Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2003-11-25 21:17:42    
Tiba Ya Cock Tail

cri
   Taarifa ya uchunguzi iliyotolewa hivi karibuni na wanasayansi wa Uingereza inasema kuwa 90% ya wagonjwa wa ukimwi wanaopata tiba ya mchanganyiko wa madawa "Cock Tail" wanaweza kurefusha maisha kwa miaka zaidi ya 10. Wanasayansi wa Uingereza baada ya kufanya uchambuzi juu ya tafiti 22 kuhusu tiba ya cock tail, uliofanywa katika nchi za Ulaya, Australia na Canada, waligundua kuwa katika muda wa miaka minne tangu cock tail kuanza kutumiwa na wagonjwa wa ukimwi kati ya mwaka 1997 na mwaka 2010, idadi ya wagonjwa wa ukimwi waliofariki ilipungua kwa 80%. Kabla ya tiba hiyo kutumiwa, watu wa makamo walioambukizwa virusi vya ukimwi, waliweza kuishi kwa miaka 6 hadi miaka 8 tu. Hivi sasa, 90% ya wagonjwa wa ukimwi wanaopata tiba ya cock tail wanaweza kuishi kwa miaka zaidi ya 10. Watafiti wanasema kuwa takwimu hizo zimeleta matumaini ya tiba kwa wagonjwa wa ukimwi kwamba kutokana na tiba hiyo, ugonjwa huo unaoua watu utaweza kubadilika kuwa ugonjwa wa muda mrefu. Kiongozi wa utafiti huo Bw. Hurload Peter alisema, ?Tunatarajia tiba hiyo itafanya kazi kubwa zaidi katika kuongeza muda wa maisha ya watu walioambukizwa virusi vya ukimwi, na hatimaye kuwawezesha kuishi kwa miaka iliyolingana na watu wasioambukizwa.? Aidha, katika utafiti uligundua kwamba idadi ya vifo vya wagonjwa walioambukizwa virusi vya ukimwi kwa sindano ya mihadarati ni mara 4 ya watu walioambukizwa virusi kwa kujamiiana. Taarifa inasema kuwa wagonjwa ambao ni wanaotumia mihadarati, huwa hawana fedha ya kununua madawa ya kutosha kutibu ukimwi, na kwamba wakati wanapochoma sindano za mihadarati, ni rahisi kuambukizwa virusi vya magonjwa mengine. Tiba ya cock tail ni mbinu mwafaka kabisa kwa hivi sasa ya kutibu wagonjwa wa ukimwi, iliyogunduliwa na mwanasayansi wa Marekani mwenye asili ya China Bw. He Da-yi mwaka 1996. Tiba hiyo ni inadhibiti ugonjwa wa ukimwi kwa mseto wa madawa . Hivi sasa, idadi ya watu wenye virusi vya ukimwi duniani imepindukia milioni 40, wengi wao wakiwa katika bara la Afrika, lakini wagonjwa hao hawawezi kupata tiba nzuri kutokana na kushindwa kumudu gharama kubwa za tiba ya cock tail.