Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
v Sura mpya ya kando za mto Changjiang mjini Wuhan 2007/09/27
Mji wa Wuhan uliopo katikati ya China ni mji mkuu wa mkoa wa Hubei. Mto Changjiang na tawi lake kuu mto Hanshui unapita kwenye mji huo. Tangu mwaka 2000, serikali ya mji wa Wuhan ilianza kukarabati kingo za kuzuia mafuriko na kuboresha mazingira kwenye kando za mito hiyo, hivi sasa sehemu hiyo inaonekana kuwa na sura mpya inayopendeza.
v Ndoa kwenye kituo cha kuwazlzimisha watumiaji kuacha kutumia dawa za kulevya 2007/09/14
Hivi karibuni, shamrashamra zilionekana kwenye kituo cha kuwalazimisha watumiaji wa dawa za kulevya waache kutumia dawa za kulevya, mji wa Kunming mkoani Yunnan. Watumiaji wanne wa dawa za kulevya walikuwa wanafunga ndoa.
v Chongqing: Mji uliojengwa mlimani 2007/08/23

Chongqing ni mji unaowavutia watu kati ya miji iliyopo kusini magharibi mwa China. Mji huo unajulikana kama mji wa mlima au mji wa mito kutokana na kwamba ulijengwa mlimani na kuzungukwa na mito miwili.

v Motaboti zachangia kupunguza msongamano wa magari mjini Guangzhou, China 2007/08/16
Guangzhou ni mji mkuu wa jimbo la Guangdong, kusini mwa China. Mto Zhujiang unapita kwenye mji huo ambao unaugawa mji huo katika sehemu tatu. Ili kupunguza msongamano wa magari barabarani, usafiri wa motaboti ulianzishwa kwenye mto Zhujiang mwezi Aprili mwaka huu, kuchukua nafasi ya vivuko vikongwe. Hivi sasa motaboti, mabasi na subway zimekuwa ni mtandao wa kisasa wa mawasiliano ya mji wa Guangzhou.
v Chaguo kubwa la usafiri lasaidia kupanua upeo wa macho wa wachina 2007/08/08
Watalii wengi wakitaka kwenda Lhasa, mkoani Tibet, hawana chaguo lingine ila tu kupanda ndege, lakini kutokana na ujenzi wa reli ya Qinghai-Tibet, muda si mrefu baadaye, watu wataweza kufika Lhasa kwa kupanda gari moshi. Wakati huo, watu wataweza kuutembelea mji wa Lhasa, ambao huitwa mji wa mwangaza wa jua kwa kuendesha magari binafsi, kupanda ndege na gari moshi. Kutokana na kuongezeka kwa chaguo la usafiri, upeo wa wachina utapanuka siku hadi siku.
v Bi. Zhai Zhaoxiu na picha alizochora kwenye kuta za nyumba za kijijini 2007/07/18
Mwandishi wetu wa habari alipoingia kwenye kijiji cha Loujiashan cha wilaya ya Zhanyi mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China aliona picha nyingi nzuri zilizochorwa kwenye kuta za nyumba za wanakijiji. Picha hizo zinaonesha mandhari ya kimaumbile na maisha ya wanavijiji kama vile shughuli za kilimo na hali ya wakulima kucheza michezo ya kisanaa.
v Wahongkong wanaoishi hapa China Bara 2007/06/28
Tarehe mosi Julai mwaka huu, Wachina wataadhimisha miaka 10 tangu China irudishe mamlaka yake Hong Kong. Katika miaka hiyo 10 iliyopita, idadi ya wakazi wa Hong Kong waliopata ajira hapa China Bara imekuwa inazidi kuongezeka. Leo katika kipindi hiki cha Tazama China, tunazungumzia Wahongkong wanaofanya kazi hapa mjini Beijing. Karibuni.
v Wataalamu wa kigeni wanaofanya kazi nchini China  2007/06/07
Leo katika kipindi chetu cha Tazama China, tunawaletea maelezo kuhudu wataalamu wa kigeni wanaofanya kazi nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni kutokana na China kufungua mlango zaidi kwa nje kwenye sekta mbalimbali, mahitaji ya China kwa wataalamu wa nchi za nje pia yanaongezaka siku hadi siku.
v Wazee watunzwa na wahudumu wa nyumbani wanaolipwa na serikali 2007/05/31
Hivi sasa jamii ya China ni jamii yenye idadi kubwa ya wazee. Kuhakikisha wazee wanakuwa na maisha mazuri ni suala linalofuatiliwa nchini China. Makala hii inaelezea hatua iliyochukuliwa na serikali ya mji wa Wuhan, mji ulioko katikati ya China, ambapo serikali ilitoa fedha za kuwalipa wahudumu wa nyumbani ili wawatunze wazee.
v Mtaa wa makazi wenye masikilizano ni msingi wa kujenga jamii yenye masikilizano 2007/05/24
Mtaa wa makazi wa bustani ya vijana ni mtaa ulioanzishwa miaka mingi iliyopita huko Jinan, mji wa mashariki mwa China. Mtaa huo wa makazi una eneo lisilozidi kilomita moja ya mraba, lakini kwenye mtaa huo zinaishi familia zaidi ya elfu 6. Nyumba nyingi za huko ni nyumba kongwe, ambazo zina eneo dogo na haizna zana za kisasa, kama vile gesi na vifaa vya kuleta joto. Hata hivyo huu ni mtaa wa makazi wa kwanza katika China Bara uliopewa tuzo ya mtaa wa makazi salama iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10