3: Uchumi wa China

Hali ya Maisha Kiuchumi

Pato na Matumizi ya Wakazi

Ikiulinganishwa na miaka zaidi ya 50 iliyopita, kiwango cha maisha ya watu wa China kimeinuka sana, na hata ikilinganishwa na kile cha miaka zaidi ya 20 iliyopita, kimeinuka kwa udhahiri. Pato la watu linaongezeka kwa mfululizo, na mali zao pia zimeongezeka. Hivi sasa watu wa China wanatumia fedha zaidi katika kununua nyumba, magari, kompyuta, vyeti vya hisa na kwenda kutembelea nchi za nje.

Katika kipindi cha miaka zaidi ya 20 baada ya mwaka 1979, uchumi wa China ulipata maendeleo ya kasi, na pato la wakazi pia liliongezeka kwa haraka. Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kuwa wastani wa pato la wakazi wa sehemu za vijijini kwa mwaka 2002 ulifikia Yuan 2,476 kutoka Yuan 134 mwaka 1978, na wastani wa ongezeko la pato ulikuwa 7.2% kwa mwaka. Wastani wa pato la wakazi wa mijini ulifikia Yuan 7,703 kutoka Yuan 343, ambalo ni ongezeko la 6.7% kwa mwaka.

Mwaka 2003, maisha ya wakazi wa China yaliendelea kuboreshwa. Wastani wa pato la wakazi wa mijini ulikuwa Yuan 8,472. Na baada ya kuondoa mfumuko wa bei, ongezeko halisi lilikuwa 9%, wastani wa pato la wakazi wa vijijini ulikuwa Yuan 2,622 likiwa ni ongezeko la 4.3%, ambapo fedha za matumizi ya vyakula zilichukua 37.1% ya jumla ya matumizi ya fedha kwa wakazi wa mijini ambalo ni pungufu kwa 0.6%, wakati zile za wakazi wa vijijini zilikuwa 45.6%, ambalo ni pungufu kwa 0.6% pia. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana magari ya binafsi yalifikia milioni 4.89, likiwa ni ongezeko la magari milioni 1.46 kuliko yale ya mwaka uliotangulia.

Hivi sasa hali ya upungufu wa chakula na bidhaa zinazohitajika kwa matumizi ya kila siku, imetoweka kabisa. Mabadiliko ya matumizi ya fedha kwa wakazi yanaonesha kuwa fedha zinazotumika kununua chakula, nguo na mahitaji ya lazima zimepungua, lakini fedha zinazotumika katika kujiendeleza na kununua vitu vinavyoboresha maisha, kama vile nyumba, magari, simu za mikononi, matibabu na utunzaji wa afya, zinaongezeka haraka, na maisha ya wakazi yanaboreshwa hatua kwa hatua.

Dhamana ya Jamii

BIMA YA UZEENI

Katika miaka ya karibuni, bima ya uzeeni imekuwa ikiendelea kukua kwa haraka. Zamani bima hiyo iliwahusu wafanyakazi wa viwanda vya kserikali na ushirikika, lakini hivi sasa imekuzwa hadi kwa wafanyakazi wa viwanda vyote na idara zisizo za uzalishaji mali ambazo zinaendeshwa kama za uzalishaji wa mali. Hivi sasa haki za wafanyakazi wa viwanda visivyo vya kiserikali pia zimehakikishwa. Hadi mwishoni mwa mwaka 2002, nchini China kulikuwa na wafanyakazi milioni 111.29, na wastafu milioni 36.08, ambao walishiriki bima ya uzeeni. Na ilipofika mwishoni mwa mwaka 2003, idadi ya watu walioshiriki kwenye bima ya uzeeni ilikuwa milioni 154.90, likiwa ni ongezeko la milioni 7.53.

BIMA AFYA

Bima ya afya kimisingi imefikia viwanda na idara zote zisizo za uzalishaji wa mali, ofisi za serikali na makundi katika jamii ya mijini. Bima ya aina hiyo ni moja ya bima za jamii inayoendelezwa katika maeneo makubwa. Katika mwaka 2002, idadi ya hospitali, zahanati na vituo vya kuzuia maambukizi ya maradhi nchini China ilifikia laki 2.9, vitanda vya wagonjwa milioni 3.21, pamoja na madakatari na wauguzi milioni 4.44. Katika miji mikubwa kama ile ya Beijing, Shanghai, Tianjin na Chongqing, kuna hospitani za hali ya juu za kansa, ugonjwa na moyo na mishipa ya damu, macho, meno, tiba za jadi ya China, maradhi ya kuambukiza, hospitali maalumu za aina mbalimbali. Katika miji ya wastani ya mikoa, kuna hospitali zenye zana za kisasa na hospitali maalumu. Hivi sasa, katika sehemu ya vijijini kuna mfumo wa utibabu wa ngazi za wilaya, tarafa na vijiji. China ina hozpitali za ngazi ya wilaya zaidi ya 2,000 pamoja na zahanati elfu 48 za tarafa.

Katika mwisho wa mwaka 2003, idadi ya watu walioshiriki bima ya utibabu ilikuwa milioni 108.95, likiwa ni ongezeko la milioni 14.94, ambao milioni 79.77 ni wafanya kazi, na milioni 29.18 ni wastafu kazi.

BIMA YA KUKOSA AJIRA

China ni nchi yenye idadi kubwa ya watu, hivyo inakabiliwa shinikizo kubwa la ajira. Ili kupunguza tatizo la ajira, toka mwaka 1993, serikali ya China ilitekeleza sera za soko la nguvu-kazi, kutafuta njia za kuongeza ajira. Serikali ya China ilianzisha mradi wa kuwapatia kazi wafanyakazi waliopunguzwa kutoka viwanda vya kiserikali kutokana na marekebisho ya muundo wa uzalishaji mali. Hadi mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya watu wenye ajira katika miji yote nchini ilikuwa milioni 247.80,. Toka mwaka 1998, zaidi ya wafanyakazi milioni 18 waliopunguzwa kutoka kwenye viwanda vya serikali, walipata ajira mpya kwa njia za mbalimbali. Mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya watu waliokosa ajira ilikuwa kiasi cha 4%. Kufuata utaratibu wa bima ya kukosa ajira katika idara mbalimbali zisizo za uzalishaji mali, kumehimiza uhamiaji mwafaka wa nguvukazi na kuanzishwa kwa soko la nguvukazi. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2003, idadi ya watu walioshiriki kwenye bima ya kukosa ajira nchini China ilikuwa milioni 103.73. Miji yote nchini ikiwa ni pamoja ya ngazi ya wilaya, imefuata utaratibu wa dhamana ya kiwango cha chini cha maisha, ambao unatoa dhama ya maisha ya kiwango cha chini kwa wakazi wa mijini ambao pato lao ni chini ya kiwango cha chini katika miji wanayoishi. Mwaka 2003, wakazi milioni 22.35 wa mijini walipata dhamana ya maisha ya kiwango cha chini. Hivi sasa utaratibu huo umetatua shida ya wakazi maskini wa miji ya China.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12