• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Siku ya manunuzi kwenye mtandao wa Internet
    Jana tarehe 11 mwezi wa 11 ilikuwa siku ya manunuzi kwenye mtandao wa Internet. Kwenye tovuti nyingi za manunuzi, bei za bidhaa zilishuka kwa kiasi kikubwa, hata punguzo la asilimia 50 na zaidi. Wachina wengi wamezoea kununua vitu kwenye mtandao wa Internet. Takwimu zilizotolewa na idara ya takwimu ya China zinaonyesha kuwa, mwaka jana thamani ya biashara kwenye mtandao wa Internet ya China ilifikia dola za kimarekani bilioni 2.6, ambayo ni ongezeko la asilimia 60 kuliko mwaka juzi.
    • Juhudi za elimu katika kupunguza umaskini
    Kuna msemo wa Kiswahili unaosema "elimu ni ufunguo wa maisha", na huu ndio kwa miaka mingi umekuwa ukitumika kuhimiza watu kuhusu elimu. Hapa China pia kuna msemo kama huo unaosema "ujuzi unabadilisha hatma ya mtu". Katika kipindi hiki tutaangalia hatua halisi na jinsi zinavyoweza kupunguza umaskini.
    • China yapambana na hali ya umaskini
    • China yakabiliwa na changamoto ya ongezeko la idadi ya wazee
    China ni nchi ambayo inakabiliwa na mabadiliko katika muundo wa idadi ya watu, kutokana na utekelezaji wa sera ya mtoto mmoja. Kuinuka kwa kiwango cha maisha na kuboreka kwa huduma za afya, wachina kwa sasa wanaishi kwa muda mrefu, hali ambayo imefanya idadi ya wazee iongezeke. Lakini ongezeko la idadi ya wazee limeleta changamoto nyingine, nayo ni namna ya kuwatunze wazee.
    • Wafanyakazi wahamiaji
    Kila ifikapo mwezi Oktoba haa wakati wa sikukuu ya taifa ya China, na kuendelea suala la wafanyakazi wahamiaji huwa linajitokeza tena na kuanza kuzungumzwa. Kwanza ni kutokana na na msongamano wa abiria kwenye vyombo vya usafiri, na baadaye mambo wanayokumbana nayo baadhi ya wafanyakazi wahamiaji. Katika kipindi hiki tutaangalia hali ilivyokuwa na maana hasa ya wafanyakazi wahamiaji tukilinganisha ilivyo na kwenye nchi za Afrika Mashariki.
    • Safisha safisha kwenye mtandao wa internet
    Hivi karibuni, wizara ya utamaduni ya China imetangaza safisha safisha kwenye mtandao wa internet. Safisha safisha hiyo inahusu kuondoa nyimbo zenye maudhui mabaya kutoka kwenye mtandao wa Internet. Wizara hiyo imetoa orodha ya nyimbo 120 zinazotukuza au kuchochea vurugu, uhalifu au kuvuruga maadili ya jamii. Katika kipindi hiki, tunawafahamisha wasikilizaji kuhusu juhudi na changamoto za China katika kusimamia usafi wa mtandao wa Internet, na kufanya usiwe uwanja wa kukiuka haki miliki za wengine au kuvuruga maadili ya jadi.
    • Utaratibu wa Elimu wa China
    Wiki hii msikilizaji shule zimefunguliwa hapa China, wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na hata wa vyuo wameanza masomo yao. Kama tulivyowahi kukufahamisha katika siku za nyuma, utaratibu wa elimu hapa China ni tofauti na utaratibu wa elimu katika nchi zetu.
    • Wasikilizaji na walimu wa Afrika wanavyoona elimu hapa China
    Baada ya vipindi vitatu vilivyotangulia, tutakuwa na maoni kutoka kwa wasikilizaji na walimu kuhusu shule zinavyoendeshwa hapa China. Mwalimu mmoja wa Nairibo anaongea mambo manne kuhusu nidhamu na usimamizi wa nidhamu shuleni. Kwa undani zaidi hebu sikilize kipindi chetu.
    • Mbinu za ufundishaji za walimu wa China
    Kuna filamu moja iliyooneshwa na televisheni ya BBC iliyopewa jina "Je watoto wetu ni wakakamavu?". Filamu hiyo inaonesha walimu watano wachina waliokwenda kuwafundisha watoto 50 wa Uingereza kwa muda wa mwezi mmoja katika shule moja ya mji wa Hampshire. lengo lilikuwa ni kuangalia kama wanafunzi hao wako sawa na wenzao katika shule za Uingereza na kuangalia kama njia ya ufundishaji ya walimu wachina inaongeza uwezo wa wanafunzi kimasomo.
    • Nidhamu ya shuleni
    Wanafunzi wanapokuwa darasani hapa China, wanatakiwa kumsikiliza mwalimu. Kuna tofauti kidogo kati ya jinsi watoto kwenye nchi za Afrika wanavyofundishwa na jinsi wanavyofundishwa hapa China. Hapa China mara nyingi mwalimu anaongea mwanafunzi anasikiliza, hakuna nafasi ya kutosha kwa mwanafunzi kumkatisha mwalimu na kuuliza swali, japo mwalimu anaweza kuwauliza maswali wanafunzi.
