kuondoa urasimu
    Hivi sasa kuna mjadala unaoendelea hapa China kuhusu changamoto ndogo ndogo wanazokabiliana nazo watu wanapotafuta huduma kwenye idara za serikali. Kutokana na kufuata utaratibu kupita kiasi hata kwenye mambo madogo madogo, baadhi ya watu wanaona kuwa huu ni urasimu usiohitajika.
    • China yafanya juhudi kupambana na matumizi ya tumbaku
    Tarehe 31 Mei itakuwa ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani. China ambayo ni nchi inayoongoza kwa matumizi ya tumbaku duniani inaungana na nchi nyingine kuadhimisha siku hiyo. Hapa China tunaona wazi kabisa kuwa serikali iko makini sana kufuata maelekezo ya shirika la afya la kimataifa WHO kuhusu kupiga marufuku matangazo ya tumbaku. Toka nimefika hapa China hadi leo sijawahi kusikia radioni, au kuona kwenye TV na hata kwenye gazeti tangazo la biashara linalohusiana na tumbaku, hata ukitembelea barabarani huwezi kuona mabango yenye matangazo yanayohamasisha watu kutumia tumbaku.
    • Juhudi za China katika kupunguza maafa
    China ni moja kati ya nchi zinazokumbwa na maafa makubwa ya asili. Mfano wa majanga makubwa yaliyotokea miaka ya karibuni ni tetemeko kubwa la ardhi la mji wa Wenchuan mwaka 2008, lililosababisha vifo vya watu karibu elfu 70. Janga hilo lilifanya wachina waanze kujadili namna na kujikinga na kupunguza maafa inapotokea janga kubwa kama hilo.
    • Umuhimu wa familia kwa wachina
    Wachina kwa kawaida ni watu wa familia. Na umuhimu wa familia kwa wachina una historia ndefu, kwa tunaoishi hapa Beijing na tukitembelea sehemu za katikati ya Beijing ambazo zilikuwa na nyumba za zamani, tunaweza kuona nyumba ambazo ndani yake kulikuwa na familia hata za vizazi vitatu, yaani babu na bibi, baba na mama, na watoto wanaishi katika nyumba moja, na wengine tunasikia hata kama hawaishi kwenye nyuma moja basi, wanaishi karibu na wazazi wao au ndugu wa karibu. Kwa hiyo kwa ujumla familia ni kitu chenye umuhimu wa kipekee kwa wachina.
    • Huduma ya mtandao wa internet
    China ni nchi iliyopiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.Lakini maendeleo ya huduma ya Internet kwa kiasi fulani hayana uwiano mzuri. Kuna baadhi ya maeneo ya China, hasa ya mijini, huduma ya internet imefika kila kona, na kuna baadhi ya maeneo bado huduma ya internet haijawafikia watu wote kwa njia sawa na watu wa mijini au maeneo yenye maendeleo makubwa kiuchumi.
    • Wachina wanavyolinda mazingira ya asili ya dunia
    Tarehe 22 Aprili ilikuwa ni siku ya sayari ya dunia, siku maalumu iliyopangwa na Umoja wa Mataifa kuwakumbusha watu kuwa na mwamko wa kuwa na mienendo inayolinda dunia yetu.
    • Maendeleo ya usimamizi wa mtandao wa internet ya China

    Siku hizi kuwasiliana na mtu yoyote katika nchi yoyote imekuwa rahisi, habari, picha na video vinawafikia watu kwa urahisi sana ikilinagnishwa na miaka ya nyuma. Lakini kwa upande mwingine urahisi huo umeleta changamoto kubwa sana kwa jamii na hata kwa serikali za nchi zenye matumizi makubwa ya mtandao wa Internet. Serikali ya China imeweka kanuni, sheria na hatua nyingi za kusimamia mtandao wa Internet.

    • Usimamizi wa fedha za familia hapa China
    Katika utamaduni wa China wanaume na wanawake wanashirikiana kusimamia mali za familia, lakini kuna wakati wanawake wanasimamia matumizi ya kila siku ya fedha za familia, na wakati mwingine wanaweka kumbukumbu ya matumizi ya fedha ambayo wakati fulani wanaume wanaweza kuona ni madogo madogo na yasiyo na umuhimu mkubwa. Kutokana na sababu hii wasichana wa China toka wanapokuwa watoto wanafundishwa kusimamia fedha za familia. Na uhodari wao katika hilo, ni moja ya msingi wa hali bora ya familia. Jukumu kubwa la wanaume ni kufanya kazi ya kuchuma pesa.
    • China yaufanya michezo wa soka kuwa somo rasmi shuleni
    • Beijing yatoa rasimu ya agizo kuhusu majina ya miji na mitaa hapa Beijing
    Katika siku za karibuni serikali ya mji wa Beijing ilitoa rasimu ya agizo kuhusu majina ya miji na mitaa hapa Beijing. Rasimu hiyo inataka kupiga marufuku majina ya viongozi, majina ya kigeni au maneno machafu kuwa majina ya mitaa, lakini vilevile inahimiza majina ya kale yalindwe na kuhifadhiwa, na majina ya sehemu mpya yasitukuzwe sana.
