3: Uchumi wa China

Mfumo wa Mambo ya Fedha

Benki na Usimamizi Wake

Hivi sasa China imejenga mfumo wa mambo ya fedha ambao Benki Kuu inafanya udhibiti na usimamizi, benki za taifa ni uti wa mgongo, mambo ya fedha ya kisiasa kuachana na mambo ya fedha ya kibiashara, kuwa na uhusiano wa ushirikiano na kusaidiana kati ya mifumo mbalimbali ya mambo ya fedha.

Benki ya Umma ya China, ambayo ilikwa ni Benki Kuu nchini China, inafanya udhibiti na usimamizi wa sekta ya mambo ya fedha ya China. Benki nne za Viwanda na Biashara, China, Kilimo ya China na Ujenzi ni benki za biashara za taifa. Licha ya benki hizo, China pia imeanzisha benki tatu za kisiasa ambazo ni za maendeleo ya kilimo, ustawishaji wa taifa na usafirishaji nje na uagizajia wa bidhaa wa taifa. Mwaka 1995, China ilitekeleza "Sheria ya benki za biashara" ambayo iliweka mazingira ya uanzishaji wa mfumo wa benki za biashara na mashirika ya mambo ya fedha, na kutoa mujibu wa kisheria kwa benki maalumu za taifa kubadilika kuwa benki za biashara za taifa. Tokea mwaka 1996, mfumo wa mambo ya fedha uliimarishwa na kuboreshwa hatua kwa hatua, benki za biashara za taifa ziligeuzwa kuwa mashirika ya mambo ya fedha ya kisasa, kuongeza na kurekebisha benki zaidi ya 120 za wastani na ndogo za utaratibu wa hisa, kunyoosha na kuendeleza mashirika ya sekta ya fedha, yakiwa ni pamoja na ya soko la vyeti vya hisa na bima.

Kamati ya usimamizi ya sekta ya benki ya China ni idara ya usimamizi ya benki za China. Tarehe 28, Aprili, mwaka 2003 ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake, ambayo ni kubuni utaratibu na kanuni za usimamizi wa mashirika ya fedha yanayohusika na sekta ya benki, kukagua na kuyadhibu yale yanayokiuka kanuni za kisheria.

Masoko ya Vyeti vya Hisa na Usimamizi Wake

Mwaka 1990 na mwaka 1991, China ilianzisha masoko ya vyeti vya hisa katika miji ya Shanghai na Shenzhen. Katika muda wa miaka zaidi ya 10, masoko hayo ya China yalipita katika njia ambayo nchi nyingi zilitumia miaka zaidi ya 100. Hivi leo, masoko hayo yamekuwa ni upinde unaobeba mitaji yenye thamani ya Yuan zaidi ya trioni 4, kampuni zaidi ya 1,200 za biashara ya vyeti vya hisa na wawekezaji zaidi ya milioni70.

Mwaka 1998, China ilianzisha kamati ya usimamizi ya masoko ya vyeti vya hisa, ikiwa ni idara ya serikali inayosimamia masoko ya vyeti vya hisa na bidhaa zitakazozalishwa inaongoza moja kwa moja vitengo vya mfumo wa masoko ya vyeti vya hisa na bidhaa zitakazozalishwa, kuimarisha usimamizi juu ya sekta ya masoko ya vyeti vya hisa na bidhaa zitakazozalishwa na kuongeza uhakika wa habari zinazotangazwa. Kwa wananchi, masoko ya vyeti vya hisa yamekuwa moja ya njia muhimu ya uwekezaji. Hivi sasa masoko ya vyeti vya hisa ya Shanghai na Shenzhen yanaongoza masoko hayo ya China. Mfumo wa upigaji wa hesabu wa biashara ya vyeti vya hisa umeenea kila sehemu nchini, hivi sasa biashara ya vyeti vya hisa imeweza kufanyika kwenye mtandao wa kompyuta na mbinu muhimu za kiteknolojia zimefikia kiwango cha kimaendeleo duniani. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, idadi ya masoko ya vyeti vya hisa nchini, ambayo ni pamoja na ya vyeti vya hisa vya aina za A na B, yamefikia 1287 kutoka 1224 ya mwishoni mwa mwaka uliotangulia, na jumla ya thamani ya hisa ilikuwa Yuan 42,578, ikiwa ni ongezeko la 11% kuliko lile la mwishoni mwa mwaka uliopita.

