Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-07 18:55:56    
Elimu na mtandao wa internet nchini China

cri
Hivi sasa nchini China, watu wengi zaidi wanapenda kupata elimu kupitia mtandao wa internet. Wanafunzi wanaweza kusoma kwa kutumia kompyuta zenye picha na sauti; na wafanyakazi wanaweza kuendelea masomo yao kupitia mtandao wa internet. Hivi sasa kujifunza kwa kupitia mtandao wa internet kunakaribishwa na watu wengi zaidi nchini China.

    Kutokana na maendeleo makubwa ya kazi ya mtandao wa internet ya China, watu wengi zaidi wanajifunza kwa kupitia njia mtandao wa internet. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa watu wanaotumia mtandao wa internet wanafikia milioni 80, na kati ya hao watu wenye umri chini ya wa miaka 30 wanachukua 70%. Mtandao wa internet umekuwa njia muhimu kwa watu kupata elimu, kubadilishana mawazo na kucheza michezo.

    Mbali na hayo, ikilinganishwa na njia ya kujifunza darasani, mtandao wa internet una faida nyingi zaidi. Kwa mfano, kiuchumi ni rahisi zaidi, , kutokuwa na kikwazo cha wakati, ni rahisi kubadilishana mawazo na watu wengine, kupata habari zenye picha, sauti na maneno kwa wakati huo huo. Mbali na hayo, bila kujali umri wa mwanafunzi ni mkubwa au mdogo, anaweza kujifunza kwa kupitia mtandao wa internet.

    Sasa, elimu ya mtandao wa internet ya China ina sehemu tatu. Kwanza kutoa elimu ya kimsingi kwa wanafunzi wa shule za kimsingi na sekondari; pili, kutoa elimu kwa watu wazima; na tatu, kuwaandaa wafanyakazi ufundi wa aina mbalimbali.

    Chini ya hali hiyo, shule za mtandao wa internet za China zinaendelea kwa kasi kubwa. Miongoni mwa shule hizo, shule za kimsingi za mtandao wa internet ambazo zinatoa elimu kwa wanafunzi wa shule za kimsingi na sekondari zimekuwa sehemu muhimu katika elimu ya kimsingi nchini China. Kwa mfano, mwezi May, June mwaka 2003, hali ya uambukizaji wa ugonjwa wa SARS ilikuwa inateseka sana mjini Beijing, wanafunzi mamia wa shule za msingi na sekondali walikuwa wanapaswa kusimama nyumbani, lakini waliweza kujifunza kwa kutumia mtandao wa internet na televisheni. Wanafunzi na walimu walifanya mawasiliano kwa kupitia mtandao wa internet. Wanafunzi wengi wa shule za msingi na sekondari waliona kuwa, kujifunza katika mtandao wa internet kunawasaidia wanafunzi kukuza maeneo yao ya elimu, wanaweza kupata elimu nyingi ambazo hazikuweza kupatikana darasani.

    Kutokana na mahitaji ya jamii, elimu ya mtandao wa internet kwa watu wazima inaendelea kwa kasi kubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa, sasa kuna vyuo vikuu 68 vilianzisha masomo ya elimu ya mtandao wa internet nchini China, wanafunzi walioandikisha shuleni wamefikia milioni 1. vyuo vikuu hivyo si kama tu vilianzisha masomo kwa wanafunzi wanaosoma shuleni, bali pia vilianzisha masomo yasiyokuwa na digri kes wafanyakazi ili kuwakidhi mahitaji yao kazini.

    Chini ya mwendo huu mzuri wa elimu ya mtandao wa internet, makampuni na vikundi mbalimbali vya jamii pia vilianzisha masomo ya mtandao wa internet, kwa mfano masomo ya mitihani ya TOEFL, GRE, kompyuta n.k. na makampuni kadhaa yaliwaandaa wafanyakazi wao kwa kupitia mtandao wa internet ili kuongeza uwezo na ubora wa wafanyakati. Bibi yanhua anafanya kazi katika Kampuni ya kigeni alisema kuwa, sasa watu wengi wanashikilia kujifunza wakati wa kupumzika, kujifunza shuleni si njia moja tu ya kupata elimu, kila wakati, ukitembelea mtandao wa internet unaweza kujiongeza elimu na uwezo.

    Habari zinasema kuwa, idara husika za elimu ya China zilianzisha mradi moja uitwao "Ujenzi wa masomo ya elimu ya mtandao wa internet", mradi huo ulipangwa kuanzisha masomo ya aina 200 na akiba ya mitihani ya aina mbalimbali, ambapo vyuo vikuu kadhaa vya elimu ya mtandao wa internet vinatazamiwa kupewa misaada kutokana na mpango huo. Mbali na kuviunga mkono vyuo vikuu vilivyoko sehemu tajiri, katika sehemu ya Magharibi ya China ambayo uchumi wa sehemu hiyo si nzuri sana pia itapewa misaada mikubwa, hivyo wanafunzi wa sehemu nyingi za China wanaweza kufaidiwa kwa njia hiyo yenye teknolojia ya hali ya juu, na ubora nzima wa elimu ya juu unainukiwa sana nchini China.

    Wataalamu walisema kuwa, elimu ya mtandao wa internet itakuwa njia mpya yenye ubora wa upesi zaidi, maeneo makubwa zaidi nchini China. Pamoja na elimu ya darasani, elimu ya radio, elimu ya televisheni, zimekuwa mfumo wa elimu wenye ubora nyingi. Tunaimani kuwa, teknolojia inayoendelea kwa kasi kubwa siku hadi siku zinawawezesha wachina wengi zaidi kujiboresha kwa kupitia mtandao wa internet.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-07