Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-22 21:31:37    
Misaada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka familia maskini nchini China

cri
    Nchini China, watoto wakimaliza masomo ya sekondari wanashiriki kwenye mtihani kabla ya kuingia vyuo vikuu. Ni wale wanaofaulu mtihani ndio wanaoweza kuendelea na masomo ya vyuo vikuu, na upo ushindani mkali sana. Kupokea hati ya kuandikisha ya vyuo vikuu ni jambo ya kufurahia watu, isipokuwa Bibi Lin Xue, msichana kutoka faimilia ya wakulima mjini Dalian, kaskazini mashariki ya China, ambaye alikuwa analialia kwa siku kadhaa.

    Msichana huyo alipata taarifa kutoka chuo kikuu cha udaktari cha China ikimwarifu kuwa, amefaulu mtihani na angejiandikisha kwenye chuo kikuu hicho. Lakini Bibi Lin aliamua kuficha taarifa hiyo bila kuwaambia wazazi wake, akaacha nafasi hiyo ya kubadilisha hatma yake.

    Jambo hilo lilitokea mwaka 2000. Bibi Lin alikumbusha, akisema, alifahamu wazi kwamba, familia yake yenye mizigo mikubwa ya madeni haina uwezo wa kumudu ada yake kwenye chuo kikuu. Baba yake alikuwa ameumwa kwa miaka mingi, kabla ya kushiriki kwake kwenye mtihani, mama yake aligunduliwa kuwa na cancer, na kaka yake mdogo bado anasoma shuleni.

    Akishakata nia, msichana huyo alikwenda kutafuta kazi za vibarua. Alikiri kwamba, wakati ule alikuwa amepoteza matumaini yote.

    Lakini Bibi Lin Xue ni mwenye bahati nzuri. Habari kuhusu yeye kuacha nafasi ya kusoma kwenye vyuo vikuu ikapatikana na madaktari wa Chuo kikuu cha udaktari wa Kichina cha Jinzhou mjini Danlian, ambao walimchangia Renminbi Yuan elfu 6, sawa na dola za kimarekani 750. kwa hivyo, baada ya kuacha masomo ya zaidi ya mwaka mmoja, Lin Xue alirudi kwenye shule, na kufaulu mtihani na kuandikishwa kwa mara nyingine tena na chuo kikuu cha udaktari wa China mwaka jana.

    Chuo kikuu hicho kiliamua kuwa, Lin Xue anaweza kuahirisha kulipa ada mpaka atakapokuwa na uwezo. Mbali na hayo, anasaidiwa Yuan za Renminbi elfu 2 kila mwaka kutoka kwa mradi uitwao "ukuta mkuu mpya" ambao umeandaliwa na Shirikisho la mfuko wa uondokanaji umaskini la China, ukilenga kuwatolea misaada wanafunzi wa vyuo vikuu wenye shinda kubwa ya kiuchumi.

    Tokea katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, China ilianza mageuzi makubwa ya elimu ya juu. Ada za vyuo vikuu zilipanda juu kutoka mamia ya Yuan za Renminbi kwa mwaka mpaka elfu 3 hadi 5, hata kufikia elfu 7 na 8 kila mwaka. Mbali na ada hizo, wanafunzi wanakabiliwa na gharama za makazi na matumizi ya maisha.

    Katika China, wastani wa mapato ya familia maskini ni Yuan 200 za Renminbi kwa mwezi. Hivyo familia hizo hazina uwezo wa kumudu ada kubwa za elimu ya juu. Kwa mujibu wa takwimu za shirikisho la mfuko wa uondokanaji umaskini la China, miongoni mwa wanafunzi wapatao milioni 16 wanaosoma sekondari nchini kote, kila mmoja kati ya watano anatoka familia maskini. Je, kama watoto hao wanastahili kufungwa nje ya milango ya vyuo vikuu kutokana na familia zao kushindwa kumudu ada za elimu ya juu? Suala hilo limejadiliwa sana kwenye jamii.

    Sambamba na mageuzi ya elimu ya juu, wizara ya elimu ya China iliagiza vyuo vikuu kuwafuatilia wanafunzi kutoka familia maskini na kuwatolea misaada. Mwaka jana, wizara ya elimu iliandaa msaada wa masomo wa kitaifa, ambao kila mwaka husaidia wanafunzi maskini hodari wa vyuo vikuu wapatao elfu 45, jumla ya Yuan za Renminbi milioni 2, kiasi ambacho ni sawa na dola za kimarekani laki 2 na elfu 50. Aidha, wanafunzi wanaoshinda msaada huo pia wanasamehewa ada za mwaka mmoja. Mbali na hayo, wizara ya elimu iliagiza vyuo vikuu mbalimbali kuhakikisha watoto maskini waliofaulu mtihani wa kuingia vyuo vikuu wasiache masomo kutokana na kushindwa kulipa ada.

    Bw. Tang Jun ni mtafiti wa sera za kijamii kwenye taasisi ya sayansi za kijamii ya China, anaeleza maoni yake kwamba, hatuwezi kusimamia na kuendesha vyuo vikuu kama tunavyoendesha biashara viwandani, hii ni kitu muhimu sana. Msomi huyo anakubali kuwa, vyuo vikuu kudai ada kubwa ni ya haki kwa kulingana na uchumi wa soko huria, lakini anasisitiza kuwa, ni lazima zipo njia za kuwasaidia wanafunzi maskini.

    Mwandishi He Jianming anajulikana kwa vitabu vyake vya kufuatilia wanyonge, anasema kuwa, suala la wanafunzi maskini wa vyuo vikuu linazingatiwa zaidi na serikali na jamii. Mwandishi huyo aliwahi kutembelea vyuo vikuu zaidi ya 40 nchini kote akichunguza suala la wanafunzi maskini. Anaeleza furaha yake kwamba, hivi sasa umejengwa mfumo wa kuwasaidia wanafunzi hao, ambao ni pamoja na utoaji mikopo ya mabenki, michango ya jamii, nafasi za vibarua kwa wanafunzi hao na misaada ya masomo. Anasema, hatua hizo si kama tu zimewaletea matumaini wanafunzi maskini, bali pia jamii yetu.

    Bwana mmoja ambaye hataki jina lake kutajwa pamoja na marafiki zake, walichangia Renminbi Yuan elfu 2, sawa na dola za kimarekani 250 kwa mradi wa "ukuta mkuu mpya" unaosaidia wanafunzi maskini. Anasema kuwa, fedha hizo si kitu kwetu, lakini ni msaada mkubwa kwa wanafunzi maskini. Iwapo naweza kuwasaidia kwenye njia yao ya kuelekea mafanikio, nafurahi sana. Sisi tumepata fedha tukinufaishwa na sera za mageuzi na maendeleo, ni wajibu wetu kuwatunza wenzetu wasio na bahati nzuri kama sisi.

    Naibu mkuu wa shirikisho la mfuko wa uondokanaji umaskini la China Bw. He Daofeng anasema kuwa, wanafunzi wa vyuo vikuu ni uti wa mgongo wa ujenzi na maendeleo ya taifa, wanastahili kutunzwa na kusaidiwa na jamii.

    Katibu mkuu wa shirikisho la taaluma ya ukuta mkuu la China Bw. Dong Yaohui alieleza maoni yake, kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka familia maskini si wanyonge. Kuwasaidia ni kuwatia moyo watu wanaopata mafanikio. Tunawatolea misaada si kutokana na huruma, bali ni heshima kwa ushujaa na mafanikio yao.

Idhaa ya Kiswahili 2004-04-22