    • Hadhi na mchango wa mapambano ya wachina dhidi ya uvamizi wa Japan katika vita dhidi ya ufashisti duniani
    Leo ni siku ya maadhimisho ya miaka 70 tangu China ipate ushindi kwenye vita ya kupambana na wavamizi wajapan. Katika kuadhimisha ushindi huo, China leo imefanya gwaride kubwa leo asubuhi hapa Beijing. Ushindi huo msikilizaji ulipatikana baada ya mapambano makali yaliyodumu kwa miaka 14, na kusababisha hasara kubwa ya mali na maisha ya watu, wengi wakiwa raia wa kawaida.
    • Umuhimu wa michezo katika jamii ya China
    Wakati mashindano ya kimataifa ya michezo ya riadha IAAF yanaendelea kufanyika hapa Beijing, kumekuwa na hali ya kutofurahisha kwa wachina, kwa kuwa tangu mwanariadha Liu Xiang atikise ulimwengu wa mbio fupi, bado hajatokea mwanariadha mwingine mchina aliyeweza kutwaa medali ya dhahabu kwenye mbio fupi na hata mbio ndefu. Japokuwa wanamichezo wa China wameonesha uhodari kwenye michezo mingine, kutong'ara kwenye mbio kunawafanya baadhi ya wachina wasiwe na furaha.
    • Mji wa Zhengzhou-Mji mkubwa ulioko katikati wa China
    Mji wa Zhengzhou ulioko katikati ya China. Mji huu wenye historia ndefu umekuwa ni mji wenye maendeleo ya kasi, na sasa unaendelea kukua kuwa moja kati ya miji ya kisasa na wenye nguvu ya ushindani. Wiki hii ni wiki ya matangazo ya redio na maonyesho ya picha za mji wa Zhengzhou. Uzinduzi wa wiki hiyo umefanyika mjini Nairobi, Kenya. Mwezetu Ronald Mutie alibahatika kutembelea mji huo. Kwenye kipindi hiki atatufahamisha zaidi kuhusu historia, mambo yalivyo sasa ya mji huo na hata wenyeji wanaelezaje ni mambo gani yanapatikana kwenye mji huo.
    • Chakula cha ulaji
    China ni moja ya nchi zinazotajwa kuwa na utamaduni wa muda mrefu wa vyakula, na ina vyakula vingi sana, lakini kwa muda mrefu wachina wamekuwa wakitajwa kuwa ni watu wenye miili mizuri, kwa maana ya kuwa si wanene na si wembamba, na wana desturi nzuri za kula. Lakini katika miaka ya hivi karibuni kumeanza kuwa na matatizo.
    • Umuhimu wa reli ya TAZARA katika uhusiano kati ya China na Afrika
    Mwaka huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 45 tangu reli ya TAZARA ianze kufanya kazi. Hivi karibuni kitabu maalum kuhusu reli ya TAZARA kilizinduliwa kwenye hafla iliyohudhuriwa na maofisa wa China na wengine kutoka Tanzania na Zambia.
    • Huduma mpya ya Taxi
    Huduma ya Taxi ya Uber, iliyoanzishwa na kampuni ya Uber ya California Marekani, ambayo kwa sasa imeenea kwenye nchi zaidi ya 50 duniani. Huduma hii inamfanya mteja yoyote mwenye simu ya mkononi aina ya smartphone, kutumia application maalumu kwenye simu ya mkononi kuita taxi na kuelekeza muda na mahali pa kumfuata.
    • Tatizo la dawa za kulevya nchini China
    Mwisho mwa mwezi uliopita, serikali ya China ilitoa ripoti ya kwanza kuhusu hali ya tatizo la dawa za kulevya. Ripoti hiyo inaeleza ukubwa wa tatizo, changamoto zake na juhudi zinazofanywa na serikali ya China na jamii ya China kwa ujumla kupambana na tatizo hili.
    • Ugonjwa wa Simu
    Kwa sasa matumizi ya internet kwa njia ya simu ni jambo lililozoeleka karibu katika miji mingi ya Afrika. Hapa China matumizi ya internet kwa njia ya simu yanaendelea kubadilika kila kukicha, na sasa imefikia kasi kuwa watu wana uraibu wa internet na wengine ni kama hawezi hata kuacha simu zao.
    • Treni ya kasi ya China
    Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, mtandao wa reli ya kasi hapa China umefikia zaidi ya kilometa elfu 16, na umepita kwenye mikoa 28 kati ya mikoa yote 33 ya China.Kwenye kipindi hiki tunazungumzia Treni ya kasi ya China na inavyobadilisha maisha ya watu, iwe ni kwa mambo ya kijamii au kwa mambo ya kiuchumi.
    • Matunzo ya uzeeni
    Kutokana na maendeleo ya huduma za afya, lishe na hata maisha kwa ujumla, kwa sasa wachina wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko zamani. Lakini kutokana na mchanganyiko wa mabadiliko ya muundo wa familia za China na ongezeko la idadi ya wazee, jamii ya China imefikia hatua ya kuanza kuangalia namna ya kuwatunza wazee, hasa wale ambao umri wao ni mkubwa sana na hawawezi kujitunza, hali ambayo ni tofauti na mfumo wa jamii wa jadi yaani kutunzwa na wanafamilia.
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako