3: Uchumi wa China

Miradi Mikubwa

Mradi wa Magenge Matatu

Mto Changjiang una rasimali kubwa ya maji, mradi wa maji wa Magenge Matatu ni mradi muhimu wa kupunguza tatizo la maji na kustawisha mto Changjiang. Mradi wa Magenge Matatu uko katika sehemu ya Sandouping, ya mji wa Yichang, mkoa wa Hubei, sehemu ya kati ya mto Changjiang. Katika sehemu hiyo Mto Changjiang ni mpana, chini yake kuna mawe magumu na makubwa ya granite, yanayoweza kudhibiti maji ya sehemu ya juu ya mto yenye eneo la kilomita za mraba 100, ambapo maji yanayopita huko ni mita za ujazo karibu bilioni 500 kwa mwaka.

Ujenzi wa mradi wa maji wa Magenge Matatu unatumia mpango wa kukamilishwa moja kwa moja, kulimbikiza maji kwa viplindi mbalimbali, na kuhamisha wakazi hatua kwa hatua. Sehemu ya juu ya ukingo wa maji ya bwawa ina urefu wa mita 3,035, maji baada ya kulimbikizwa katika hali ya kawaida ni yanakuwa na kina cha mita 175. Bwawa la maji la mradi huo linaweza kulimbikiza jumla ya mita za ujazo bilioni 39.3.

Baada ya ujenzi wake kukamilika, mradi wa Magenge Matatu utakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mafuriko, kuzalisha umeme, kuendeleza uchukuzi, ufugaji samaki, utalii, kuhifadhi mazingira ya asili, kuboresha mazingira, kuhamisha wakazi katika maeneo ya ustawishaji, kupeleka maji kutoka sehemu ya kusini kwenda sehemu ya kaskazini na kumwagilia maji mashamba.

Mradi wa Kupeleka Maji Kaskazini Kutoka Kusini

Sehemu ya kusini ya China Ina maji mengi, lakini sehemu ya kaskazini ina upungufu wa maji. Ili kupeleka maji ya sehemu ya kusinii kwa sehemu ya kaskazini yenye ukame, wanasayansi na wahandisi wa China walifanya uchunguzi na upimaji porini kwa miaka 50.

Maji ya sehemu ya kusini yanapelekwa sehemu ya kaskazini kwa njia tatu za mashariki, kati na magharibi, ambazo zinakutana na mito minne mikubwa ya Changjiang, Manjano, Huai na Hai, ili kugawa rasilimali ya maji kufuatana na hali halisi.

Njia ya mashariki: kuchukua maji ya mto Changjiang katika mji wa Yangzhou, ulioko sehemu ya chini ya mto Changjiang, kupelekwa sehemu ya kaskazini kwa kupitia mfereji kati ya Beijing na Hangzhou na mito mingine inayokwenda sambamba nao, na kuungana na maziwa ya Hongze, Luoma, Nansi na Dongping. Maji yanayoletwa kutoka sehemu ya kusini yatapelekwa kwa njia mbili ndogo, ambazo moja ni inaelekea sehemu ya kaskazini kupitia mto Manjano; na njia nyingine inaelekea upande wa mashariki hadi Yantai na Weihai, mkoani Shandong.

Njia ya katikati inachukua maji kutoka bwawa la maji la Danjiangkou, kuelekea sehemu ya kaskazini sambamba na njia ya reli kati ya Beijing na Guangzhou hadi miji ya Beijing na Tianjin.

Njia ya magharibi ni kuchukua maji kutoka bwawa la maji litakalojengwa karibu na mto Tongtian, tawi la mto Yalong na mto Dadu katika sehemu ya juu ya mto Changjiang, na kuyapeleka hadi sehemu ya juu ya mto Manjano. Uwezo wa kupeleka maji kwa njia hizo tatu ni mita za ujazo bilioni 44.8 katika mwaka 2050, ambazo njia ya mashariki ni mita za ujazo bilioni 14.8, njia ya kati ni bilioni 13 na ya magharibi ni mita za ujazo bilioni 17.

Ujenzi wa mradi huo wa kupeleka maji unafanywa kwa vipindi tofauti kufuatana na hali halisi. Hivi sasa ujenzi umeanza katika sehemu nne za njia za mashariki na kati.

