• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 3-Oktoba 9)

    (GMT+08:00) 2020-10-09 16:08:35

    Tanzania yarekodi ongezeko kubwa la watalii kutoka nje ya nchi

    Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Hamisi Kigwangala amesema, idadi ya watalii kutoka nje wanaotembelea nchini humo imeanza kuongezeka baada ya nchi hiyo kufungua anga yake kwa ndege za kimataifa Mei 18 baada ya janga la virusi vya Corona.

    Amesema takwimu zilizoandikishwa kuanzia mwezi Juni zinaonyesha kuwa idadi ya watalii wa kigeni imeongezeka ikilinganishwa na mwezi April na Mei. Waziri huyo amesema, mwezi Julai, Hifadhi ya Ngorongoro ilipokea watalii 1,972 ikilinganishwa na watalii 202 waliopokelewa mwezi April.

    Kigwangala amesema, mwaka jana, Tanzania ilipokea watalii 1,527,230 na kuingiza dola za kimarekani bilioni 2.6, pia ameongeza kuwa sekta ya utalii inatoa ajira milioni 1.6 rasmi na zisizo rasmi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako