Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-31 16:08:48    
Huduma za vikundi vya matibabu vinavyotembelea katika sehemu za makazi ya watu

cri
    Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na njia mpya ya kutoa matibabu nchini China, nayo ni vikundi vya matibabu vinavyotembelea watu vinaendelea katika sehemu nyingi nchini China. njia hiyo imekaribishwa sana na watu. Kutokana na ubora wa vikundi hivyo, watu wa maeneo hayo hawapaswi kwenda hospitali, na kutokuwa na wasiwasi wa kuambukizwa magonjwa mengine wakati wanapokuwa hospitali.

    Mama Zhou ana umri wa miaka 70, anaishi karibu na uwanja wa ndege wa Beijing. Siku moja, alijisikia vibaya ghafla, lakini hakutaka kwenda hospitali, hivyo familia yake ilipiga simu kwa kikundi cha matibabu. Baada ya dakika 10 tu, kikundi kimoja cha matibabu kilichoundwa na madaktari wa upimaji, X-ray, hifadhi ya afya waliwasili katika nyumba yake, walimtibu bi Zhou kwa wakati. Baada ya hapo, madaktari walimtembelea Bi Zhou kila siku, ili kujua hali ya maendeleo ya Mama Zhou   hadi alipopona kikamilifu.

    Kikundi hicho kilitoka Hospitali ya Gaobeidian ya Beijing, hospitali hiyo ina vikundi hivyo vitatu, kila siku, vinatembelea katika sehemu mbalimbali za makazi ya watu na kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa. Kama hospitali hiyo, hospitali nyingi za Beijing zimeanzisha vikundi hivyo na vituo vya matibabu katika sehemu mbalimbali za makazi ya watu. Katika sehemu nyingine nchini China, miji mingi mingine ilianzisha vikundi hivyo kwa ili kuwatoa urahisi kwa watu. Kwa mfano, kikundi cha matibabu cha gari kinachotembelea sehemu ya makazi ya watu kimeandaliwa kutoa huduma saa 24 kila siku.

    Vikundi vya matibabu vinafanana na hospitali mbalimbali zilizohamahama, sio kama madaktari wanapeleka madawa kwa wagonjwa peke yake, bali pia wanawapeleka wagonjwa wale wenye hali vibaya kwenye hospitali kubwa, na kueneza elimu za afya kwa wakazi.

    Utaratibu wa kutoza fedha hauna tofauti kwa hospitali, bila kujali wagonjwa kutibiwa hospitalini na nyumbani wanatozwa pesa kwa kiwango kimoja. Hivyo, watu wanapenda sana njia hiyo ya kutoa huduma ya matibabu.

    Miaka miwili iliyopita, sehemu mbalimbali zilizoko mbali na miji pia zilianzisha vikundi vya matibabu vinavyotembelea wagonjwa. Kuna kampuni moja ya China iliyoko mkoa wa Yunnan, Magharibi-Kusini ya China. Kwa kuwa, kampuni hiyo iko sehemu ya milimani, maisha ya wafanyakazi ni magumu. Zamani, wafanyakazi walipokuwa wagonjwa, ilikuwa ni vigumu sana kwao kutibiwa. Lakini sasa, tangu kuanzishwa kwa kikundi cha matibabu kinachotembelea wagonjwa katika sehemu hiyo, wafanyakazi wa kampuni hiyo hawana wasiwasi tena kuhusu afya zao. Mfanyakazi mmoja aitwaye Yang Wenmin alisema kuwa, kuna wakati mtoto wake wenye umri wa miaka miwili tu alikuwa na usingizi mzito kutokana na homa na mafua, na mvua ilikuwa inanyesha sana, na alikuwa na biashara nje. Katika hali hiyo ya dharura, mkewe alijaribu kupiga simu kwa kikundi cha matibabu? baada ya muda mfupi tu, madaktari wa kituo cha huduma ya matibabu ya mji wa Chuxiong, mkoani Yuan walifika nyumbani kwake na kumtibu mtoto wake, na hali ya mtotoa wake ilianza kubadilika na kuwa nzuri. Bw. Yang alisema kuwa, kikundi cha matibabu kilimwokoa mtoto wake.

    Lakini sasa bado hakuna vikundi vya matibabu vya kutosha katika vijiji vingi nchini China. Miaka mingi iliyopita, maendeleo ya huduma za afya vijijini yalikuwa ya polepole kuliko yale ya mijini. Asilimia 80 ya vifaa vya matibabu na hospitali ziliwekwa mijini. Katika vijiji vingi kuna hospitali ndogo tu, ambazo hazikuwa na vifaa vya matibabu na madaktari wa kutosha. Kutokana na hali hiyo, idara za wizara ya afya ya China ziliamua kuwa, zitapeleka vikundi vingi zaidi vya matibabu katika sehemu zilizoko mbali na miji ili kuwasaidia wakazi wa sehemu hizo kuboresha mazingira ya matibabu na kushirikiana na madaktari wa sehemu hizo kufanya kazi.

    Sasa, vikundi vingi zaidi vya magari vya matibabu kutoka mijini vinakwenda vijijini ili kutoa huduma za matibabu na kuwapelekea wakulima madawa. Ofisa mmoja wa Shirika la wanawake na watoto la China alijulisha kuwa, alianzisha kikundi kimoja cha matibabu chenye magari 200, ambapo kiliitwa "Magari ya afya kwa kina Mama", ili kuwasaidia wanawake kujenga afya katika sehemu za umasikini.

    Mbali na hayo, jumuiya ya kimataifa pia inazingatia mambo ya vikundi vya matibabu vilivyotembelea watu nchini China. Kwa mfano Kampuni ya Kodak ilitengeneza magari mapya ya huduma za matibabu kwa China, yanayoweza kutoa huduma nzuri zaidi kwa watu walioko sehemu za watu masikini.

    Lakini kwa kuwa, huduma ya kikundi cha matibabu haikuwekwa kwenye utaratibu wa kiserikali, wagonjwa wanapaswa kujigharamia wenyewe, hivyo, bado wagonjwa wengi wanakwenda kuwafuata madaktari hospitalini. Hivi sasa, idara za wizara ya afya ya China na usalama wa jamii zinajitahidi kuiweka huduma hiyo kwenye sera ya serikali. Wakati huo, wagonjwa wote wataweza kunufaika kwa urahisi na huduma ya vikundi vya matibabu vilivyotembelea watu.

Idhaa ya kiswahili 2004-03-31