Bima na Usimamizi Wake

Shughuli za bima baada ya kuzorota kwa miaka 29, zilianza kurejea katika hali ya zamani toka mwaka 1980. Mwaka 1981, Shirika la Bima la China, ambalo hapo zamani ilikuwa idara moja ya serikali, lilianzisha matawi yake kutoka mikoa na miji inayodhibitiwa moja kwa moja na serikali kuu hadi wilaya. Kampuni za bima zinazojulikana kwa Usalama na Pasifiki, ambazo shughuli zake hasa ziko katika sehemu ya pwani ya China, zilianzishwa mwaka 1988. Mwaka 1996, Shirika la Bima la China lilipiga hatua moja kubwa katika kubadilisha utaratibu wa usimamizi na uendeshaji wa kazi, na kuungana na masoko ya kimataifa. Kuanziashwa kwa "Sheria ya bima" mwaka 1985 na kuanzishwa kwa kamati ya usimamizi wa shughuli za bima ya China mwaka 1988, kumeweka mujibu wa sheria na kanuni za uendeshaji kazi kwa shughuli za bima nchini.

Hivi sasa, hapa nchini kuna kampuni za bima na wakala wa bima zaidi ya elfu 70, ambazo zimeanzishwa bima za uzeeni, afya, ajali na mali. Hivi sasa kuna kampuni za bima za kigeni zaidi ya 30 nchini China, wakati kampuni zaidi ya 100 za nchi za nje zimefungua ofisi zake nchini, zikitarajia kuingia katika soko la bima ya China. Katika mwaka 2003, pato la kampuni za bima za nchi za nje nchini China lilikuwa Yuan zaidi ya bilioni 388, likiwa ni ongezeko la 27.1%.

Fedha za Renminbi na Usimamizi wa Fedha za Kigeni

Fedha za Renminbi ni fedha za China zilizothibitishwa kisheria, ambazo zinatolewa na kusimamizwa na Benki ya Umma ya China. Kiasi cha kubadilisha fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni, kinathibitishwa na Benki ya Umma ya China, na kutangazwa na idara ya usimamizi wa fedha za kigeni ya taifa. Ubadiliishaji wa fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni, unadhibitiwa na serikali, na kutekelezwa na idara ya usimamizi wa fedha za kigeni ya taifa.

Mwaka 1994, China ilifanya mageuzi ya utaratibu wa fedha za kigeni, kufanya ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni kulingana na utaratibu wa kimataifa, ubadilishaji wa fedha za Renminbi na fedha za kigeni unashughulikiwa na benki na kuwa na utaratibu wa aina moja kwa shughuli za benki za China katika masoko ya fedha za kigeni. Kutokana na msingi huo, mwaka 1996 China iliweka mauzo ya fedha za kigeni ya kampuni au viwanda vilivyowekezwa na wafanyabiashara wa nchi za nje katika utaratibu wa shughuli za benki, na kutangulia kukubali kabla ya muda, kifungu cha nane cha mkataba wa Shirika la Sarafu Duniani kuhusu matumizi muhimu ya fedha za Renminbi yanaweza kubadilishwa kwa fedha za kigeni. Licha ya hayo, China imeshiriki na kukuza ushirikiano wa mambo ya fedha wa ubadilishanaji wa fedha wa pande mbili kati ya nchi za umoja wa Asia ya Kusini Mashariki na Japan na Korea ya Kusini. Hususan katika kipindi wakati mgogoro fedha wa Asia ulipozuka, si kama tu China ilishikilia kutopunguza thamani ya fedha za Renminbi, bali pia ilitoa misaada ya fedha kwa nchi zilizokumbwa na mgogoro ya fedha, na kuwa nguzo muhimu iliyohifadhi utulivu wa masoko ya fedha ya Asia.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, akiba ya fedha za kigeni ya China ilifikia dola za kimarekani bilioni 403.3, kiasi hiki ni ongezeko la dola za kimarekani bilioni 116.8 kulimo kile cha mwishoni mwa mwaka uliotangulia. Kiasi cha ubadilishaji kati ya fedha za Renminbi na fedha za kigeni kinatulia kinadumishwa katika hali ya utulivu.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12