China yapongeza serikali ya mpito ya Sudan kwa kusaini makubaliano ya amani na kundi la upinzani
China imepongeza na kuiunga mkono serikali ya mpito ya Sudan kwa kusaini rasmi makubaliano kamili ya amani na kundi kuu la upinzani SRF.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema makubaliano hayo yaliyosainiwa tarehe 3, Oktoba mjini Juba, Sudan Kusini, yatasaidia Sudan kusukuma mbele mchakato wa mpito wa kisiasa kwa utulivu na China inatarajia pande zote husika zitatekeleza makubaliano hayo ya amani kwa makini. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kufanya kazi za kiujenzi ili kuleta amani, utulivu na maendeleo nchini Sudan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |