Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Wanafunzi kutoka nchi za nje wafurahia kusoma na kuishi huko Shenzhen 2007/05/03
Mliyosikia ni rekodi ya watu wakisoma shairi kwa lugha ya Kichina sanifu. Lakini watu hao si Wachina, bali ni wanafunzi wa Korea ya Kusini wanaosoma huko Shenzhen, mji wa kusini mwa China. Hivi sasa wanafunzi wengi kutoka nchi za nje wanasoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mjini humo
v Vitu vya sanaa za mikono vya makabila madogo madogo mkoani Qinghai 2007/04/25
Katika mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa China, wanaishi watu wa makabila mengi yakiwemo Wa-han, Wa-tibet, Wa-hui, Wa-tu, Wa-sala na Wa-mongolia. Watu wa makabila hayo wanapojitahidi kujiendeleza kiuchumi, pia wamevumbua utamaduni wenye umaalum wa kikabila. Hadi baadhi ya ustadi wa kutengeneza vitu vya sanaa kwa mkono bado unaenea.
v Soko la Xiushui yenye sura mpya katika ulinzi wa hakimiliki 2007/04/12
Soko la Xiushui lililopo kando ya barabara kuu ya Changan hapa mjini Beijing, ni maarufu kwa biashara ya nguo. Soko hilo linawavutia sana wageni kutokana na kuwa na nguo za hariri za mtindo wa Kichina. Zamani kwenye soko hilo, kulikuwa na wafanyabiashara waliokuwa wanauza nguo zilizokuwa zimewekwa chapa maarufu za bandia
v Shanghai yafanya juhudi kubwa kuandaa maonesho ya bidhaa duniani mwaka 2010 2007/04/04
Maonesho ya bidhaa duniani yanatarajiwa kufanyika mwaka 2010 huko Shanghai, mji wa mashariki mwa China. Hivi sasa ni miaka mitatu imebaki kabla ya kufunguliwa kwa maonesho hayo, shughuli mbalimbali za maandalizi ya maonesho hayo zinaendelea vizuri mjini Shanghai.
v Ziara ya jahazi la Sweden la Goetheborg nchini China 2007/03/21
Katika nusu ya pili ya mwaka 2006 kundi la Wasweden lilikuja nchini China kwa jahazi la Goetheborg lililotengenezwa kwa kuiga mfano wa jahazi kama hilo lililokuwepo karne ya 18. Katika ziara ya miezi minne nchini China, watu wa Sweden walitembelea mkoa wa Anhui wakiwa na chai ya kale ya China iliyozalishwa kwenye mkoa huo.
v Kwaheri makazi ya muda! 2007/03/08
Katika miaka mingi iliyopita, mkoa wa Liaoning wa China ulikuwa unajulikana kwa kuwa na viwanda vingi. Ili kuwapa wafanyakazi makazi, nyumba nyingi za muda zilijengwa mkoani humo.
v Watu wa nchi za kigeni washuhudia maendeleo ya mji wa Shijiazhuang 2007/02/22

Shijiazhuang ni mji mkuu wa mkoa wa Hebei, katikati ya China. Mji huu ulianzishwa na kuendelezwa kutokana na ujenzi wa reli. Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo umewavutia wageni wengi kwenda kusoma, kufanya kazi na hata kuishi huko.

v Kheri ya mwaka mpya wa Kichina! 2007/02/15
Sikukuu ya Spring ambayo ni mwaka mpya wa jadi kwa kalenda ya kilimo ya China inakaribia. Sikukuu hiyo kubwa kuliko nyingine katika jamii ya Wachina itaanza tarehe 18, Februari mwaka huu. Hivi sasa nchini China, ama vijijini au mijini, watu wana pilikapilika nyingi wakifanya maandalizi kwa ajili ya sikukuu hiyo ya jadi.
v Juhudi za China kujenga jamii yenye masikilizano 2007/02/08
Katika juhudi za China kujenga jamii yenye masikilizano, suala moja kubwa ni hali ya kutokuwepo kwa uwiano wa maendeleo kati ya miji na vijiji na kati ya sehemu mbalimbali
v China ilivyoweka lengo kuu la kujenga jamii yenye masikilizano 2007/02/01
Katika mwaka 2006 tuliouaga hivi karibuni, China ilipata ongezeko kubwa la uchumi kiasi kwamba, pato la taifa katika kipindi cha miezi 9 ya kwanza ya mwaka 2006 liliongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7. Hata hivyo maendeleo yanayowavutia watu wengi si maendeleo katika sekta ya uchumi tu, bali ni kutokana na serikali ya China kuweka bayana lengo la kujenga jamii yenye masikilizano na tayari imechukua hatua halisi. Sasa juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10