Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-17 20:24:19    
Katibu mkuu wa chama tawala cha congres cha Sudan akizungumzia ushirikiano kati ya China na Sudan

cri
     Kutokana na mwaliko wa chama cha kikomunisti cha China, ujumbe wa chama tawala cha congres cha Sudan ulioongozwa na katibu mkuu wa chama hicho Dr. Omer, ulifanya ziara ya wiki moja nchini China kuanzia tarehe 23 mwezi Septemba, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa chama cha congres cha Sudan kutembelea China tangu uanzishwe uhusiano na chama cha kikomunisti cha China mwezi Agosti mwaka jana. Katika hoteli ya wageni waheshimiwa wa taifa ya Diaoyutai ya Beijing, waandishi wa habari wa China walimhoji Dr. Omer.

    Kwanza Dr. Omer aliwaambia waandishi wa habari kuwa, China inamwachia kumbukumbu nzuri sana, ujumbe aliouongoza naye ulikaribishwa kila sehemu ulipokwenda, hali ambayo iliwafanya wajumbe waone ukarimu na urafiki mkubwa wa wachina kwa wasudan. Dr. Omer alisema kuwa, alikuwa na mazungumzo ya kirafiki na viongozi kadhaa muhimu wa China akiwemo mwenyekiti wa halmashauri kuu ya baraza la mashauriano ya kisiasa ya taifa la China Bw. Jia Qinglin, ambapo alimjulisha maendeleo na mafanikio yaliyopatikana nchini China tangu utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Dr. Omer na wajumbe wengine walieleza kufurahishwa na maendeleo na ustawi wa China.

    Kama ilivyo kwa chama cha kikomunisti cha China, chama cha congres cha Sudan kinabeba jukumu la kuongoza wananchi wa nchi hiyo kujenga taifa na kuendeleza uchumi. Katika masuala mengi ya kimataifa, Sudan na China zina msimamo unaofanana. Kuhusu suala la Taiwan, serikali ya Sudan inaiunga mkono kithabiti serikali ya China, na China pia inashikilia haki na usawa katika mambo ya kimataifa. Hivyo nchi hizi mbili zinashirikiana sana katika jumuiya ya kimataifa. Dr. Omer alisema kuwa chama cha congres Cha Sudan kinasifu sana maendeleo ya uhusiano na chama cha kikomunisti cha China na uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Katika ziara hiyo, vyama hivyo viwili vilitia saini mkataba wa kukuza ushirikiano. Dr. Omer alieleza imani yake kwamba, mazungumzo hayo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya vyama hivyo viwili bila shaka yataanzisha mustakbali mzuri wa ushirikiano.

    Dr. Omer alisema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na jitihada za pamoja, urafiki kati ya Sudan na China na ushirikiano wa biashara umepata mafanikio makubwa, na una mustakabali mzuri. Sudan ni nchi kubwa yenye maliasili nyingi, ina mazao mbalimbali, na inajulikana kama ghala la nafaka la Afrika, na kwa upande wa bidhaa za mifugo inashika nafasi ya kwanza kati ya nchi za kiarabu na nafasi ya pili katika nchi za Afrika. Mbali na hayo, Sudan ina hzina kubwa ya maliasili ya madini na mafuta. Katika miaka ya hivi karibuni, mafuta na gesi nyingi viligunduliwa nchini Sudan, hali ambayo imeweka msingi mzuri wa maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo, pia inatoa fursa nzuri kwa Sudan na China kuzidisha ushirikiano wa nishati.

    Dr. Omer alisema kuwa, hivi sasa, ushirikiano katika sekta ya nishati kati ya China na Sudan unaendelea kwa kina, ambapo makampuni zaidi ya 10 za China yameanzisha shughuli nchini Sudan, shughuli za makampuni hayo zinahusu mafuta, ardhi na nyumba, ujenzi wa madaraja na barabara, na ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme. Ushirikiano katika sekta ya mafuta unawafurahisha zaidi watu. Katika makampuni zaidi ya 10 ya mafuta ya nchi za kigeni nchini Sudan, shughuli za kampuni ya mafuta na gasi ya China inaendelea vizuri zaidi.

    Jambo lingine linalomfurahisha Dr. Omer ni kwamba, baada ya mazungumzo magumu ya wiki tatu, serikali na jeshi la uasi la Sudan tarehe 24 mwezi Septemba nchini Kenya, zilifikia mkataba juu ya suala la usalama katika muda wa mpito wa miaka 6 ijayo. Wachambuzi wanaona kwamba, mkataba huo ni muhimu sana, na unamaanisha kuwa maendeleo ya amani ya Sudan yamepiga hatua kubwa. Maendeleo ya nchi na maisha bora ya watu hayawezi kupatikana bila utulivu na amani kupatikana kwanza. Aidha, utulivu na amani nchini Sudan bila shaka utaanzisha mazingira mazuri ya kuzidisha mawasiliano na ushirikiano kati ya China na nchi hiyo ya Afrika. Katika hotuba yake iliyotolewa tarehe 25 mwezi Septemba hapa Beijing, Dr. Omer alifafanua vizuri jambo hilo.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-07