Mradi wa Reli ya Qinghai na Tibet

Reli kati ya Qinghai na Tibet yenye urefu wa kilomita 1,118, inaanzia sehemu ya Geermu ya mkoa wa Qinghai hadi mji wa Lhasa, mkoani Tibet. Reli kati ya Qinghai na Tibet ni reli ndefu kabisa kujengwa katika uwanda wa juu, ambayo kilomita 965 kati yan 1,118 zinapita kwenye uwanda wa juu wenye mita 4,000 kutoka usawa wa bahari. Sehemu ya kuingia mlima wa Tanggula ina urefu wa mita 5,072 kutoka usawa wa bahari.

Hatua ya kwanza ya ujenzi wa reli kati ya Qinghai na Tibet, ambao ni kati ya mji wa Xining na Geermu ulianza zamani, hatua ya pili ya ujenzi kati ya Geermu na Lhasa ulizinduliwa rasmi mwezi Februali mwaka 2001. Hivi sasa, kazi za kutandika reli kwa umbali wa kilomita 317 imemalizika, ikiwa ni 28.6% ya jumla urefu wa reli hiyo.

Matatizo makubwa kwenye ujenzi wa reli hiyo ni kupita kwenye ardhi yenye barafu kutokana na baridi kali kwenye uwanda wa juu, licha ya hayo, sehemu nyingi inazopita reli hiyo, ni mahali kwenye mabonde na chini kuna maji maji na majani, pamoja na sehemu ambazo huchukuliwa na wenyeji kuwa ni sehemu zisizopitika kwenye uwanda wa juu. Ili kuhifadhi majani na miti ya huko, ujenzi wa reli katika sehemu hiyo umegawanyika katika vipindi vingi, na kupanda majani na miti iliyohamishwa kutoka sehemu nyingine. Kwa sehemu zenye mazingira bora zilizoko kusini mwa mlima wa Kunlun, wafanyakazi wanapanda majani kwa kusambaza mbegu nzuri za majani yanayofaa kwa huko, na kufunika ardhi kwa karatasi za plastiki ili kuziwezesha mbegu za majani kuchipuka haraka, na kufanya kando mbili za njia ya reli kufunikwa na majani.

Ujenzi unaofanyika kwenye sehemu zenye urefu wa kilomita 550 za udongo ulioganda kutokana na baridi, hatua nyingi za kiteknolojia zimechukuliwa zikiwa ni pamoja na kutandika vitu vinavyohifadhi joto, reli inayopita kwenye daraja refu na kujenga matuta ya reli yanayopitika katka hali yoyote ya hewa, ili kuhifadhi kadiri iwezavyo mazingira yenye ardhi inayoganda barafu.

Ili kuhifadhi rasilimali za wanyama na mimea ya hifadhi za kimaumbile za Kekexili, Chanzo cha Mito Mitatu na Qiangtang, mahandaki na madaraja yanajengwa katika sehemu wanazopita wanyama. Magari moshi ya abiria yanayopita huko, takataka zinazuiliwa ndani ya magari, isipokuwa zinashushwa katika baadhi ya sehemu maalumu zilizoko kando kando za njia ya reli.

Sehemu muhimu za mfumo wa kuleta joto zilizoko katika vituo muhimu vya magari moshi vya reli hiyo, lazima vitumie mafuta ya dizeli au nishati nyingine safi zinazotokana na jua na upepo. Maji machafu yanayotokea majumbani hayaruhusiwi kutolewa kabla ya kusafishwa kwanza.

Mradi wa Kupeleka Gesi

Gesi ya sehemu ya magharibi inayotoka katika mikoa ya Xinjiang, Qinghai, Sichuan na ukanda wa Eerduosi, inatarajiwa kupelekwa sehemu ya mashariki ya delta ya mto Changjiang.

