Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-20 22:06:53    
Serikali ya China kutilia maanani kinga na tiba ya ukimwi

cri
    Naibu waziri mkuu wa China Bibi Wu Yi amesema hivi karibuni kuwa, China inapaswa kuwahamasisha zaidi watu katika jamii nzima na kushirikisha nguvu zote katika kusukuma mbele bila kupoteza fursa kazi ya kinga na tiba ya ukimwi, na kudhibiti kwa hatua madhubuti maambukizi ya haraka ya ugonjwa wa ukimwi.

    Bibi Wu Yi amesema kwenye mkutano wa taifa wa kinga na tiba ya ukimwi uliofanyika hapa Beijing kuwa, serikali ya China inatilia maanani sana kinga na tiba ya ukimwi, na imepata mafanikio katika kazi hiyo. Hivi sasa maambukizi ya ukimwi yanaelekea kwa watu wa kawaida kutoka watu wenye tabia mbaya ambao ni rahisi kuambukizwa virusi vya ukimwi, na ni lazima kudhibiti kazi ya kipindi hiki, kuchukua hatua imara kwa kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

    Bibi Wu amesisitiza kuongeza elimu ya kukinga ukimwi, kupiga vita uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine, kugundua kwa kadiri iwezekanavyo watu walioambukizwa virusi vya ukimwi na kutoa ripoti kwa wakati.

    Naibu waziri wa afya wa China Bwana Wang Longde hivi karibuni alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa, katika kazi za kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi za siku zijazo, China itaanzisha kampeni ya kutoa elimu nchini kote kuhusu ugonjwa wa ukimwi na kuchukua hatua za kinga na udhibiti wa ukimwi.

    Bwana Wang amesema, hivi sasa maambukizi ya ukimwi yanaelekea kwa watu wa kawaida kutoka watu wenye hatari ya kuambikizwa virusi vya ukimwi nchini China, kutokana na njia ya maambukizi ya ukimwi nchini China, China itashikilia kazi kuu ya kinga ya ukimwi, na kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi ya ukimwi.

    Bwana Wang ameeleza kuwa, China itaimarisha kazi ya kubuni sheria kuhusu kinga na tiba ya ukimwi, kufanya utafiti kuhusu utaratibu wa bima husika, na kuwapatia msaada wa lazima watu wanaoshughulikia kinga na tiba ya ukimwi wakati watakapoambukizwa kwa ghafla virusi vya ukimwi. Pia amesema kuwa China itaimarisha matibabu ya ugonjwa wa ukimwi.

    Bwana Wang amefahamisha kuwa, serikali kuu ya China itatenga fedha ili kununua madawa ya kupambana na virusi vya ukimwi na madawa ya upimaji, pia itatoa misaada kwa sehemu zenye matatizo ya kiuchumi, na kuwapatia matibabu bure wakulima na wagonjwa wa ukimwi wa mijini wenye matatizo ya kiuchumi.

    Naibu waziri wa afya wa China Bwana Gao Qiang hivi karibuni alisema kuwa, wizara ya afya ya China itazidi kukamilisha mfumo wake wa kutoa ripoti kuhusu milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, na kazi ya kutoa taarifa kuhusu milipuko hiyo inatekelezwa kwa sheria.

    Bwana Gao Qiang amesema kuwa, ofisi na watu maalumu lazima wawekwe katika idara za huduma za afya kushughulikia kazi ya kutoa ripoti na ukaguzi wa hali ilivyo ya maambukizi ya magonjwa . Na idara na mtu yeyote aliyeacha, kuficha na kupuuza kazi ya kutoa ripoti kuhusu mlipuko wa ugonjwa atashughulikiwa.

    Ili kukabiliana na hali ngumu ya hivi sasa katika mapambano dhidi ya ukimwi nchini China, hivi karibuni, serikali ya China imeanza kutekeleza sera mpya za kuwasaidia wagonjwa wa ukimwi na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

    Sera hizo ni pamoja na kuwatibu bila malipo wagonjwa ambao ni wakulima au wakazi wa mijini wenye shida za kiuchumi; katika maeneo yanayoathiriwa vibaya na maambukizi ya ukimwi, watu kwa hiari wanapata ushauri na kupimwa damu bila malipo; na watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kutokana na ukimwi wanapewa elimu bure.

    Hivi sasa idadi ya watu wenye ukimwi imefikia laki 8.4 katika China bara, na maambukizi ya ugonjwa huo yapo katika kipindi muhimu ambapo ukimwi umeanza kuenea miongoni mwa watu wa kawaida kutoka kwa watu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa. Serikali ya China inahamasisha nguvu za jamii nzima na kuchukua hatua zenye ufanisi ili kuzuia uenezi na maambuziki ya ukimwi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-04-20