    • Kujisomea kuna manufaa makubwa kwa jamii yote
    • Pilikapiliya ya maandalizi ya mwaka mpya wa jadi wa China
    • Hali ya masikilizano ya kidini nchini China
    Wiki hii ni wiki ya masikilizano ya kidini duniani, wiki iliyotajwa na Umoja wa Mataifa kuwa ya wiki ya kuhimiza watu duniani kuishi kwa masikilizano bila kujali tofauti za kidini, na kukumbuka madhara yaliyotokea na yanayoweza kutokea kutokana watu kutowavumilia wenzao kwa dini au imani tofauti. China ni nchi yenye makabila 56, dini zaidi ya tano, na makundi mengine mbalimbali yenye imani za jadi, lakini ni nchi yenye kiwango cha juu cha masikilizano. Tutawafahamisha ni vipi wenzetu wanaweza kuwa na masikilizano katika hali ya kuwa na idadi kubwa ya watu, makabila mengi na dini mbalimbali.
    • Utamaduni wa kunywa kahawa nchini China
    Katika hali ya kawaida wachina ni watu wanaopenda kunywa chai. Kahawa naweza kusema ni utamaduni wa kigeni kabisa kwao, lakini kwa sasa ukiwa hapa China na hasa kwenye miji mikubwa, karibu kila mahali kuna migahawa ya chai. Karibu migahawa yote ni ya kimagharibi kama vile Starbucks, Costa coffee na mingine. Kwa hiyo kwa upande fulani tunapozungumzia unywaji kahawa hapa China hatuzungumzii utamaduni wa jadi wa China, tunazungumzia utamaduni ambao ndio unaanza kuenea.
    • Masikilizano ya kijamii na jinsi yanavyohimizwa katika sehemu za kazi na kwenye miji mbalimbali
    China inafahamika kuwa ni nchi kubwa na yenye watu wengi. Kwa nchi kubwa na yenye watu wengi kama China, lingekuwa ni jambo la kawaida kukumbwa na changamoto na misukosuko inayotokana na migongano wakati wa maingiliano ya watu. Lakini kati hali ambayo inawashangaza wengi, China ni nchi ambayo imetulia sana. Kuna baadhi ya sehemu chache tu korofi, ambazo changamoto hutokea hapa na pale.
    • Msichana mmoja na maisha yake ya matumizi ya Internet
    Hapa China kuna dada mmoja anaitwa Chen Xiao, yeye huwa anapatikana kwenye internet kwa kuwafanyia watu kazi wanazotaka na anazoweza kufanya. Anatoza karibu dola moja na nusu kwa dakika 8, karibu dola 4 kwa nusu saa na karibu dola 15 kwa saa. Baadhi ya watu wameanza kujiuliza jinsi dada huyu alivyotumia akili na kutumia muda wake kwenye internet kwa faida na sio kupoteza muda.
    • Je ni nini tunaweza kujifunza kutoka wa China kwenye kupambana na magonjwa ya maambukizi
    Bila shaka wasikilizaji mnaofuatilia habari kuhusu China, na habari za mambo ya Afya. Mtakuwa mnakumbuka kuwa China iliwahi kutikiswa na homa ya mafua makali ya SARS, na baadaye ilisumbuliwa na homa ya mafua ya ndege. Nakumbuka wakati ule hofu ilikuwa kama jinsi ilivyo sasa kwenye nchi za Afrika kuhusu Ebola. Je ni nini tunaweza kujifunza kutoka wa China kwenye kupambana na magonjwa ya maambukizi, kuwa nasi tukufahamishe.
    • China yaandaa kwa mafanikio michezo ya Olimpiki ya vijana
    Leo katika kipindi hiki tuna mada ya michezo. Tunajadili mada hii baada China kuandaa kwa mafanikio michezo ya Olimpiki ya vijana, iliyofanyika mjini Nanjing, mkoani Jiangsu. Michezo ambayo iliwashirikisha vijana kutoka katika nchi karibu zote duniani, ikiwa ni pamoja na vijana kutoa nchi za Afrika Mashariki.
    • Changamoto inayowakabili baadhi ya vijana wa China kuhusu ndoa
    Leo katika kipindi hiki tunazungumzia changamoto inayowakabili baadhi ya vijana kuhusu ndoa. Kutokana na sababu mbalimbali kama vile elimu, uwezo mdogo kiuchumi, ajira na kutojua hali ya baadaye kiuchumi itakuwaje, kuna baadhi ya vijana, wavulana kwa wasichana, huwa wanachelewa kuingia kwenye ndoa. Baadhi ya wazazi na hata ndugu, wakiona kijana amefika umri fulani (bila kujali amejiandaa vipi kiuchumi) wanashinikiza vijana kuingia kwenye ndoa. Hali hii sio kama tu iko kwenye nchi za Afrika, hata hapa China tunapoishi hali iko hivyo.
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako