3: Uchumi wa China

Hali ya Uchumi wa China

Tangu kuasisiwa China mpya mwaka 1949, uchumi wa China ulikuwa na maendeleo ya haraka. Hususan baada ya kufanya mageuzi na ufunguaji mlango kwa nje mwaka 1978, uchumi wa China ulikuwa na wastani wa ongezeko la zaidi ya 9% kwa mwaka. Mwaka 2003, jumla ya thamani ya uzalishaji mali nchini ilifikia dola za kimarekani trilioni 1 na bilioni 400, na uchumi wa China ulichukua nafasi ya sita duniani ikizifuata Marekani, Japan, Ujerumani, Uingereza na Ufaransa. Hadi kufikia mwishoni mwaka 2003, wastani wa thamani ya uzalishaji mali wa nchini wa kila mtu ulizidi dola za kimarekani 1,000.

Hivi sasa, hali ya uwekezaji na ununuzi nchini imekuwa ni nzuri zaidi. Mwaka 2003, thamani ya uwekezaji wa mali zisizohamishika ulizidi Yuan za Renminbi zaidi ya trilioni 5.5; jumla ya mauzo ya bidhaa ilikaribia Yuan za Renminbi trilioni 4.6; thamani ya biashara ya nje ilikuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 850, ikichukua nafasi ya nne duniani kwa ikizizidi Uingereza na Ufaransa, na kuzifuatia Marekani, Ujerumani na Japan. Hadi mwishoni mwa mwaka 2003, akiba ya fedha za kigeni ya China ilizidi dola za kimarekani bilioni 400, ikichukua nafasi ya pili ikiifuata Japan.

Baada ya kufanya mageuzi, ufunguaji mlango na ujenzi wa kisasa kwa zaidi ya miaka 20, China imemaliza hatua za kuelekea utaratibu wa uchumi wa kimasoko wa kiujamaa kutoka uchumi wa kimpango. Utaratibu wa uchumi wa kimasoko wa kiujamaa umejengwa na kukamilishwa hatua kwa hatua. Kutokana na hali hiyo, sheria na kanuni za China pia zimekamilishwa hatua kwa hatua, kiwango cha ufuanguaji wa masoko kimekuwa kikiongezeka mwaka hata mwaka, mazingira ya uwekezaji yameboreshwa bila kusita na mageuzi ya mfumo wa mambo ya sarafu yanaendelezwa kwa hatua madhubuti, hali ambayo imeweka dhamana kwa maendeleo ya uchumi taifa.

Baada ya kuingia karne mpya, China inafuata nadharia ya kuwa na maendeleo ya pande zote na uwiano kati ya binadamu na maumbile, kati ya binadamu na jamii, kati ya miji na vijiji, kati ya sehemu ya mashariki na sehemu ya magharibi na kati ya uchumi na jamii. Mwaka 2002, mkutano mkuu wa 16 wa chama cha kikomunisti cha China uliweka lengo la kujenga jamii yenye maisha bora zaidi hadi ifikapo mwaka 2020.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12