Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-01-28 21:22:30    
Wanaviwanda wa tabaka la "Mizizi ya majani" wa mkoani Zhejiang waliofanikiwa

cri
  Mkoa wa Zhejiang ulioko sehemu ya kusini mashariki ya China ni sehemu yenye shughuli nyingi za uchimi wa watu binafsi, ambapo wakazi wa huko wanapenda sana kujishughulisha na mambo ya viwanda na biashara. Pamoja na maendeleo makubwa ya uchumi wa China katika zaidi ya miaka 20 iliyopita, mali za watu binafsi za wenye viwanda zinaongezeka hatua kwa hatua, na baadhi yao wamekuwa matajiri wakubwa. Je, hao wanaviwanda na wafanya-baishara hao wenye mali nyingi ni watu wa aina gani? Na walitajirika kwa namna gani, na wanafanya nini baada ya kuwa na mali nyingi? Mwandishi wetu wa habari akiwa na maswali hayo, alitembelea mkoa wa Zhejiang na kuwahoji wafanya biashara wenye viwanda.

  Tukitupia macho juu ya historia za baadhi ya wanaviwanda mkoani Zhejiang, tutaona kuwa kabla ya hao kufanikiwa sana walikuwa watu wa kawaida kabisa, wengi wao walikuwa wakulima, wafanyakazi viwandani au mafundi. Kutokana na uchunguzi ulifanywa, wengi wa watu hao ni wenye elimu za sekondari tu.

  Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Aohua bibi Li Li-fang kabla ya miaka zaidi ya 10 iliyopita, alikuwa mtunzaji wa stoo ya kiwanda cha tarafa sehemu ya vijijini. Mwaka 1990, alianzisha karakana moja ndogo yenye wafanyakazi 7. baada ya kujitahidi kwa miaka mingi, karakana hiyo imekuwa kiwanda kikubwa cha transfoma. Hivi sasa thamani ya uzaiishaji mali ya kiwanda hicho imefikia zaidi ya Yuan milioni 300, sawa na dola za kimarekani milioni 36.6 na idadi ya wafanyakazi imezidi 1000.

  Bibi Li alipohojiwa na mwandishi wa habari, alisema kuwa shida za nyubani zilimpa moyo wa kuanzisha kiwanda. "Afya ya mume wangu si nzuri, ana ugonjwa wa moyo. Mara kwa mara aliugua hadi kukimbizwa hospitalini, na kila mara tulipaswa kulipa Yuan elfu makumi kadhaa. Lakini watu ule tulifanya kazi viwandani, mshahara wetu wa mwaka mzina haukuzidi Yuan elfu kumi, tulikuwa na shida kubwa ya kiuchumi. Hivyo nilipiga moyo konde kuanzisha kiwanda hivho. Wakati ule, hali yangu ilikuwa si nzuri, Yuan elfu 30 zilizohitajiwa katika uanzishaji wa kiwanda, mimi nilikopa kutoka kwa babara."

  Ni kama bibi Li alivyokuwa, wanaviwanda wengi wa mkoa wa Zhejiang walikuwa katika tabaka la chini katika jamii. Lengo lao la mwanzoni halikuwa la kuonyesha mafanikio yao au kupata mali nyingi, bali ni kuondoa shida zao za kiuchumi. Hivyo wanauchumi wengi waliita hali ya ustawi wa uchumi wa watu binafsi kuwa ni uchumi wa "Mizizi ya majani".

  Walijitegemea kwa mitaji na uzoefu unaohitajiwa katika uanzishaji wa viwanda vyao, walijiimarisha katika hali yenye shida na kuelekea mafanikio. Katika miaka ya karibuni, wataalamu wengi wa nchini na wa nchi za nje walifanya utafiti juu ya siri yao ya kufanikiwa. Baadhi ya watu wanaona kwamba kitu muhimu kilichowapelekea hadi kufanikiwa ni kujinyima katika mahitaji maishani mwao, bidii za kazi na akili katika mambo ya biashara.

  Lakini wanaviwanda wa mkoani Zhejiang wanapenda kusema kuwa sababu ya kimsingi ya kufanikiwa kwao ni seta za mageuzi na ufunguaji mlango zilizoanza kutekelezwa toka mwishoni mwa karne ya 70. sera hizo zilibuniwa kwa ajili ya kuanzisha uchumi wa kimasoko na kuongeza pato la wakulima. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya lifti ya Xizi mjini Hangzhou Bw. Wang Yong-fu alisema kuwa sera za mageuzi na ufunguaji mlango zilileta nafasi nzuri kwa uanzishaji wa kampuni yake. Alisema, "Mwanzoni hatukuwa lengo kubwa, kwani wakati ule tulikuwa tumefurahi kwa kuweza kuondokana na mashamba ya kilimo na kuanzisha makampuni yetu wenyewe. Maendeleo yanategemea nafasi, kwa bahati nzuri tuliipata, kama mageuzi yakifanyika mapema zaidi, sisi bado tulikuwa watoto, ama mageuzi yakifanyika chelewa zaidi, tutakuwa tumezeeka. Hii ni nafasi inayotokea kwa nadra ambayo sisi tumeipata kwa bahati nzuri."

  Bwana Wang ana ushahidi mwingi unazochangia hoja yake. Mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, Bw. Wang alikuwa na kiwanda cha mitambo ya kilimo katika kiunga cha mji wa Hangzhou kilichotengeneza vipuli vya trakta. Baada ya kufanya mageuzi na kutekeleza sera za ufunguaji mlango, uchumi wa Hangzhou ulikuwa na ongezeko la kasi ambapo majumba marefu yalijengwa mjini humo. Aliona kuwa lifti zitahiwajiwa kwa wingi, hivyo akishirikiana na watu wengine alianzisha kampuni inayozalisha lifti ambayo pato lake limefikia Yuan zaidi ya bilioni 2, sawa na dola za kimarekani milioni 244 kwa mwaka.

  Mazingira ya maisha na hadhi ya wanaviwanda waliofanikiwa vimekuwa tofauti kabisa na vile vya zamani, hivi sasa baadhi yao wanaanza kunufaisha jamii kwa mali walizopata. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya nguo ya Fukeda mkoani Zhejiang Bw. Xu Nian-yu alianzisha eneo la ustawishaji wa viwanda na kutaka viwanda vinavyojengwa katika eneo hilo viajiri wakazi wa sehemu ya magharibi ya China. Alisema, "Mwaka 2003, badala ya kufuatilia faida, tulizingatia kunufaisha jamii. Lengo letu la kuanzisha eneo la ustawishaji wa viwanda ni kuchangia utatuzi wa ukosefu wa nafasi za ajira.

  Hivi sasa, wanaviwanda wa mkoani Zhejiang wameona dosari zao za upungufu wa elimu uzoefu wa usimamizi wa kazi. Hivyo wengi wao wamejiendeleza kwa masomo yanayohusu usimamizi wa viwanda.

Idhaa ya Kiswahili 2004-01-28