Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-21 22:02:19    
Barua za wasikilizaji 21/3/2004

cri
    Msikilizaji wetu Bennard Atsango Shivoga wa sanduku la posta 21606 Nairobi Kenya ametuletea barua akisema kuwa kwanza kabisa angependa kupongeza wafanyakazi wa Radio China kimataifa kwa juhudi zao kubwa sana kwa kuwaletea habari kemkem kuhusu maisha na utamaduni wa nchi ya China, na pia anapenda sana habari muhimu kuhusu China na sehemu za ulimwengu zilizotolewa na idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa, ambazo zinawafurahisha watu wa Kenya.

    Anasema, amefurahishwa sana na jinsi China inavyoendelea katika mambo ya kiuchumi, kilimo, michezo na utamaduni wao kutokana na matangazo ya CRI. Lakini maoni yake hasa kuhusu idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa ni kwamba muda ni mfupi sana na mambo ni mengi ambayo wataka kujua kwa urefu, kwa hivyo maoni yake ni kwamba Radio China kimataifa iongeze muda wake wa matangazo ili wapate mambo muhimu zaidi ya China.

    Msikilizaji Tomas M.K.Kiizoya ambaye barua zake huhifadhiwa na Embassy of Finland sanduku la posta 30379 Nairobi Kenya anasema katika barua yake kwamba, vipindi vya Radio China kimataifa vimeanza kurushwa nchini Kenya katika English Service KBC kuanzia tarehe mosi Septemba mwaka huu vinasikika nchini kote Kenya katika saa 11 hadi saa 12 jioni. Hapo Nairobi vinasikika katika mita 95.6 ya FM, 747khz, 100 km na 160 km.

    Anasema, mambo yaliyomo katika vipindi ni habari na maelezo baada ya habari, yeye anavipenda vipindi vyote. Kuhusu salamu zenu, na vipindi maalum mbalimbali kama vile jifunze kichina, anaona kwa kweli kichina ni kizuri kujifunza lakini ni kigumu kujifunza. Anavipenda vipindi vingine kama wapenzi wa michezo, vijana, nchi yetu mbioni, klabu ya utamaduni, muziki wa kichina, daraja la urafiki kati ya China na Afrika na kadhalika, na kipindi kinachopendwa zaidi na wasikilizaji wa Afrika ni salamu zenu na sanduku la barua. Salamu zenu inarushwa kila siku. Ameanza kusikiliza vipindi vya CRI hasa vipindi vya kiswahili kuanzia 11.30 hadi 12 jioni. Anasema, Radio China kimataifa ndio mambo yote, anaomba Mungu awabariki wahusika.

    Bwana Elisha Mudaki wa sanduku la posta 30379 Nairobi Kenya anasema katika barua yake kwamba, shukrani kwa kipindi mlichoanzisha ambacho kinaendelea katika idhaa ya kiingereza ya KBC kuanzia saa 11 hadi saa 12 jioni, yeye mwenyewe amefurahishwa na taarifa zetu za habari na maelezo baada ya habari. Hasa amependezwa na kipindi cha jifunze kichina, ambacho ni kipindi kizuri, ingawa kingali kigumu, lakini ana hakika kwamba hivi karibuni atajua kichina, anasema muziki wetu wa kichina unampendeza sana.

    Anasema mwishoni kwamba tunaposema majina yetu, tusitamke kwa haraka, maana hawawezi kushika matamshi, na pia kama ingewezekana wangependa saa ibadilishwe iwe kuanzia saa kumi na moja unusu hadi kumi na mbili unusu, ili wengi wawe ndani ya manyomba, yeye atakuwa shabiki wetu na ikiwa kutatoa kosa atajaribu kutuelezea. Na angependa kujua je, kuna kiswahili kinachoongea nchini China? Maana kiswahili cha mtangazaji ni kizuri sana, anataka sisi tunamjibu.

    Tunapenda kumwambia kwamba, nchini China hakuna lugha ya kiswahili, lakini wapo watu wengi waliojifunza kiswahili kwa ajili ya kushughulikia kazi ya kiswahili, watangazaji wetu wa kiswahili walisoma kiswahili nchini China, na wengi waliwahi kusoma nchini Tanzania na Kenya, hata mpaka sasa wako wanafunzi wengi wanaosoma kiswahili katika chuo kikuu cha Radio cha Beijing na chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing.

    Msikilizaji wetu Ally Omar Seif wa Mlindo, Pandani Wete, Pemba sanduku la posta 114 Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, anapenda kuchukua fursa hii kutushudhuru sana kutokana na ushirikiano kati yetu na yeye msikilizaji wetu wa kudumu, pamoja na yote hayo, anashukuru kwa kumtumia barua kumjulisha hali mbalimbali.

    Anasema angependa kutuarifu kwamba, bado angali msikilizaji wetu, lakini baadhi ya wakati hawezi kupata vizuri matangazo yetu, ila anazidi kutupongeza na kutupa mkono wa pongezi kutokana na kuanzishwa kwa mawasiliano ya utangazaji kati ya CRI na KBC, ingawa yeye hayumo katika usikilizaji lakini yuko pamoja na sisi ila hali ya kutumia barua ni ngumu kutokanana na hali ya kimaisha, pamoja na klabu yake ya wasikilizaji ambayo jina lake bado hajalituma katika idhaa yetu.

    Na mwisho anatoa mapendekezo akisema kuwa, kwa kweli CRI ni radio inayothamini wasikilizaji wake kuliko radio zote, kwa hivyo vipindi vya idhaa vimepangika vizuri na kuvutia, ila kipindi cha Tazama China, na kuwa nami jifunze kichina vingeongezewa muda japo dakika 3, suala hilo tumewafahamisha wasikilizaji wetu mara kwa mara kwamba, kutokana na mpango wetu uliothibitishwa na mamlaka ya CRI, si rahisi kuongeza au kupunguza muda wa vipindi vyetu, lakini huenda kila baada ya muda tunaweza kufanya mpangio mpya kuhusu vipindi vyetu, ama wasikilizaji wetu wana maoni na mapendekezo, tutayazingatia kwa makini.

    Msikilizaji wetu Peter A.Tungu wa Don Bosco Secondari school sanduku la posta 434-didia, Shinyanga Tanzania anasema katika barua yake kwamba, yeye ni mvulana mwenye umri wa miaka 18 anasoma kidato cha tatu katika sekondari ya Don Bosco. Yeye pia ni mpenzi sana wa kusikiliza idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa.

    Anasema lengo la barua yake ni kutaka kutoa maoni juu ya vipindi na matangazo yetu, kwamba, yeye ni mmojawapo wa wasikilizaji wetu, anawapongeza sana kwa matangazo yetu yanayorushwa moja kwa moja kutoka China, kwani yanampasha habari mbalimbali pamoja na matukio yanayojiri hapa duniani, hivyo ni mojawapo ya maoni yake kwamba, tuendelee kurusha na kuimarisha matangazo yetu.

    Anasema, kuhusu vipindi vyetu kwa kweli anausifu sana mpangilio na mfululizo wa vipindi vyetu, yaani vinampa hamu ya kuendelea kusikiliza, kwani mpangilio mzuri unawafurahisha wasikilizaji. Hivyo maoni na mapendekezo yake kwa ujumla wanaomba tuendelee kuwarushia matangazo yetu na pia tuimarishe vipindi. Asante sana ndugu Peter A. Tungu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-03-21