Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-17 20:31:49    
Mashamba yanayowekezwa na wachina nchini Zambia

cri
    Katika ardhi ya Zambia ya kilomita laki 7 elfu 50 za mraba, yapo mashamba mbalimbali yaliyowekezwa na wachina. Kama tujuavyo, kilimo ni kazi inayotakiwa gharama kubwa, na kupata ufanisi polepole, lakini wachina waliowekezwa vitega uchumi kwenye sekta ya kilimo nchini Zambia wanafanya kazi kwa bidii kubwa na kupata ufanisi mzuri kwenye mashamba yao.

    Katika mashamba mengi yaliyowekezwa na wachina nchini Zambia, shamba la Wangchi linaendeshwa vizuri zaidi, mayai yanayozalishwa kwenye shamba hilo yanachukua nusu ya yalekwenye soko la Lusaka mji mkuu wa nchi hiyo.

    Shamba la Wangchi lililoko milimani kilomita 50 kutoka kaskazini-mashairki ya Lusaka, pia linajulikana kama shamba la ampuni ya kilimo ya China, shamba hilo lina eneo la hekta elfu 3, lilinunuliwa na kampuni ya kilimo ya China mwaka 1993 kwa kuwekezwa fedha za dola za kimarekani laki 2 na elfu 20. Zamani sehemu hiyo ilikuwa milima mitupu, hakuna umeme na maji, baada ya kufanya juhudi kubwa, mashamba ya kulimwa na visima vimechimbwa, na waya za umeme zimewekwa.

    Hivi sasa shamba la Wangchi hasa linashughulikia mifugo, lina ng'ombe zaidi ya 900, nguruwe zaidi ya 700, na kuku zaidi ya laki 1 elfu 30. Kila siku linuza mayai zaidi ya elfu 48 namaziwa litre 1200. Zaidi ya hayo, kaika shamba hilo pia imepandwa mahindi ili kupunguza gharama ya chakula cha mifugo.

    Shamba la Wangchi pia limetoa nafasi za ajira kwa wazambia.Hivi sasa shamba hilo limewaajiri wafanyakazi wenyeji zaidi ya 200, wakiwemo wafanyakazi rasmi 90 na wengine zaidi ya 110 wa kibarua. Wafanyakazi rasmi wanapewa mshahara mzuri na huduma mbalimbali ikiwemo bima ya uzee, mbali na hayo kila mfanyakazi anapangishwa bweni ya bure, na kila mwaka ana likizo ya mwezi mmoja.

    Shamba la Urafiki wa China na Zambia liko kilomita 20 toka magharibi ya Lusaka. Mwezi Februali mwaka 2003, mwenyekiti wa halmashauri kuu ya baraza la mashauriano ya kisiasa ya China bwana Li Ruihuan alipofanya ziara nchini Zambia, alitembelea shamba hilo, ambo alieleza kuwa shamba la urafiki wa China na Zambia linapaswa kufanya kazi za kutoa vielelezo, ili kuhimiza zaidi uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Zambia.

    Shamba la Urafiki wa China na Zambia lenye eneo la hekta 667, lilianzishwa mwezi Novemba mwaka 1990 na Kampuni ya Kilimo ya China pamoja na Kampuni ya Kilimo ya Jiangsu China kwa kuwekeza fedha za dola za kimarekani zaidi ya laki 3 elfu 17, Shughuli zake kubwa ni kupanda mahindi na maharagwe, pia linafuga ng'ombe na nguruwe.

    Mkuu wa shamba hilo bwana Dong Fafu alifahamisha kuwa, shamba hilo sasa lina wafanyakazi 8 kutoka China, wafanyakazi wengine 165 wa aina mbalimbali wote ni wenyeji wa Zambia. Bwana Dong alisema kuwa shamba hilo siku zote linafuata sheria za Zambia, linawatolea wakati wafanyakazi wake mishahara, vitu vya huduma, fedha za kustaafu, ada ya bima na nyinginezo, zaidi ya hayo pia linawatolea mabweni, maji na umeme.

    Bwana Dong alisema kuwa, kutokana na juhudi za pamoja za wachian na wazambia, Shamba la Urafiki wa China na Zambia limepata ufanisi mzuri. Wizara ya kilimo, na idara kuu ya takwimu ya Zambia kila mwaka zinafanya uchunguzi juu ya hali mbalimbali za shamba hilo, na kutaka wengine wajifunze uzoefu wa shamba hilo.

    Mwaka 2002 shamba hilo lilipata faida za dola za kimarekani laki 4, mwaka 2003, mazao ya mahindi yalikuwa mazuri sana, na mazo ya ngano yalifanya juhudi kubwa kwa wawezavyo kuendesha vizuri Shamba la Urafiki wa China na Zambia, ili kuongeza mali kwa ajili ya Zambia na kutia nuru kwa China.

    Ikilinganishwa na makampuni, ni vigumu kwa watu binafsi kuendesha vizuri mshamba katika nchi za nje. Bwana Hu aliwahi kuwa mpishi wa hospitali moja kwa mkoa wa Henan, China, alikwenda Zambia mara mbili kwa kufuata kikundi cha madaktari wa China. Mwaka 1997 bwana Hu alinunua shamba moja kwa fedha alizozikopa kutoka nchini China. Baada ya kufanya juhudi kubwa, miaka mitaatu iliyopita alinunua shamba lingine jipya. Sasa mashamba yake yanafuga nguruwe zaidi ya 200, na kuku zaidi ya elfu 15 Mbali na hayo, bwana Hu pia alipanda mboga nyingi. Licha ya mashamba, Bwana Hu ana viwanda vya kutengeneza mabao na mahindi, na mabao mengi yaayotengenezwa na kiwanda chake yanauzia Afrika ya Kusini. Li Guo ni mfanyabiashara wenye shamba kubwa zaidi ya uyoya nchini Zambia. Alihitimu kutoka chuo kikuu cha tiba cha China, na alikwenda Zambia mwaka 2000 kuanzisha shamba lake la uyoya.

    Li Guo alisema kuwa, hivi sasa Zambia inaagiza uyoya kilogramu elfu 1 hadi elfu 2 kutoka Afrika a Kusini kila wiki, hivyo, mustakabali wa biashara ya uyoya nchini Zambia utakuwa mzuri sana. Alieleza kuwa, lengo lake ni kupanua ukubwa wa kazi yake, na kuanzisha shughuli za nchi za nje. Anaamini kuwa, ipo siku atafaikiwa kutimiza lengo lake baada ya kufanya juhudu kubwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-04-07