Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-03 17:44:16    
Nini maana ya homa ya mafua ya ndege na athari zake kwa binadamu.

cri

Mabata wanapewa chanjo dhidi ya homa ya mafua ya ndege.   

    Maambukizi ya homa ya mafua ya ndege yanaenea katika baadhi ya nchi na sehemu barani Asia tokea mwezi Desemba mwaka 2003. Hivi sasa nchi za China, Thailand, Cambodia, Vietnam, Japan na Korea ya Kusini zimetoa taarifa kuhusu kugunduliwa maambukizi ya homa ya mafua ya ndege katika nchi hizo, ambapo mamilioni kuku wamekufa au kuchinjwa kutokana na maradhi hayo nchini Vietnam na Thailand. Je, homa ya mafua ya ndege ni ugonjwawa namna gani? Maradhi hayo yana madhara gani? Na jinsi gani binadamu wanaweza kujikinga nayo?

    Homa ya mafua ya ndeg ni maradhi ya kuambukiza ya kuku, bata, bata mzinga na njiwa yanayosababishwa na virusi vya mafua ya aina ya A, na kuku walioambukizwa virusi vya aina hiyo , huonekana kuwa na matatizo katika mwili mzima au katika mishipa ya kukupumua, ikiwa ni pamoja na kuduwaa, kukohoa, kupiga chfya na kotokwa machozi mengi. Homa kali ya mafua ya ndege inapomshambulia ndege, uwezekano wa kufa ni 100%. Hivyo, homa kali ya mafua ya ndege inachukuliwa na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani kuwa ni maradhi hatari ya wanyama ya ngazi ya A.

    Hatua nne zinaweza kuthibitisha virusi wanaoambukizwa kuku na bata kama ni vya aina ya A, ambazo ni pamoja na ya kwanza, baada ya kuibuka maambukizi ya homa kali ya mafua ya ndege, wataalamu waende kufanya uchunguzi na upimaji katika sehemu zenye maambukizi. Pili, kuthibitisha kwa upimaji wa majimaji yaliyopo kwenye damu (serum). Tatu ni kutengenisha na kuthibitisha virusi katika maabara. Na nne ni idara za kilimo ambazo zinathibitisha kwa hatua ya mwisho kutokana na matokeo ya upimaji uliofanywa katika maabra.

    Kuhusu madhara ya homa ya mafua ya ndege kwa binadamu, matokeo ya utafiti husika uliofanywa yanaonyesha kwamba binadamu wanaweza kuwa na virusi vya homa ya mafua ya ndege bila kuonekana kuwa na matatizo yoyote, ila tu nguvu za kinga miilini mwa binadamu zinapopungua, virusi hivyo huanza kumuathiri binadamu. Matokeo ya upimaji wa mwanzo juu ya gene za binadamu yanaonesha kuwa, hiva sasa virusi vinavyoambukiza binadamu vinatokana na kuku na ndege tu, wala haviambukizwi kutoka kwa binadamu walioambukizwa.   

    Kuhusu udhibiti wa maambukizi ya virusi vya homa ya mafua ya ndege kwa binadamu, wataalamu husika wanasema kuwa, kwanza tunapaswa kugundua haraka kuku walioambukizwa na virusi vya homa ya mafua ya ndege na kuwaua wote ili kutokomeza chanzo cha maambukizi kwa binadamu. Pili ni kutokuwa karibu na kuku walioambukizwa virusi vya homa ya mafua ya ndege. Wafanyakazi wanaonyunyiza madawa ya kuua vijidudu na wale wanaochinja kuku wanaoshukiwa kuambukizwa virusi, wanapaswa kupewa madawa ya kinga kabla ya kufanya shughuli zao, na wanapaswa kuzingatia usafi, kuvaa vitambaa vya kufunika mdomo, kuvaa mipira ya mikonoi na nguo maalumu za kinga. Baada ya kumaliza kazi zao, wanapaswa kuua vijidudu miilini mwao. Na tatu ni kuchunguza kwa makini watu waliokuwa karibu na kuku walioambukizwa virusi vya homa ya mafua ya ndege, na kuwatenga watu waliokwisha ambukizwa virusi hivyo na kuwatibu haraka.

    Kwa watu wa kawaida, wataalamu wanashauri kuwa wakati wanapopika mayai na nyama ya kuku, wanapaswa kuyachemsha mpaka viive vizuri. Kwa kawaida, virusi vinakufa katika halijoto zaidi ya nyuzi 70, kwa hivyo binadamu walila nyama za kuku zilizopikwa, hawawezi kaambukizwa maradhi hayo.

    Ni tofauti na virusi vya SARS vilivyoibuka mwaka 2003 barani Asia, virusi vya homa ya mafua ya ndege siyo vya aina mpya. Mtaalamu wa Wizara ya kilimo ya China Bw. Jia Youling alisema kuwa, mapambano dhidi ya maambukizi ya homa ya mafua ya ndege yalianza miaka zaidi ya mia moja iliyopita, hivyo nchi nyingi zimekuwa na uzoefu katika udhibiti wa maambukizi ya maradhi hayo. Pia alisema, kutokana na uzoefu wa udhibiti wa nchi mbalimbali, homa kali ya mafua ya ndege yanapoibuka, sehemu zote zenye maambukizi zinatakiwa kuwekwa kwenye karatini bila kusita na kuzishughulikia ipasavyo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-03-03