Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-02-05 20:22:47    
Utaratibu wa kiwango cha usalama wa kupewa mikopo kwa wakazi watimiza matarajio yao ya kununua nyumba

cri
  Wasikilizaji wapendwa, kifuatacho ni kipindi cha nchi yetu mbioni. Kuwa na nyumba nzuri ni matarajio ya familia za wakazi wa mijini. Katika miaka ya karibuni, wakazi wengi nchini China wamenunua nyumba zao kwa mikopo ya benki. Lakini, wakazi wengi wenye mawazo ya kuomba mikopo ya nyumba walisitasita wakiona mchakato wa kuomba mikopo ni mkubwa na kuchukua muda mrefu. Hivi karibuni, mji wa Shanghai ulirahisisha utaratibu wa kuomba mikopo ya nyumba, hatua ambayo imewawezesha wakazi wengi wa Shanghai kupata nyumba zao wenyewe.

  Dada Xu ni mzawa wa Shanghai, baada ya kumaliza masomo yake katika chuo kikuu alitamani kuwa na nyumba yeke mwenyewe. Kutokana na kwamba alianza kazi miaka michache iliyopita, hana akiba nyingi ya fedha, hivyo alikuwa na wazo la kununua nyumba kwa mkopo wa benki, lakini alisitasita baada ya kuona mchakato wa kuomba mkopo ni mgumu na kuchukua muda mrefu.

  Alisema, "Nitafunga ndoa, hivyo ninataka sana kununua nyumba. Rafiki yangu mmoja alinunua nyumba kwa mkopo wa benki, lakini mchakato wa kupewa mkopo ni mgumu, sisi wanunuzi wa nyumba hatufahamu vizuri kanuni za utoaji wa mkopo wa nyumba, kwa kawaida, wanunuzi wanajaza fumu kwa kuelekezwa na wauzaji nyumba."

  Habari zinasema kuwa mtu akiomba mkopo wa nyumba, benki ya biashara inataka mwombaji ajaze fomu nyingi na kutoa habari zake mbalimbali, kisha benki itafanya uchunguzi ambao utachukua muda wa miezi miwili au mitatu. Hali hiyo imekwamisha maendeleo ya ununuzi wa nyumba kwa mikopo ya benki hapa nchini na kuwaudhi waombaji.

  Wanauchumi wanasema kuwa chanzo cha kuwepo shida katika uwombaji wa mikopo ya nyumba ni kwamba China bado haijajenga utaratibu wa kiwango cha usalama wa kupewa mikopo kwa wakazi. Chini ya utaratibu huo, makampuni ya utoaji wa habari kuhusu kiwango cha uaminifu cha wakazi yanaandika historia ya kila mtu ya urudishaji fedha za mikopo aliyopewa, na kutoa tathimini juu ya kiwango chake cha usalama wa kupewa mikopo, ambayo itaweza kufikiriwa na benki za biashara wkati zinapotoa mikopo kwa watu. Katika muda mrefu uliopita, utaratibu wa kiwango cha usalama wa kupewa mikopo cha wakazi haukukamilishwa vizuri ambapo historia za watu za kuredisha fedha za mikopo hazikuandikwa kwa kigezo cha namna moja. Hivyo, benki za biashara zinapotoa mikopo zinatumia mchakato mkubwa ili kuzuia hatari na kulinda maslahi yake.

  Shanghai ni mji unaoendelea kwa haraka katika utoaji wa mikopo kwa wakazi ambapo benki nyingi za biashara mjini humu zina shughuli za utoaji mikopo kwa wakazi. Katika shughuli hizo, waombaji mikopo wanalalamika sana juu ya mchakato wake mkubwa, wakati benki za biashara nazo zinahisi kushindwa kudhibiti mwafaka hali ya hatari inayotokea katika utoaji wa mikopo. Ili kutatua hitilafu hizo, mwaka 2000 serikali ya Shanghai iliamua kujenga utaratibu wa kiwango cha usalama wa kupewa mikopo kwa wanamji wake ambapo ilitumia mbinu inayotumika na nchi nyingi duniani ya kuanzisha kampuni ya wakala inayojulikana kwa kampuni ya utoaji habari kuhusu kiwango cha usalama wa kupewa mikopo kwa wakazi ambayo imekusanya habari zote kuhusu urudishaji wa fedha za mikopo za kila mwanamji.

  Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Zhou Wei-dong alipoeleza shughuli za kampuni yao alisema, "Kampuni yetu inakusanya habri za utoaji mikopo zilizoko katika benki mbalimbali za biashara. Kama vile, mtu fulani alipewa mkopo lini, hali ya urudishaji wa fedha za mkopo ikoje, ambazo zitahifadhiwa katika kampyuta za kampuni yetu. Baada ya hapo, mtu yeyote akiomba mkopo ukiwa ni pamoja na kununua nyumba, gari au vitu vingine vikubwa na kudumu, au kuomba kadi za ukopeshaji, benki za biashara itakuja kwetu kuangalia rekodi ya historia yake."

  Habari zinasema kuwa hivi sasa kampuni ya kiwango cha usalama wa kupewa mikopo kwa wanamji ya Shanghai imekusanya rekodi za historia za wanamji milioni kadhaa na kuandika taarifa kuhusu tathimini za uaminifu wao zikiwa ni pamoja na zile kuhusu vitendo vyake vya kuomba mkopo mkubwa kwa kusudia baya, kutorudisha fedha za mikopo alizokopeshwa, kukwepa ushuru au kupewa adhabu na idara za usalama. Habari kuhusu makosa yake zitahifadhiwa miaka 7.

  Baada ya kujenga utaratibu huo, benki za biashara zilizoko mjini Shanghai zinaweza kupata taarifa kuhusu kiwango cha uaminifu cha mwanamji fulani kwa sekonde chache tu, na zinaweza kuamua kumpa mkopo au la, au kumkopesha kiasi gani cha fedha. Bw. Zhou alisema, "Hapo zamai, benki zinapotoa mikopo, zinaona kwamba kuna hatari nyingi katika shughuli hizo. Hivi sasa, benki zinaona kwamba mfumo wa rekodi za uaminifu wa wakazi ni wa pekee unaotegemeka, na hakuna mbinu yoyote nyingine inayoweza kuzifahamisha hali ya uaminifu za wakazi kwa gharama ndogo."

  Habari zinasema kuwa tangu kujenga utaratibu wa usalama wa kupewa mikopo kwa wanamji mwaka 2000, maendeleo ya kasi yalipatikana katika utoaji wa mikopo. Hadi nusu ya kwanza ya mwaka uliopita, benki za biashara mjini Shanghai zilitoa mikopo zaidi ya Yuan za Renminbi bilioni 130, sawa na dola za kimarekani bilioni 15.8 kwa ajili ya matumizi ya wanamji ikichukua zaidi ya 12% ya jumla ya mikopo iliyotolewa na benki hizo na kuchukua nafasi ya kwanza hapa nchini ambapo fedha za mikopo zilizoshindwa kurudishwa ni chini ya 1% tu.

  Utaratibu wa kiwango cha usalama wa kupewa mikopo kwa wananchi mjini Shanghai umewanufaisha wakazi wa mji huo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-02-05