Nguo na Mapambo ya Makabila Madogo madogo 2005/08/26 |
Utamaduni na sanaa nchini China 3 2005/08/19 Mafanikio makubwa sana yamepatikana katika uenezaji wa muziki wa symphony nchini China. Katika Jumba la muziki la Beijing , kila mwaka hufanywa maonyesho mara zaidi ya 300, na tamasha kubwa za muziki wa siku za spring na nyinginezo huwaburudisha watu sana . Hivi leo, wanamuziki wenye vipawa wa China wanajitokeza kizazi hadi kizazi. |
Utamaduni na sanaa nchini China 2 2005/08/12 Katika miaka 20 iliyopita tangu yafanywe mageuzi na ufunguaji mlango wazi kwa nje, sanaa ya sarakasi ya China ilipata mafanikio katika mashindano makubwa ya kimataifa, ustadi wa kijadi wa michezo mingi imepata kuinuliwa zaidi na kuwavuta sana watu macho. |
Utamaduni na sanaa nchini China 1 2005/08/05 Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, uliwekwa mkururo wa sera za utamaduni za kuhimiza michezo ya aina mbalimbali isitawishwe na kuwatumikia umma na ujamaa, kupokea mambo mazuri ya kale na ya nchi za nje, yote hayo yameweka msingi imara kwa ukuaji wa utamaduni na sanaa. |
Mchoraji Chen Zhizhuang 2005/08/01 Marehemu Chen Zhizhuang ni mchoraji aliyejulikana baada ya kufariki dunia. Alizaliwa mwaka 1913 na kufariki dunia mwaka 1976 katika wilaya ya Rongchang mkoani Sichuan. Wakati alipokuwa hai, alikuwa anaitunza familia yake yenye watu 7 kwa mashahara wake mdogo aliokuwa akilipwa kutoka kwenye jumba la utamaduni na historia la Sichuan. |
Vipuzi vya miti 2005/07/22 Katika wilaya ya Tancheng, mkoa wa Shandong kuna kijiji maarufu kinachojulikana nchini kote kwa utengenezaji wake wa vipuzi vya miti. Kijiji hicho si kingine isipokuwa ni Kijiji cha Fannian. Wanakijiji wa huko wamerithi ufundi wa kutengeneza vipuzi vya namna hii kutoka kwa mababu zao vizazi kwa vizazi. |
Makazi ya China Kwenye Stempu 2005/07/22 China ina maeneo mapana na makabila mengi. Kutokana na tofauti za mazingira asilia na jadi mbalimbali za utamaduni, makazi ya watu katika sehemu mbalimbali yanatofautiana kabisa kiujenzi. Katika hali ya maendeleo ya ujenzi wa kisasa na kuongezeka siku hadi siku kwa nyumba zenye ghorofa nyingi, makazi ya kijadi ya mitindo mbalimbali pamoja na mila na desturi za kienyeji vikiwa ni sehemu ya mirathi ya utamaduni wa taifa la China vinazidi kupendwa na wananchi wa China. |
Tabia za wayi za kuvaa mapama 2005/07/15 Matawi mbalimbali ya kabila la Wayi, kila moja likiwa na desturi, mavazi na mila zake yanatapakaa huko na huko katika eneo pana la mikoa ya Yunnan, Guizhou na Sichuan. Mavazi yao, hasa ya wanawake yana uzuri wa kipekee na yanatofautiana sana na yale ya watu wa kabila la wahan waliowengi. |
Wushu--Gongfu ya China 2005/07/08 Wushu ni urithi bora wa utamaduni wa taifa la China, na pia ni moja ya michezo ya ridhaa ya jadi ya taifa. Na inapendwa sana na wananchi wengi. Katika muda mrefu wa ukuaji wake, wushu imeunda njia ya kujizoeza na mitindo ya maonyesho ya kipekee. |
Mawe ya rangi ya Lingshan 2005/07/01 Mawe ya rangi yanayopatikana kwenye mlima huo, kabla ya Enzi ya Ming yaliwahi kuwa miongoni mwa vitu vilivyopelekwa kwa wafalme sawa na lulu za Hepu mkoani humo. Katika historia ya Wilaya ya Lingshan imeandikwa kuwa mawe ya rangi, yaani yale mazuri miongoni mwa mawe, nayo ni bora kama jedi, huwa na mandhari ya milima, mito, misitu, moshi, mawingu, ndege na wanyama juu yake. |