Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-14 15:14:51    
Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha Qinshan

cri

Mwezi Oktoba mwaka 2003, viongozi na wataalamu wa nishati ya nyukilia wa China na Canada walifika huko Haiyan mkoani Zhejiang, Mashariki ya China kushiriki kwenye sherehe ya kukamilika kwa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha Qinshan cha kipindi cha tatu.

    Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha Qinshan cha kipindi cha tatu ni kituo cha tano cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia kilichojengwa nchini China, ambacho pia ni kituo cha kwanza chenye kinu kinachoendeshwa kwa nguvu ya maji kutonana na nishati ya nyuklia. Kilitumia teknolojia ya Canada kuhusu kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia. Kituo hicho kina seti mbili za mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia zenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa megawati 700, uwekezaji vitega uchumi umefikia dola za kimarekani bilioni 2.8, huo ni mradi mkubwa kabisa wa ushirikiano kati ya China na Canada mpaka sasa. Tangu mradi huo ulipoanzishwa, ulizingatiwa sana na serikali za nchi hizi mbili. Mwaka 1996, mawaziri wakuu wa nchi hizi mbili walihudhuria sherehe ya kutia saini mkataba wa mradi wa huo. Sasa viongozi wa serikali za nchi mbili walisherehekea kwa pamoja kukamilika kwa mradi huo. Kituo cha kuzlaisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha kipindi cha tatu cha Qinshan kilisifiwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa katika matumizi ya kiamani ya nishati ya nyukilia kwa ushirikiano wa China na nchi za nje .

    Meneja Mkuu wa Kampuni ya viwanda vya nishati ya nyukilia ya China Bw. Kang Rixin alisema kuwa, kituo kicho kilijengwa tayari kwa sifa bora ni ufanisi mzuri chini ya ushirikiano wa kirafiki wa mafundi na wafanyakazi wa China na Canada. Meneja mkuu Kang anasema:

    "Ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha kipindi cha tatu cha Qinshan kilichukua nafasi ya kwanza miongoni mwa vituo mbalimbali vya aina hiyo duniani. Mbali na hayo, teknolojia ya kituo hicho iko mbele duniani. Mafanikio hayo mazuri yalipatikana kutokana na jitihada kubwa za nchi mbili. Watu wa China au wa Canada, wote tunafurahia sana."

    Ujenzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha kipindi cha tatu cha Qinshan ulianza kujengwa Mwaka 1998, katika muda usiofikia miaka minne na nusu, mashine za seti ya kwanza zilianza kufanya kazi, zikaanza kuzalisha umeme kwa zaidi ya mwezi mmoja kabla ya mpango uliowekwa. Miezi sita tu baada ya hapo, mashine za seti ya pili zilianza kufanya kazi ya kuzalisha umeme, ujenzi wake ulikamilika mapema kwa miezi minne kabla ya mpango uliowekwa, na matumizi ya ujenzi wa mradi huo yalipungua kwa 10% kuliko bajeti ya awali. Mafaniko ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha kipindi cha tatu cha Qinshan yalitokana na ushirikiano mzuri wa wajenzi na mafundi wa China na Canada. Tangu kituo hicho kilipoingia katika kipindi cha majaribio na marekebisho, Bw. Wan Wensheng alikuwa kiongozi wa kazi hiyo. Kutokana na mkataba uliowekwa, watu wa Canada walielekeza kiteknolojia, na kazi za kufanya majaribio na marekebisho ya mashine zilifanywa na wachina. Mwanzoni, kutokana na tofauti za lugha na desturi za kufanya kazi kwa pande hizo mbili, walikuwa na matatizo ya kubadilishana mawazo, lakini baada ya jitihada za wafanyakazi wa pande mbili , mwishowe wakaweza kushirikiana na kupata maoni ya pamoja wakahakikisha ujenzi wa mradi unaendelea vizuri. Bwana Wang anasema:

    " Kwenye kipindi cha kufanya majaribio na marekebisho ya mashine, ili kuhakikisha ujenzi wa mradi unaendelea bila vikwazo, pande mbili ziliimarisha maelewano na maingiliano, na wafanyakazi wa China waliwawezesha wafanyakazi wa Canada kuelewa desturi za wachina katika kufanya kazi, na wachina pia walijitahidi kuambatana na utaratibu wa watu wa Canada. Kwa ujumla, ushirikiano wa mafundi wa China na Canada ni mzuri sana."

    Teknolojia za ujenzi wa Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha kipindi cha tatu cha Qinshan ziliingizwa kutoka Canada, lakini kwenye kipindi cha ujenzi, mafundi wa China waliposhirikiana na mafundi wa Canada walitumia ipasavyo akili na uhodari wao, walifanya uboreshaji wa kazi za kiteknolojia zaidi ya 90, na zaidi ya 20 miongoni mwao zilitumiwa kwa mara ya kwanza katika ujenzi wa vituo vya aina hiyo duniani. Mafanikio hayo yalikiwezesha ujenzi wa kituo hicho kufikia kiwango cha juu duniani katika uwezo wa kiteknolojia, uwezo wa usalama na malengo ya kiuchumi. Hivyo, mafanikio yaliyopatika katika ujenzi wa kituo hicho yalionesha nguvu za mafundi wa China na Canada.

    Naibu Mkuu wa Kampuni ya nishati ya atomiki ya Canada Bw. Kenneth Petrunik alisema:

    " Wakati ujenzi wa mradi huo umepamba moto kipindi cha pamba moto, mafundi wa Canada 100 tu walishiriki kazi hiyo, lakini mafundi wa China walifikia zaidi ya elfu 10. Hivyo, tunaweza kusema kuwa, kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo ni mafanikio kwa wachina, kwani juhudi za wachina zilichukua 99%."

    Waziri mkuu wa Canada Bw. Jean Chretien alisifu sana mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha kipindi cha tatu cha Qinshan. Kwenye mkutano wa kusherehekea kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo Bwana Chretien alisema:

    " Kufanikiwa kwa ujenzi wa mradi huo ni matokeo ya jitihada kubwa na ushirikiano mzuri wa wafanyakazi na mafundi wa China na Canada. Kwenye kipindi cha ujenzi, mafundi wa nchi hizo mbili walitatua matatizo pamoja na kubadilishana mawazo. Kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kumeweka msingi mzuri kwa ushirikiano wa katika matumizi ya kiamani ya nishati ya nyukilia kati ya China na Canada siku za usoni."

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Zeng Peiyan alisema :

    " China na Canada unaweza kusaidiana sana kiuchumi, na zina nguvu kubwa ya kufanya maingiliano kuhusu teknolojia za kiuchumi. Tuna matumaini ya kidhati kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili na kuwakaribisha wafanyabiashara wa Canada kuwekeza vitega uchumi nchini China."

Idhaa ya kiswahili 2004-04-14