3: Uchumi wa China

Utaratibu wa Uchumi wa Kimasoko wa Ujamaa

Miaka 30 baada ya China mpya kuasisiwa mwaka 1949, serikali ya China ilianza kufuata utaratibu wa uchumi wa kimasoko, ambao idara za wataalamu za serikali zinabuni na kuweka malengo ya maendeleo ya kiuchumi ya sekta mbalimbali. Utaratibu huo unaweza kukuza uchumi wa China kuelekea kwenye malengo yake, lakini pia ulizuia kutokea uwiano mbaya kati ya uchumi na kasi ya maendeleo.

Mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, China ilianza kufanya mageuzi ya utaratibu wa uchumi. Mwaka 1978, China ilianzisha utaratibu wa kuziwajibisha familia za wakulima vijijini katika kandarasi ya uzalishaji nafaka. Mwaka 1984, mageuzi ya utaratibu wa uchumi ya vijijini yalienea hadi mijini. Mwaka 1992, China ilithibitisha mwelekeo wa mageuzi ya utaratibu wa uchumi wa kimasoko.

Mwezi Oktoba mwaka 2003, China ilithibitisha wazi lengo na jukumu ya kukamilisha utaratibu wa uchumi wa kimasoko wa ujamaa, ambayo ni pamoja na kutumia vilivyo uwezo wa kimsingi wa masoko katika ugawaji wa rasilimali, kuimarisha nguvu ya viwanda, udhibiti wa mpango mkuu wa taifa, kuboresha kazi za serikali za usimamizi wa jamii na utoaji huduma kwa umma kwa kufuata maendeleo ya uwiano kati ya miji na vijiji, kati ya kanda na kanda, kati ya uchumi na jamii, kati ya binadamu na maumbile, kati ya maendeleo ya nchini na utashi wa maendeleo ya nchini na ufunguaji mlango kwa nje, ili kuweka uhakikisho wa kimfumo kwa ujenzi wa pande zote wa jamii yenye maisha bora. Majukumu muhimu ni kuboresha utaratibu wa kimsingi wa uchumi, ambao umilikaji wa vyombo vya uzalishaji mali wa umma ni uti wa mgongo na kuweko maendeleo ya pamoja ya umilikaji wa aina mbalimbali; kujenga mfumo unaonufaisha kubadilisha hatua kwa hatua muundo wa uchumi wa aina mbili za miji na vijiji; Kuunda mfumo unaohimiza maendeleo ya uwiano ya uchumi wa kikanda; Kujenga mfumo bora wa masoko ya kisasa wenye ufunguaji mlango na ushindani; Kuboresha mfumo wa udhibiti wa mpango mkuu wa taifa, utaratibu wa usimamizi wa kiserikali na utaratibu wa sheria ya uchumi; Kuboresha utaratibu wa ajira, ugawaji wa mapato na huduma za jamii; na kujenga mfumo unaohimiza maendeleo endelevu ya uchumi na jamii. Kutokana na mpango uliowekwa, hadi mwaka 2010 China itamaliza kujenga utaratibu kamili wa uchumi wa masoko wa ujamaa; na itakapofika mwaka 2020, itamaliza kujenga utaratibu halisi wa uchumi wa masoko wa ujamaa.

Muundo wa Utaratibu wa Umilikaji wa Vyombo Vya Uzalishaji Mali   

Kutokana na katiba ya China, katika kipindi cha mwanzo cha ujamaa, China ilishikilia utaratibu wa kimsingi wa uchumi ambao umilikaji wa vyombo vya uzalishaji mali wa umma ni uti wa mgongo na kuweko maendeleo ya pamoja ya umilikaji wa aina mbalimbali, kushikilia utaratibu wa ugawaji wa mapato ambao ugawaji wa mapato kutokana na kazi zilizofanyika ni njia kuu ya ugawaji wa mapato wa aina mbalimbali. Hivi sasa uchumi wa umilikaji nchini China ni pamoja na uchumi wa taifa, ushirika, binafsi, kujiajiri, ushirikiano, utaratibu wa hisa, uwekezaji wa wafanya biashara wa kigeni na wa Hong Kong, Macau na Taiwan.

Uchumi wa taifa ni aina ya uchumi ambayo serikali inamiliki vyombo vya uzalishaji mali; uchumi wa ushirika ni aina ya uchumi ambayo vyombo vya uzalishaji mali vinamilikiwa na mashirika ya umma; uchumi wa binafsi ni uchumi ambao watu binafsi wenye vyombo vya uzalishaji wanaajiri wafanyakazi, uchumi wa kujiajiri ni wa mtu kujitegemea kabisa katika uzalishaji kwa rasilimali na nguvu zeke mwenyewe. Uchumi wa ushirikiano ni aina ya uchumi ambayo shirika jipya la uchumi lililoungwa kwa uwekezaji wa viwanda au kampuni zenye umilikaji tofauti. Uchumi wa utaratibu wa hisa ni uchumi wa viwanda ua kampuni zilizoanzishwa na watu tofauti wenye hisa. Uchumi wa wafanya biashara wa kigeni ni uchumi ambao wafanya biashara wa kigeni kuanzisha viwanda nchini China kwa mujibu wa sheria au kanuni za sheria, ukiwa na mitindo ya aina tatu za kiwanda cha ubia kati ya China na mfanyabiashara wa kigeni, kiwanda kinachoendeshwa kwa ushirikiano kati ya China na mfanyabiashara wa kigeni na kiwanda kilichowekezwa na mfanyabiashara wa kigeni peke yake. Uchumi wa uwekezaji wa wafanya biashara wa Hong Kong, Macao na Taiwan kuanzisha viwanda vyao China bara kwa mitindo ya aina tatu ya ubia, ushirikiano na mitaji ya wafanyabiashara wa huko peke yao kwa mujibu wa sheria au kanuni za sheria kuhusu nchi za nje za Jamhuri ya watu wa China.

Katiba ya China inapiga marufuku shirika au mtu yeyote kuhujumu au kuharibu mali za taifa au za ushirika kwa njia yoyote. China inalinda haki na maslahi halali ya uchumi usio wa umilikaji wa umma kama vile wa mtu aliyejiajiri au uchumi binafsi. Mali binafsi za raia hazishambuliwi.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12