Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia

 • Ndoto ya msichana wa China kuhusu michezo ya Olimpiki
 •  2008/07/10
  Wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, watu wa China wanazidi kuonesha uchangamfu mkubwa kuhusu michezo hiyo. Katika kipindi cha leo tutasikia maelezo ya msichana wa China akieleza ndoto yake kuhusu michezo ya Olimpiki.
 • China ni maskani yangu ya pili
 •  2008/06/26
  Mwaka 2007 kutokana na mchango mkubwa aliotoa katika kuboresha utengenezaji wa mazulia wa China, Bw. Khan alipata tuzo ya urafiki, ambayo ni tuzo ya ngazi ya juu kabisa inayotolewa na serikali ya China kwa wataalam wa kigeni wanaofanya kazi nchini China
 • Mwanamke wa Korea Kusini atakayekimbiza mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing
 •  2008/06/05
  Bi. Cho Sung Hye alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, alisema (sauti 1) "Mimi ni raia wa Korea Kusini, na hivi sasa nimepata nafasi ya kuishi kwa muda mrefu nchini China. Mbali na hayo nilipewa tuzo ya urafiki na serikali ya China, na kuteuliwa kuwa mkimbiza mwenge wa michezo ya Olimpiki ya Beijing. Naona fahari kubwa, ninataka watu wote wafahamu furaha yangu."
 • China yaanzisha ghala la damu kwa ajili ya michezo ya Olimpiki
 •  2008/05/01
  Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Beijing mwezi Agosti mwaka huu ni tamasha kubwa la michezo duniani ambalo hufanyika kila baada ya miaka minne, ambapo wanamichezo na watalii kutoka nchi na sehemu mbalimbali watakutana hapa Beijing. Ili kukabiliana na ajali yoyote itakayoweza kutokea, China imeanza kuanzisha ghala la damu.
  Zaidi>>
 • Simu na hadhi yake katika maisha ya watu wa China
 •  2008/11/20
  Hivi sasa simu za mkononi zinachukua hadhi muhimu katika maisha ya watu wa China, kiasi kwamba ni mahitaji ya kila siku. Lakini amini usiamini, miaka 30 iliyopita katika sehemu nyingi nchini China, simu ilikuwa ni bidhaa isiyo ya kawaida, wakati huo njia ya posta ilikuwa ni njia muhimu ya mawasiliano kati ya watu wanaoishi katika sehemu mbili zilizoko mbali.
 • Mkoa wa Ningxia wahimiza utoaji mafunzo ya ufundi wa kazi
 •  2008/11/03
  Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia una watu wengi, lakini mashamba ya mkoa huo ni machache. Ili kuhamisha ziada ya nguvukazi vijijini, serikali ya huko inafuata hali halisi, na kuwahimiza watu hao kwenda nje ya mkoa huo kufanya kazi. Ili kuinua sifa ya watu hao, mkoa wa Ningxia unaimarisha kuhimiza utoaji mafunzo ya ufundi wa kazi.
 • Watu wenye tabasamu waonesha sura nzuri ya Beijing
 •  2008/09/24
  Katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing iliyomalizika siku chache zilizopita, kuna watu wanaojitolea milioni 1.47 waliotoa huduma katika kazi mbalimbali zikiwemo maandalizi ya mashindano, usalama, mawasiliano, utoaji huduma kwa vyombo vya habari na uendeshaji wa mji.
 • Wimbo wa Michezo ya Olimpiki "Beijing"
 •  2008/09/11
  Wanamuziki wa Bendi ya The SMU ya Ujerumani walikuja Beijing wakiwa na wimbo wao uitwao "Beijing" walioutunga kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008.
 • Maisha ya Bw. Nuttavudh Photisaro mjini Guangzhou
 •  2008/06/19
  Bw. Photisaro ni konsela wa Thailand mjini Guangzhou, China, zamani aliwahi kuwa konsela wa Thailand nchini Cambodia. Muda wake wa kufanya kazi hapa China haujatimia mwaka mmoja, lakini ameupenda mji huo mzuri.
  Zaidi>>
 • Maisha mapya ya wakazi wa kijiji cha Sangmo
 •  2008/11/12
  Kijiji cha Sangmo kilichoko umbali wa kilomita zaidi ya kumi kutoka magharibi mwa Lahsa, mji mkuu wa Tibet ni kijiji kinachofanya shughuli za utalii zinazowavutia watalii kwa mila na desturi za jadi. Leo tunawaletea maelezo juu ya maisha mapya ya wakazi wa kijiji hicho.
 • Maisha mapya ya familia moja ya kabila la Wahui
 •  2008/10/27
  Huu ni mwaka wa kumi tangu familia ya mzee Ma Tingfu wahamie kwenye nyumba mpya. Katika miaka kumi iliyopita, watu wa familia hiyo pamoja na wakazi wengine walibadilisha ardhi yenye hali ya jangwa kuwa mashamba, na wanaishi maisha mazuri.
 • Mwimbaji wa nyimbo za kabila la Wadong bibi Wu Yuzhen
 •  2008/10/20
  Bibi Wu Yuzhen wa kabila la Wadong ni msichana mwenye umri wa miaka 23 aliyezaliwa na kuishi katika wilaya ya Liping mkoani Guiyang. Sasa yeye ni mwimbaji maarufu katika sehemu hiyo, na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa utalii wa kabila la Wadong mkoani Guizhou, kwa kuwa yeye ni hodari katika kuimba wimbo maalumu wa kabila la Wadong.
  Zaidi>>
 • Bibi Wang Fang na "familia ya angels"
 •  2008/11/17
  Mama huyo anaitwa Wang Fang. Yeye ni mama wa mtoto mwenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo mjini Nanning katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, China. Katika miaka mingi iliyopita, alitumia fedha zake zote kuanzisha kituo cha kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo, yaani "familia ya angels", na kuzisaidia familia maskini zenye matatizo ya kiuchumi kutibu watoto wenye ugonjwa huo.
 • Mlemavu anayependa kuwasaidia wengine Bw. Shen Fucai
 •  2008/09/11
  Katika mji wa Baotou wa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, kaskazini mwa China, ukimtaja meneja wa kampuni ya biashara ya Aixin Bw. Shen Fucai, watu wanaomfahamu wote wanamsifu sana. Bw. Shen Fucai ni mtu asiyeweza kuona, lakini anapenda kuwasaidia watu wenye hali dhaifu. Katika miaka 6 iliyopita, siku zote anawasaidia walemavu wengine, watu wenye matatizo ya kiuchumi na watoto waliokosa masomo yao.
 • Kijana anayetunza Panda ateuliwa kuwa mkimbiza mwenge wa michezo ya Olimpiki
 •  2008/07/03
  Vileta bahati vya michezo ya Olimpiki ya Beijing ni Fuwa watano, na Fuwa mmoja aitwaye Jingjing, sura yake inayopendeza ilisanifiwa kutokana na Panda mmoja mwenye jina hilo hilo anayeishi mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China. Panda ni wanyama adimu ambao wako kwenye hatari ya kutoweka, wanapatikana nchini China tu.
  Zaidi>>
  Zaidi>>