Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-07 11:21:34    
Uhifadhi wa mimea adimu katika eneo la magenge matatu

cri

    Mradi wa magenge matatu ni mradi wa hifadhi ya maji unaojengwa kwenye sehemu iitwayo magenge matatu ya mto Changjiang, nchini China. Hivi sasa, bwawa la mradi huo limemaliza hatua ya mwanzo ya kulimbikiza maji, ambapo kina cha maji kimepanda juu na baadhi ya mimea kuzama. Katika majadiliano kuhusu manufaa na athari mbaya kutokana na mradi wa magenge matatu, suala moja linalofuatiliwa na watu ni uhifadhi wa mimea adimu ambayo ni maalumu katika eneo la ujenzi wa mradi huo. Pamoja na majadiliano hayo, hatua zimechukuliwa ili kuhifadhi mimea hiyo adimu. Makala hii ni kuhusu Bw. Xiang Xiufa na bustani yake ya mimea adimu.

Mandhari ya kupendeza ya magenge matatu.

    Siku moja ya hivi karibuni, mvua ya manyunyu ikinyesha, nilitembelea bustani ya mimea adimu kwenye eneo la magenge matatu. Katika bustani hiyo, ipo miti mikongwe na mirefu sana, na sauti za maji na milio ya ndege husikika wakati wote. Bw. Xiang Xiufu, ambaye ni mkuu wa bustani hiyo alinielezea tabia za kila aina ya mimea, hali ambayo ilionekana kuwa, yeye ni mtaalamu wa mambo ya mimea. Lakini ukweli ni kwamba, Bw. Xiang alikuwa mfanyabiashara wa mazao ya maji kwa miaka 6 iliyopita. Kwa nini ameacha biashara yake na kujishughulikia uhifadhi wa mimea adimu?

    Haya, hebu turudi katika miaka minane iliyopita, ambapo jambo lisilotarajia lilibadilisha maisha yake.

    Siku za nyuma, Bw. Xiang aliposafiri kwenye magenge matatu, ambapo pia ni mahala maarufu pa utalii, alishuhudia wakulima wenyeji wakikata miti mikongwe ili kupata kuni. Alisikitika sana, kwa vile miti mirefu na mikubwa ya namna hii, ilikuwa imekua kwa miaka mia kadhaa hata zaidi ya elfu moja. Wakati huo, ujenzi wa mradi wa magenge matatu ulikuwa umeanza kwa miaka miwili. Bw. Xiang alijiuliza, ipo miti mikongwe mingapi kando za mto Changjiang? Na kutokana na eneo kubwa mno la ujenzi wa mradi wa magenge matatu, kumekuwa na athari gani kwa mimea, hususan mimea adimu kwenye eneo hilo?

    Alipokuwa akirudi nyumbani kutoka safari hiyo, alivutiwa sana na mimea iliyo kando za mto Changjiang. Alimwajiri mtaalamu wa mambo ya miti kufanya uchunguzi, na kupata matokeo kwamba, baada ya kulimbikiza maji kwa mradi wa magenge matatu, aina zaidi ya mia moja ya mimea adimu iliyopo kando mbili za mto Changjiang itazama katika maji. Ingawa alikuwa anaendesha kwa mafanikio maeneo mawili ya kufuga mazao ya maji, akaamua kuacha biashara na kusaidia mimea.

    Mwaka 1998, kwenye mkutano mmoja ulioandaliwa na serikali, Bw. Xiang alitoa pendekezo la uhifadhi mimea adimu ya eneo la magenge matatu. Pendekezo lake lilifuatiliwa na idara husika za serikali, na katika muda wa miezi mitatu tu, shughuli za kuweka mpango na kuchagua mahala pa bustani zikakamilishwa. Idara ya mambo ya miti ilitenga Yuan za Renminbi milioni 320, ambazo ni sawa na dola za kimarekani milioni 40, kwa ajili ya uhifadhi wa mimea adimu ya eneo la magenge matatu. Na taasisi za kisayansi, ikiwemo taasisi ya mimea iliyo chini ya Taasisi ya Sayansi ya China iliunda tume ya wataalamu kufanya utafiti kuhusu mimea hiyo.

