Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2003-11-29 01:24:47    
vijana wamekuwa katika hatari zaidi ya kuathiriwa na ugonjwa wa ukimwi

cri
    Taafifa iliyorolewa hivi karibuni na Shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu kuhusu "hali ya idadi ya watu ulimwenguni kwa mwaka 2003" inasema kuwa pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu wenye umri mdogo ulimwenguni, vijana wamekuwa katika hatari zaidi ya kuathiriwa na ugonjwa wa ukimwi na matumizi ya mabavu.

    Taarifa hiyo inasema kuwa hivi sasa kila sekunde 14 kuna kijana mmoja aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi, ambao wengi wao ni vijana wa kike. Kadri idadi ya vijana inavyoongezeka katika jumla ya idadi ya watu, ndivyo matatizo ya kijamii yakiwa ni pamoja na umasikini, matumizi ya mabavu, matumizi ya mihadarati, ukahaba na ubafuzi wa kikabila yanavyoongezeka. Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya vijana wenye umri wa miaka kati ya 10 na 19 ni kiasi cha bilioni 1na milioni 200, ikiwa 20% ya jumla ya idadi ya watu ulimwenguni, ambao 90% yao wako katika nchi zinazoendelea. Aidha, idadi ya vijana venye umri wa chini ya miaka 25 imechukua 50% ya jumla ya idadi ya watu ulimwenguni.

    Taarifa hiyo inasema kuwa chanzo kimojawapo muhimu cha kuambukizwa kwa urahisi zaidi virusi vya ukimwi kwa vijana ni umasikini. Kwa mfano, wasichana wa baadhi ya nchi masikini wamekuwa mahawara na kuambukizwa virusi vya ukimwi kutokana na kutaka kupata karo ya shule na kusaidia familia zao. Licha ya hayo, katika nchi nyingi elimu kuhusu masuala ya jinsia ni mwiko kutajwa, hivyuo vijana wengi hawajui namna ya kujikinga na maradhi ya kujamiiana. Kwa mfano, nchini Somalia, ni 26% tu ya vijana waliowahi kusikia kuhusu ugonjwa wa ukimwi na ni 1% ya vijana ambao wanajua namna ya kujikinga na ukimwi.

    Idadi kubwa ya watoto walizaliwa, na idadi ndogo ya watu wanaofariki, ni hali ambayo imechangia kuongezeka sana kwa idadi ya vijana kwa hivi sasa.

    Taarifa inasema kuwa ongezeko kubwa la idadi ya vijana linatutaka kukabiliana na masuala mengi ya jamii, ladini kwa upande mweingine limetuletea fursa nzuri sana. Endapo serikali za nchi mbalimbali zitaweza kukidhi mahitaji ya elimu na afya kwa kundi hilo la watu, basi baada ya kutimiza umri wa miaka 20, wataweza kuhamasisha ongezeko la kasi la uchumi na kuleta ustawi kwa dunia yetu.