Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-28 19:42:08    
Darizi za wakazak

cri
    Katika sehemu za mbuga ya Wakazak, Mkoa wa Xinjiang, ukitembea kila hema, utaona sanaa za kijadi za darizi. Sanaa za darizi zimekuwa vitu vya lazima vya wafugaji, hupamba kuta za hema au kutandikwa juu ya vitanda, viti na sakafuni. Wafumaji hutumia nyuzi sufu zenye rangi mbalimbali kutarizi juu ya mahameli za rangi nyeusi, nyekundu au zambarau kwa kufuata mabombwe ya pembe za ng'ombe, mbuzi na kulungu au maua na majani. Sanna zao huonesha hulka za mbuga kwa mistari minene na rangi angavu.

    Kina mama wa kabila la wakazak ni mahodari wa darizi. Wao hutumia saa kadha kumaliza darizi rahisi na ndogo, na kutumia miezi michache au nusu mwaka kutarizi sanaa kubwa. Wakati bibi arusi atakapofunga ndoa humpa bwana arusi sanaa zake ili kuonesha uhodari wake. Zamani walikuwa wakitarizi sanaa zao nyumbani kwa matumizi ya binafsi tu, lakini sasa kwa kufuata sera ya mageuzi, kina mama hao wameanzisha viwanda vya sanaa za darizi kutoa bidhaa zinazopendwa kwenye masoko ya nchini na ng'ambo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-03-28