Wataalam wa afya wa China wamaliza kazi za kusaidia kupambana na COVID-19 nchini Lesotho na kuelekea Angola
Jopo la wataalam wa afya kutoka China wamemaliza kazi za kusaidia kupambana na ugonjwa wa Corona nchini Lesotho na kuelekea Angola.
Wakiwa nchini Lesotho, wataalam hao waliotumwa na serikali ya China walibadilishana maoni na wenzao kutoka idara ya afya na hospitali za Lesotho juu ya maarifa ya China ikiwemo kuongeza uwezo wa kupima virusi vya Corona, kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo kuanzia mitaani na kuwashughulikia wagonjwa kwa hali zao tofauti.
Serikali ya Lesotho imepongeza sana ujio wa wataalam hao na walipofika waziri mkuu Bw. Moeketsi Majoro alienda mwenyewe kuwapokea katika uwanja wa ndege.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |