• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 3-Oktoba 9)

    (GMT+08:00) 2020-10-09 16:08:35

    Jamii ya kimataifa yatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika kukabiliana na virusi vya Corona

    Nchi mbalimbali zimeeleza nia ya kuimarisha ushirikiano na China katika juhudi za kukabiliana na virusi vya Corona.

    Waziri wa habari wa Zimbabwe Monica Mutsvangwa ameishukuru China kwa kuipatia Zimbabwe misaada ya vifaa vya kinga na matibabu, na kusema China ilipeleka wataalamu wa kiafya nchini Zimbabwe, ambao walitoa uzoefu muhimu kuhusu jinsi ya kukinga na kutibu virusi vya Corona.

    Hadi sasa kutokana na ushirikiano wa China na Afrika, vifaa vya kukabiliana na virusi vya Corona vimepelekwa hadi nchi 20 za Afrika ambazo hazina bandari, na China imepeleka timu za wataalamu wa afya kwenda nchi 13 barani Afrika. Mkurugenzi wa mambo ya kisiasa wa chama tawala cha Kenya Jubilee Kadara Swaleh amesema, China imetoa misaada mingi ikiwemo teknolojia, uzoefu na vifaa kwa sehemu mbalimbali duniani. Katika msukosuko huo, China inajitahidi kuziunganisha nchi mbalimbali na kutoa mchango wake, badala ya kuifarakanisha dunia. Amesisitiza kuwa, ni wakati kwa binadamu kukaa pamoja kujadili ufumbuzi wa masuala yakiwemo chanjo na ukarabati wa uchumi.

    Waisrael waandamana usiku, wamtaka Waziri Mkuu ang'atuke

    Maelfu ya Waisrael wameandamana jana usiku kote Israeli dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wakiendelea na kampeni yao dhidi yakiongozi huyo licha ya serikali kupiga marufuku mikusanyiko ya watu katika juhudi mpya za kuzuia kuenea maambukizi ya virusi vya corona.

    Wakati Netanyahu amesema marufuku hiyo ni kwa lengo la kulinda usalama wa raia, waandamanaji wanamshutumu kwa kutaka kukomesha harakati zao.

    Waandamanaji hao wamekuwa wakikusanyika nje ya nyumba ya Netanyahu mjini Jerusalem kila wiki kwa zaidi ya miezi mitatu, wakimtaka ajiuzulu.

    Waandamanaji wanasema Netanyahu hapaswi kuwa Waziri Mkuu wakati anashtakiwa kwa madai ya ufisadi.

    Aidha wanamlaumu pia kwa kushindwa kuushughulikia ipasavyo mgogoro wa virusi vya corona, ambao umeharibu uchumi wa nchi hiyo. Wengi wa waandamanaji ni Waisrael vijana ambao wamepoteza kazi kutokana na janga hilo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako