Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-31 18:00:49    
maendeleo ya chumi kwenye sehemu zinazopitwa na mto Changjiang kutokana na kutumika njia ya usafirishaji kwenye sehemu ya Magenge Matatu

cri
    Lango la kudumu la mradi wa maji wa Magenge Matatu uliojengwa kwenye mto wa Changjiang ambao ni wa kwanza kwa ukubwa nchini China, lilianza kutumika mwezi Juni mwaka 2003 kwa usafiri wa meli. Wataalamu wanasema kuwa kadiri sehemu ya mto Changjiang kwenye Magenge Matatu inavyopanuka ndivyo usafirishaji kwenye mto wa Changjiang unavyokuwa muhimu zaidi kwa maendeleo ya uchumi wa sehemu wa mto Changjiang. Makala hiyo ni kuhusu maendeleo ya chumi kwenye sehemu zinazopitwa na mto Changjiang kutokana na kutumika njia ya usafirishaji kwenye sehemu ya Magenge Matatu.

    Mradi wa maji wa Magenge Matatu ya Mto Changjiang, China, ni mmojawapo miongoni mwa miradi mikubwa ya maji ulimwenguni kwa hivi sasa. Mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kuzuia mafuriko ya maji, kuzalisha umeme na usafirishaji majini. Baada ya kujengwa kwa miaka 10, uchukuzi wa majini wa Magenge Matatu umeleta manufaa. Mto Changjiang unaojulikana kama kiungo kati ya sehemu ya Mashariki, katikati na magharibi, unasifiwa kama njia ya usafirishaji toka zamani. Lakini kutokana na kuwa na sehemu nyingi zenye maji yaendayo kwa kasi na sehemu zenye maji machache kwenye sehemu za kati na mwanzo za mto Changjiang, maendeleo ya uchukuzi wa majini yalikwamishwa vibaya. Profesa Zhen Jing-dong wa taasisi ya utafiti wa maendeleo endelevu ya sehemu ya bwawa la Magenge Matatu ya chuo kikuu cha mambo ya viwanda na biashara cha Chongqing, alimwambia mwandishi wetu wa habiri kwamba baada ga maji ya bwawa la Magenge Matatu kufikia kina cha miaka 135, mabadiliko makubwa yatakayotokea ni kuboreshwa kwa mazingira ya usafirishaji. Alisema kuwa hapo awali, tofauti ya kina cha maji kati ya sehemu ya juu na ya chini kwenye umbali wa kilo mita 660 kutoka Chongqing, mji mkubwa kwenye sehemu ya magharibi nchini China hadi Yichang, mahali uliko ukingo mkubwa wa maji wa bwawa la Magenge Matatu ni zaidi ya mita 120 na kuwa na sehemu 139 zenye maji machache ambapo ile kina kifupi zaidi ni kiasi cha mita 100, na yenye njia moja tu kwa usafiri wa mota-boti, hivyo ni ya hatari sana. Hivi sasa sehemu hizo zimekuwa na maji mengi, kiasi ambacho hati kundi la moto-boti zilizobeba jumla ya tani elfu 10 ya mzigo, linaweza kusafiri moja kwa moja kutoka Shanghai ambao ni mji mkubwa wa viwanda na biashara kwenye sehemu ya pwani ya mashariki ya China hadi mji wa Chongqing, tena gharama ya usafirishaji itapungua kwa kiwango kikubwa.

    Profesa Zheng Jing-dong alisema kuwa baada ya ujenzi wa mradi wa Magenge Matatu kukamilishwa kabisa, maji ya bwawa yataongezeka kina kwa zaidi ya mita 40 ambapo njia ya usafirishaji kati ya Yichang na Chongqing itakuwa na maji yenye kina kirefu na uwezo wa usafirishaji utakuzwa kwa kiwango kikubwa, inakadiriwa kuwa uwezo wa usafirishaji utakuzwa hadi tani milioni 50 kwa mwaka kutoka milioni 10 ya hivi sasa.

    Baada ya kutumika kwa njia ya usafiri kwenye sehemu ya Magenge Matatu, mji wa Chongqing ambao uko kwenye sehemu ya mwanzo ya mto Changjiang, utapata manufaa makubwa zaidi. Kwani Chongqing itakuwa bandari moja muhimu katika sehemu ya magharibi ya China kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya usafirishaji na uchumi wake kwa haraka. Juu ya suala hilo profesa Zheng Jing-dong alisema kuwa njia ya usafirishaji ya zamani kwenye mto Changjiang ilikwamisha sana maendeleo ya uchumi ya Chongqing. Baada ya bwawa la Magenge Matatu kulimbikiza maji, mazao mengi ya sehemu ya kusini magharibi yataweza kusafirishwa kwa sehemu mbali mbali kupitia mto Changjiang, jambo ambalo litahimiza shughuli za usambazaji bidhaa za sehemu ya Chongqing. Aidha, mji wa Chongqing haukuwa na maingiliano na sehemu nyingine kutokana na mawasiliano magumu, sasa kuboreshwa kwa njia yauchukuzi majini kutachangia sana maendeleo ya uchumi ya sehemu hiyo.

    Habari zinasema kuwa katika miaka 10 ijayo, mji wa Chongqing utatenga fedha za RMB zaidi ya bilioni 14 ambazo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 1.7 kwa ujenzi wa miundo-mbinu ikiwemo bandari. Pamoja na kuonekana nafasi ya usafirishaji kwenye sehemu ya Magenge Matatu, makampuni mengi makubwa ya meli ya Chongqing yanaanza kununua meli mpya ili kupata nafasi kubwa katika ushindani wa soko la uchukuzi. Kuboreshwa kwa mazingira ya uchukuzi majini pia kumeleta manufaa kwa makampuni mengine ya huko. Makampuni yale makubwa yaliotegemea njia za usafirishaji za reli na barabara kama kampuni ya vyombo vya umeme ya Changhong na kampuni ya pombe ya Wuliangye, sasa yanavutiwa na bei nafuu ya usafirishaji wa majini ambapo yanasafirishwa bidhaa zao kwenye mto hadi mji wa Shanghai, kisha zitasafirishwa hadi nchi za nje. Baada ya kuchambua kwa makini hali ya usafirishaji wa majini, kampuni ya magari ya marekani, Ford, imechagua mji wa Chongqing kama ni kituo chake cha kuingia katika masoko ya China.

    Kuboreshwa kwa mazingira ya uchukuzi kwenye mto Changjiang, si kama tu kutanufaisha sehemu za kati na juu za mto huo, bali pia kutachangia maendeleo ya uchumi ya sehemu zote zinazopitiwa na mto huo, mtafiti wa taasisi ya uchumi ya chuo kikuu cha sayansi na jamii ya China Bw. Chen Yao alisema kuwa mwanzoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita, serikali ya China iliweka lengo la ukuzaji wa uchumi wa sehemu zinazopitiwa na mto Changjiang kutokana na ustawishaji wa sehemu ya delta ya mto huo, ambalo litatimizwa kwa karaka zaidi kutokana na kutumika kwa njia ya usafirishaji ya mto Changjiang, alisema kuwa kukuzwa kwa uwezo wa usafirishaji kwenye Magenga Matatu kunamaanisha kwamba thamini ya njia dhahabu ya usafirishaji ya mto Changjiang inaongezeka, na italeta athari kubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya sehemu zote zinazopitwa na mto huo.

    Bw. Chen alisema kuwa sehemu hizo zina rasilimali nyingi za madini zmbazo zitakuwa rahisi kusafirishwa kwenda sehemu ya viwanda ya mashariki au moja kwa moja hadi nchi za nje.

    Wataalamu walisema kuwa kuna matatizo mengi yanayotakiwa kutatuliwa kabla ya kupata ufanisi mkubwa wa kiuchumi kutokana na matumizi ya njia ya usafirishaji ya sehemu ya Magenge Matatu yakiwa ni pamoja na marekebisho ya mto katika sehmu za mwanzo na katikati ya mto Changjiang.

2004-03-31