Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-25 19:17:35    
Mradi mkubwa wa maji wa Magenge Matatu

cri

    Changjiang ni mto mkubwa hapa nchini China, maarufu kama mto mama kwa wachina. Mto huo hulea karibu nusu ya watu wa China, lakini pia huleta mafriko ya maji mara kwa mara, na kuwalazimisha watu walioishi kando yake wakimbie maskani yao.

    Miaka 100 iliyopita ,Bw. Sun Yat San ambaye ni mwanzilishi wa mapinduzi ya demukrasia ya China,kwenye sehemu ya mto huo iitwayo magenge matatu, ili kudhibiti mafriko ya maji na kuyatumia maji kwa manufaa ya watu. Lakini katika miaka 100 iliyopita, China ilikuwa nchi dhaifu na maskini sana, pendekeo la mradi huo ilikuwa ni ndoto tu.

    Mwaka 1949, Jamhuri ya watu wa China iliasisiwa,ambapo ndoto hiyo ikaanza kubadilika kuwa vitendo. Viongozi wa awamu kadhaa nchini China Bw.Mao Zedong, Deng Xiaoping na Jiang Zemin wote walieleza kufurahia mradi wa magenge matatu. Na kiongozi wa kwanza wa China Bw.Mao Zedong alitunga shairi kwa mradi huo. Mradi wa magenge matatu ni mkubwa mno,serikali ya China haina budi kushukua hatua mathubuti juu yake. Kwa hvyo,serikali iliunda asasi maalumu ya kushirikisha wataalamu wa maeneo mbalimbali,ikifanya uchunguzi na utafitijuu ya utekelezaji wa mradi huo. Kazi hiyoiliendelae kwa miaka 40, na katika kipindi hicho,China pia ilikuwa inakusanya nguvu za kiuchumi, uwezo wa kiteknolojia na maeneo megineyo.

    Mwaka 1992,kwenye mkutano wa wabunge wote wa bunge la umma ,ambalo ni chombo chenye madaraka ya juu kabisa nchini China,wabunge wengi walipiga kura za ndiyo na kupitisha uamuzi wa kujenga mradi wa magenge matatu.

    Mwaka 1994,Bw. Li Pengaliye kuwa waziri mkuu wa China wakati huo,alitangaza uzinduzi wa mradi huo . aada ya miaka 16,mradi huo utakaogharimu Renminbi Yuan bilioni 22,utakamilishwa ifikapo mwaka 2009.

    Miaka 10 imeshapita sasa. Katika sehemu iitwayo San Douping,mkoani Hubei,katikati ya China,limesimama bwawa kubwa linaloweza kukinga mafuriko makubwa sana, pamoja na mlango wa kupitisha meli ambao ni mkubwa kuloko yote duniani. Mwezi juni, mwaka huu, bwawa hilo limeanza kulimbikiza maji, na kuzalisha umeme.

Idhaa ya Kiswahili  2003-11-29