Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-19 20:42:26    
Ugonjwa wa Kifua Kikuu

cri
    Ugonjwa wa kifua kikuu pia unajulikana kama ni "Mradhi meupe ya kuambukiza". Katika karne ya 19, watu wengi walifiwa na jamaa au marafiki kutokana na maradhi hayo makali ya kuambukiza. Ingawa idadi ya wagonjwa wakifua kikuu ilipungua kwa haraka duniani kutokana na kupatikana madawa ya aina mbalimbali ya kutibu uvimbe na ya kujikinga katika karne ya 20, lakini watu watakosea endapo wanadhani kwamba sasa hawana haja ya kujihadhari tena. Shirika la afya ulimwenguni, WHO lilionya kwamba kuna uwezekano wa kuzagaa tena kwa ugonjwa wa kifua kikuu katika miaka ya karibuni, hivyo binadamu hawana budi kukaa chonjo.

    Ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa wa muda mrefu unaopunguza nguvu ya mwili kutokana na kuambukiwa na vijidudu wa ugonjwa huo. Baada ya kuambukizwa ugonjwa wa aina hiyo, mgonjwa hukohoa, pamoja kuwa na kikohozi hata chenye damu, kuumwa kufua, kuwa na homa, kusikia uchovu mwilini na kukosa hamu ya chakula. Zaidi ya 90% ya wagonjwa wa kifua kikuu waliambukizwa kutokana na hewa, watu wazima wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kutokana na vijidudu vya wagonjwa wa kifua kikuu wakati wanpokohoa, kupiga chafya au mate yao.

    Kufanikiwa kwa utengenezaji wa madawa ya kutibu uvimbe na chanjo ya kifua kikuu pamoja na kutumika kwa tiba ya dawa ya maji ya kuua vijidudu ni mnara wa ushindi wa historia ya binadamu kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu. Kutokana na hayo, Marekani katika mwanzzoni mwa miaka ya 80 ya karne ya 20, ilisema kuwa binadamu wanaweza kutokomeza kabisa ugonjwa wa kifua kikuu mwishoni mwa karne ya 20. lakini, katika miaka ya karibuni, ugonjwa wa kifua kukuu uliibuka tena katika sehemu mbalimbali duniani. Takwimu iliyotolewa katika "Siku ya kupambana na kifua kikuu duniani" inasema kuwa hivi sasa bado kuna watu 5000 wanaokufa kila siku kutokana na ugonjwa wa kuifua kikuu, na idadi ya watu wanaoambukizwa ana ugonjwa huo ni zaidi ya milioni 8 kila mwaka.

    Sababu yake kubwa ni kwamba katika miaka 20 iliyopita, sehemu nyingi duniani hazikuzingatia ugonjwa wa kifua kikuu katika uwekaji sera, hatua ambayo ilidhoofisha hata kuharibu kabisa mfumo kuzuia ugonjwa huo. Idadi ya wagonjwa wa ukimwi walioambukizwa na ugonjwa wa kifua kikuu ni mara 30 kuliko ile ya watu wa kawaida, wagonjwa wa ukimwi wengi zaidi walifariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu. Pamoja na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi duniani, idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu pia inaongezeka kwa haraka. Kujitokeza kwa vijidudu vya kifua kikuu ambayvo ni sugu kwa madawa, kumeongeza matatizo ya kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu.

    Kutokana na hayo, WHO imetangaza hali ya dharura ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani, na iliweka mpango wa vitengo mwaka 1997 unaojulikana kwa "Tiba ya muda mfupi ya kuchunguzwa moja kwa moja" ukiwa na lengo la kuponya 95% ya wagonjwa wa kifua kikuu. Kitu kilicho muhimu zaidi katika mpango huo nikwamba wagonjwa wanakunywa dawa kwa kuchunguzwa moja kwa moja na wahudumu wa afya, matibabu yasije yakacheleweshwa na kusababisha kuzagaa katika maeneo makubwa kwa ugonjwa wa kifua kikuu.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-19