    Bw. Xiang alimaliza biashara yake ya mazao ya maji na kuanza kujishughulisha na uhifadhi wa mimea adimu. Kuanzia hapo, aliteuliwa kuwa mkuu wa bustani ya mimea adimu. Akishirikiana na wataalamu, walianza kutafuta mimea adimu iliyokabiliwa na hatari ya kuzama katika maji mmoja hadi mwingine. Akikumbusha anasema, "Tulifanya uchunguzi kwenye sehemu zilizo mbali na miji, hatukufahamu kuwa, kuna nyoka wenye sumu, wala sikutambua baada ya kuumwa na nyoka. Tuliporudi kwenye kijiji, weneyji waliniambia kuwa, nimegongwa na nyoka wenye sumu, nikaona kuwa, mikono yangu ilikuwa imevimba. Nikanusurika kutokana na mitishamba ya wenyeji."

    Nyoka wenye sumu imemwachia Bw. Xiang kumbukumb ya daima, sasa kidole chake kilichoumwa hakifanyi kazi tena. Na mfupa mmoja wa ubavuni mwake ulivunjika wakati wa kuhamisha mmea mmoja mkubwa wa ajabu.

    Kadiri ujenzi wa mradi wa magenge matatu unavyoendelea siku hadi siku, ndivyo Bw. Xiang anavyozidi kuwa na shughuli nyingi. Anatafuta tafuta mimea adimu kando ya mto Changjiang, halafu kuihamisha na kuipanda kwenye bustani yake. Hivi sasa, mimea adimu zaidi ya aina 100 inakua kwenye bustani hiyo yenye hekta 80 iliyopo mjini Chongqing, kusini magharibi ya China. Mwaka 2003, bwawa la mradi wa magenge matatu lililimbikiza maji, lakini haijatokea kutokemezwa kwa mimea na wanyama walioishi katika maeneo yaliyozama kwenye maji yaliyopo kando mbili za mto Changjiang. Hakufanya kwa bure jitihada za miaka 6 wakati anapoangalia mimea aliyohamia mwenyewe kwenye bustani yake, Bw. Xiang anafurahi sana.

    "Wakati wa kugundua aina mpya ya mmea, nafurahi na kusisimka sana. Halafu nikamhamia na kupanda kwenye bustani, ambapo mmea anaweza kukua, hali ambayo inanipeleka kuona kuwa, shughuli hii ninayofanya ni yenye umuhimu."

    Kwa maoni ya Bw. Xiang, mimea yote ni ya hai, na ina busara. Kwenye sura ya pili ya kadi ya jina lake, inachapishwa kauli isemayo, "Binadamu huwa na dunia moja, lakini dunia haiwezi kuwa na binadamu peke yake."

    Kwenye bustani yake ya mimea adimu, kuna mimea yenye thamani ya juu inayoweza kutengenezwa kuwa madawa. Watu wengine walimshawishi Bw. Xiang auze mimea hiyo kwa bei kubwa, lakini akawafukuza akiwa na hasira. Wengine wanamcheka na kusema yeye ni mpumbavu kwa vile, anajishughulikia uhifadhi wa mimea ambao ni jambo lisilo na faida, lakini Bw. Xiang amaacha biashara kubwa zinazoweza kuchuma fedha nyingi.

    Ofisi ya Bw. Xiang ipo nyumbani kwake, ni chumba kisichozidi mita 10 za mraba, ambacho kimejaa vitabu kuhusu uhifadhi wa mimea. Alisema shabaha lake ni kujenga bustani yenye aina nyingi kabisa za mimea nchini China, na kuanzisha ghala ya geni za mimea inayokabiliwa na hatari ya kutoweka.

Idhaa ya Kiswahili 2004-04-08