Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-23 16:07:03    
Maisha ya watu wanaoishi pembeni mwa Mfereji Jinghang

cri

    Katika sehemu ya mashariki ya China, upo mfereji mkubwa wenye urefu wa kilomita karibu 1,800. Kwa kuwa unaunganisha mji mkuu Beijing na mji mwingine Hangzhou, unaitwa mfereji wa Jianghang, ambao ni mrefu kabisa duniani.

    Katika historia ya miaka zaidi ya 1,400, mfereji wa Jinghang ulifanya kazi muhimu ya usafiri kati ya sehemu za kaskazini na kusini za China. Ustawi wa Hangzhou, mji uliopo kusini kabisa, pia ulitokana na mfereji huo, ambapo katika miaka elfu moja iliyopita, ulikuwa mji mkubwa maarufu kusini mwa China. Je, hivi sasa, katika mji huo, vipi maisha ya wakazi wanaokaa kando ya mfereji huo?

    Katika mfereji wa Jinghang, siku zote huwa kuna meli nyingi zinazosafiri. Siku nenda siku rudi, meli hizo zikichukua wasafiri na mizigo mbalimbali zinafanya safari mjini Hangzhou.

    Barabara ya Xiaohe ni kongwe na ipo karibu na mfereji, ambapo nyumba za mbao zenye orofa mbili zimejipanga moja baada ya nyingine barabarani. Familia ya mama Han yenye vizazi vitano imekaa hapa kama jirani ya mfereji kwa miaka zaidi ya 100.

    Anasema, "Pamoja na mama yangu, tumekaa hapa kwa miaka 114. Mimi nina umri wa miaka 83 mwaka huu, dada yangu ana umri wa miaka 89. Tunaupenda sana mfereji. Tulizaliwa hapa, tulikua hapa. Mimi na dada yangu, kwa jumla tuna watoto na majukuu zaidi ya 30".

    Mtaa wa Can Huayuan uliopo kando ya mfereji ulijengwa katika miaka ya karibuni. Mama Jiang Lanping mwenye umri wa zaidi ya miaka 70 ni mkazi wa mtaani. Kila anapoangalia mfereji uliopo karibu, anakumbusha picha ya miaka 40 iliyopita, ambapo maji yalikuwa safi yenye samaki wengi.

    Anasema, "Sisi wakazi wa Hangzhou tunayo tabia ya kuwapa wajaza wazito chakula cha samaki iitwayo Crucian. Lakini wakati ule ilikuwa hakuna samaki ya namna hii kuuzwa sokoni, tunafanyaje? Mume wangu alitembeatembea, akaona watu waliovua samaki kando ya mfereji. Alijaribu kuvua, na akapata debe zima la samaki ya namna hii katika adhuhuri. Nilimwuliza samaka wametoka wapi? Alijibu kutoka kwa mfereji."

    Mama Jiang aliongeza kusema kuwa, miaka 40 iliyopita, mfereji ulikuwa safi sana. Wakazi walioishi pembeni mwa mfereji huo walitumia maji ya mfereji kufulia nguo, kuosha mchele na mboga.

    Tokea miaka ya 50 ya karne iliyopita, viwanda vingi vilianza kujitokeza mjini Hangzhou. Kutokana na ufinyu wa mawazo ya kuhifadhi mfereji, wakazi walipoongeza uzalishaji viwandani na kuingia kwenye maisha ya burudani, walitoa maji machafu katika mfereji bila ya kuyashughulikia. Na wakalipizwa kisasi na mfereji kwa haraka sana.

    Mama Huang Baoyu anasimulia, akisema, "Kutokana na uchafuzi, katika miezi kadhaa kila mwaka, hatukuweza kunuwa maji ya mfereji, kwa kuwa, maji yalitoa harufu mbaya, na wali uliopikwa kwa kutumia maji ya namna hii pia ulitoa harufu mbaya."

    Katika miaka ya karibuni, serikali imetambua umuhimu wa mazingira na wakazi pia wamekubali wazo la kuhifadhi mazingira, ambapo suala la uchafuzi wa mfereji pia limefuatiliwa na watu. Serikali ya mji wa Hangzhou ilitoa uamuzi wa kupiga marufuku kutoa maji machafu kwenye mfereji. Mbali na hayo, ilihamisha viwanda kadhaa vinavyoleta uchafuzi. Baadhi ya wakazi wanajitolea kusimamia ubora wa maji ya mfereji. Kila wanapogundua kitendo cha kutoa maji machafu katika mfereji, wanakizuia kwa wakati.

    Serikali ya mji wa Hangzhou ilitoa uamuzi mwaka jana kuwa, itafanya mpangilio na uboreshaji wa pande zote kwa mfereji wa kilomita 39 ndani ya mji huo pamoja na kando mbili za mfereji. Bw. Wu Weijin ambaye ni mhandisi wa ngazi ya juu anayeshughulikia mpangilio wa mji huo, anasema kuwa, mfereji huo utakuwa na ubora sawa na mto wa Seine nchini Ufaransa katika miaka 20 ijayo. Anasema, "Serikali ya mji wa Hangzhou imetangaza wazi uwezo wa mfereji katika pande 6 muhimu, nazo ni utamaduni, utalii, mazingira, biashara, makazi na usafiri wa meli. Lakini usafiri wa meli unapaswa kudhibitiwa ndani ya mji. Inatubidi kuweka mpango mpya wa mfereji, kuuhifadhi na kuuendeleza. Tunalenga kutumia miaka 10 hadi 20 kwa ajili ya kukamilisha kazi za kupanga upya majengo pembeni mwa mfereji, na kutengeneza sura mpya ya mfereji. Baada ya miaka 20, sehemu za kando za mfereji zitajulikana ulimwenguni kama sehemu nzuri za utalii, ambapo ubora wake utakuwa sawa na mto wa Seine."

    Kutokana na masimulizi ya Bw. Wu, tunaweza kubuni picha za kupendeza za mfereji katika siku za baadaye, ambapo utaweza kuchukua meli kuelekea moja kwa moja maziwa ya Qiantang na Xihu, ambayo ni maarufu kwa mandhari nzuri na kumbukumbu za kiutamaduni. Pia utaweza kupata burudani ya mandhari pembeni mwa mfereji, pamoja na barabara kongwe ambazo zimehifadhiwa kama zilivyokuwa miaka 100 iliyopita.

    Wakazi wanaoishi pembeni mwa mfereji wanatarajia siku ambayo mradi wa uboreshwaji wa mfereji utakapokamilishwa. Mama Huang Yubao alisema kuwa, atafurahi kuona sura mpya ya mfereji.

Idhaa ya Kiswahili 2004-03-25