Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-17 20:27:45    
Barabara ya China

cri
    Katika nchi nyingi za Afrika, watu husumbuka kutokana na barabara zilizoharibika kwa miaka mingi. Lakini barabara ya kiwango cha juu inayoitwa "Barabara ya China" inaonekana kama ni mpya baada ya kutumiwa kwa miaka 3, na inasifiwa sana na waafrika.

    Barabara hiyo ina urefu wa kilomita 150. Mwandishi wa habari alikutana na dereva mwafrika aitwaye David aliyekuwa akiendesha gari kwenye barabara hiyo mara kwa mara. David alisema kuwa, amewahi kuendesha gari kwenye barabara  mbalimbali nchini Kenya kwa miaka 10, lakini anahisi kuwa barabara zilizojengwa na China ni nzuri zaidi. Anaona kuwa, wachina wanawajengea waafrika barabara zinazowafurahisha.

    "Barabara ya China" ilijengwa na Kampuni ya barabara na madaraja ya China ( China Road and Bridge Corporation). Barabara hiyo ni sehemu moja ya barabara muhimu sana za kimataifa zilizopo Afrika Mashariki. Inaanzia kutoka pwani ya Bahari ya Hindi nchini Kenya, na kuunganisha sehemu za Tanzania, Uganda, Burudi, Rwanda, Sudan na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Barabara hiyo ni muhimu sana kwa mawasiliano kati ya Bahari ya Hindi na bara la Afrika.

    Kampuni ya barabara na madaraja ya China iliingia katika soko la dunia mwaka 1979, ambapo ilianzisha miradi zaidi ya 500 ya ujenzi barani Asia, Afrika na sehemu ya Mashariki ya kati. Thamani ya miradi hiyo ilizidi dola za kimarekani bilioni 3. Kampuni hiyo inashughulikia nyanja mbalimbali, zikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, usambazaji wa maji, ujenzi wa viwanda na wa makazi, reli, na viwanja vya ndege. Kampuni hiyo pia ilijenga madaraja matano huko Mosul nchini Iraq, sehemu ya kaskazini ya barabara la Kowloon huko Hongkong, na barabara ya taifa ya A109 ya Kenya. Kuanzia mwaka 1985, kampuni hiyo ilikuwa katika nafasi 225 za mwanzo duniani katika Rekodi ya habari ya Ujenzi wa miradi ya Marekani kwa miaka mingi mfululizo, na ilishika nafasi ya 88 katika rekodi hiyo mwaka 1998. Katika miaka ya hivi karibuni, kati ya kampuni 50 kubwa sana za China zinazoshughulikia ujenzi katika nchi za nje, mapato ya ujenzi wa kampuni hiyo ipo katika nafasi 5 za mwanzo. Hivi sasa, kampuni hiyo ina ofisi 20 nchi za nje, na kufanya kazi katika nchi na sehemu zaidi ya 30 duniani.

    Kampuni ya barabara na madaraja ya China iliingia katika soko la ujenzi la Afrika mwaka 1999, ni moja kati ya kampuni za China zilizoingia bara la Afrika mapema zaidi. Katika miaka 20 iliyopita, kampuni hiyo ilifanya usimamizi wa kisasa barani Afrika, na ilijitahidi kuinua uwezo wake, na ilivyokuwa na uhusiano mzuri na wafanyakazi wa Tanzania ilisifiwa sana na wenyeji wa huko. Kampuni hiyo ilishinda kampuni zaidi ya 20 za nchi za nje kutokana mafanikio iliyoyapata katika miaka mingi iliyopita, na ilipata fursa ya kujenga barabara hiyo inayoitwa "Barabara ya China."

    Katika hatua ya ujenzi wa barabara hiyo, kampuni hiyo ilitumia ufundi mbalimbali wa kisasa, na ilitumia miaka miwili na nusu kumaliza ujenzi huo tarehe 31, Agosti, mwaka 2000, kabla ya muda uliopangwa. Kutokana ujenzi huo, Kampuni ya barabara na mashamba ya China ilisaidia Kenya kuandaa mamia ya wahandisi na mafundi. Pia wafanyakazi wa China waliwaokoa watu mia kadhaa waliokumbwa na ajali bila ya kujali maisha yao yenyewe.

    Barabara hiyo ilisifiwa sana na serikali ya Kenya. Rais wa zamani wa Kenya Bw. Daniel Arap Moi alisema kuwa, endapo kampuni zote zitafanya vizuri kama kampuni hiyo ya China, Kenya itapata maendeleo makubwa zaidi. Mwakilishi wa kampuni iliyowekeza vitega uchumi katika ujengzi wa barabara hiyo pia alisifu kuwa, mradi huo ni mfano mzuri kwa uwekezaji wenye ufanisi barani Afrika. Meneja wa ofisi ya Kampuni kuu ya barabara na madaraja ya China huko Nairobi Bw. Wang Xiaoguan alisema kuwa, "Barabara ya China" inawaletea sifa nyingi, ambapo wanaona fahari kubwa sana. Barabara hiyo ina umuhimu mkubwa wa kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika.

    Ni kweli, miundo mbinu mibovu ni tatizo kubwa linalowakabili waafrika, pia ni kikwazo kwa maendeleo ya uchumi barani Afrika. Hivyo, hivi sasa, suala linalofuatiliwa na waafrika ni kujitahidi kutafuta njia mpya ya kuendeleza uchumi.

    Mfanyabiashara wa Afrika aitwaye John Muge alimwambia mwandishi wa habari kuwa, hivi sasa, nchi nyingi za Afrika zimeanza kuelewa kuwa ujenzi wa barabara wa Asia unafuata mazingira halisi. Huo ni mwelekeo muhimu sana. Garama za ujenzi kwa kampuni za Ulaya ni kubwa sana, na zinaweka masharti mengi, na haziwezi kulingana na mahitaji ya Afrika. Hivi sasa, "Barabara ya China" inaota mizizi mioyo ni mwa waafrika. Mkenya mmoja alimwambia mwandishi wa habari kuwa, wachina waliwasili Afrika kwa kupanda meli miaka mia kadhaa iliyopita. Sasa, tunataka kusema, "Karibuni" wachina wanaokuja Afrika kwa vyombo vya kisasa vya usafiri.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-07