Sehemu za kati na magharibi za China kuna mabonde 6 yenye mafuta ya asili ya petroli na gesi, ambayo ni pamoja na Talimu, Zhengeer, Duha, Chaidamu, Eerduosi na Sichuan. Rasilimali za gesi zinakadiriwa kuwa ni mita za ujazo bilioni 2.24 na kuchukua 58.9% ya jumla ya rasilimali za gesi ya China, ambayo ni mita za ujazo trilioni 3.8. Kutokana na hali ya rasilimali za gesi, pamoja na uchunguzi na upimaji wa hivi sasa, serikali imeamua kuanzisha ujenzi wa mradi wa kupeleka gesi ya sehemu ya magharibi kwenye sehemu ya mashariki, kuharakisha ujenzi wa kutandika mabomba ya kupelekea gesi, licha ya kujenga njia ya mabomba ya kupelekea gesi kutoka mkoa wa Shanxi katika sehemu ya Beijing, zitajengwa njia 3 za kupelekea gesi ya asili kutoka Talimu kwenda Shanghai, kutoka Sebei ya mkoa wa Qinghai kwenda Xining na Lanzhou, na kutoka wilaya ya Zhong ya Chongqing kwenda mji wa Wuhan mkoani Hubei, ili kubadilisha hali bora ya rasilimali kuwa hali bora ya uchumi na kukidhi mahitaji ya haraka ya sehemu ya mashariki kwa gesi ya asili. Aidha, kutokana na mpango unaobuniwa hivi sasa, mabomba ya kupelekea ges kutoka Seberia ya magharibi ya Russia, yataungana na mabomba makubwa ya kupeleka gesi ya mradi wa kupeleka gesi ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki. Mbali na hayo, mpango mwingine unabuniwa hivi sasa wa kuchukua gesi ya Seberia ya mashariki ya Russia, nchi hizo pia zinahesabiwa kama ni kupeleka gesi ya sehemu ya magharibi katika sehemu ya mashariki.

Kwa namna nyingine, kupeleka gesi ya sehemu ya magharibi katika sehemu ya mashariki ni mradi wa kupeleka gesi kutoka sehemu ya Talimu ya mkoa wa Xinjiang katika delta ya mto Changjiang ya Shanghai. Njia hiyo ya mabomba, ambayo ina urefu wa kilomita 4,200, na mabomba yenye mpenyo milimita 1118, inapitia mikoa 8 ikiwemo Xinjiang, Jiangsu na mji wa Shanghai, uwezo wake wa kupeleka gesi ni mita za ujazo bilioni 12, na kugharimiwa Yuan bilioni 120.

Hivi sasa, ujenzi wa mradi wa kupeleka gesi umekamilishwa kwa 48%, na ujenzi wa sehemu ya mashariki ya njia ya mabomba umekamilika kabisa, na kuanza kupeleka gesi ya asili sehemu ya mashariki ya China.

Mradi wa Kupeleka Umeme

Mradi wa kupeleka umeme kutoka sehemu ya magharibi kwenda sehemu ya mashariki ni mradi kwa ajili ya kupeleka umeme mwingi kutoka sehemu ya magharibi kwenda sehemu iliyoendelea ya mashariki. Kwa kuwa sehemu nyingi za uzalishaji wa umeme ziko katika sehemu za magharibi na kaskazini, lakini matumizi ya nishati ya umeme yako katika sehemu zilizoendelea za kandokando ya reli kati ya Beijing na Guangzhou na upande wa mashariki ya njia hiyo ya reli.

Mradi wa kupeleka umeme wa magharibi katika sehemu ya mashariki ni wa kujenga njia tatu za kupleleka umeme za kaskazini, katikati na kusini.

Njia ya kaskazini ni pamoja na mifumo ya umeme ya kaskazini mashariki, kaskazini , Shandong na kaskazini magharibi, hususan kuzalisha umeme kwa nguvu za maji katika sehemu ya kaskazini magharibi na kupeleka umeme kwa mifumo ya umeme ya Beijing, Tianjin,Hebei na Shandong.

Njia ya katikati ni pamoja na mifumo ya umeme ya sehemu za mashariki, katikati, Sichuan, na Fujian, hususan kuzalisha umeme kwa nguvu za maji ya mto Changjiang, na kupeleka umeme kwa sehemu za katikati, mashariki na Fujian, ambazo ni sehemu kubwa ya kupelekwa umeme kutoka sehemu ya magharibi, na kuleta athari kubwa kwa mfumo wa umeme wa nchi nzima.

Njia ya kusini ya kupeleka umeme ni kuzalisha umeme kwa nguvu za maji za mto Wu ulioko mkoani Guizhou, mto Lancang na mto mwekundu ulioko mkoani Yunnan, pamoja na umeme unaozalishwa na kiwanda cha umeme cha Kengkou cha mikoa miwili ya Yunnan na Guizhou na kupeleka umeme kwenye sehemu za mkoa wa Guangdong. Mradi wa kupeleka umeme kutoka sehemu ya magharibi katika sehemu ya mashariki ni mradi mkubwa nchini China, na ni sehemu muhimu ya mkakati uliotolewa na serikali ya China wa kustawisha sehemu ya magharibi, ambayo inaunganisha rasilimali nyingi za sehemu ya magharibi na masoko makubwa ya sehemu ya mashariki, na itachangia maendeleo makubwa ya sekta ya uzalishaji wa umeme na uchumi wa taifa.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12