Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-26 16:20:44    
Utafiti wa binadamu kuhusu mwezi

cri
Chombo cha kwanza cha uchunguzi wa mwezi cha Ulaya kilirushwa angani tarehe 27 mwezi Septemba mwaka uliopita, hatua ambayo imedhihirisha kuwa utafiti wa mwezi umeamsha shauku kubwa ya mataifa makubwa yaliyoendelea katika usafiri wa anga ya juu.

    Binadamu walianza na shughuli za uchunguzi na utafiti wa kisayansi juu ya mwezi toka miaka ya 50 ya karne ya 20, Urusi ya zamani ilifaulu kurusha setlaiti ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu kwenye anga ya juu mwaka 1957, na binadamu walianza kuingia anga ya juu na kufanya utafiti juu ya mwezi baada ya Urusi kumpeleka mwanaanga wake Bw. Yuli Gagalin kwenye mihimili karibu na dunia.

    Marekani na Urusi ya zamani zilikuwa na ushindani wa sayansi na teknolojia za anga ya juu kwa kufuatilia utafiti wa mwezi. Kufanikiwa kwa usafiri wa chombo cha anga ya juu kilichojulikana kwa Apollo nchini Marekani mwaka 1969, kulitimiza matumaini ya binadamu ya kupanda kwenye mwezi. Katika mwaka ule kulikuwa na wanaanga 12 ambao walipelekwa kwenye mwezi na kuleta ardhini mawe ya huko yenye uzito wa kilo 440.

    Mwaka 1972, baada ya Marekani kufanikisha "mpango wa Apollo", utafiti kuhusu mwezi ulipungua kwa muda fulani kutokana na gharama kubwa ya shughuli za utafiti wa mwezi. Lakini binadamu walishindwa kujizuia kwa kishawishi cha mazingira asilia na rasilimali pekee za mwezi, isitoshe, maendeleo ya teknolojia ya usafiri kwenye anga ya juu yalileta uwezekano kwa binadmau wa kufanya utafiti kwa undani zaidi juu ya mwezi, hivyo katika mwisho wa miaka ya 90 ya karne ya 20, binadamu walitupia macho tena kwa mwezi.

Mwaka 1986, Marekani ilitoa wazo la kurudi tena kwenye mwezi na kujenga vituo huko, baadaye ilirusha vyombo viwili vya uchunguzi katika mwaka 1994 na mwaka 1998.

    Wakati huo huo, Russia nayo ilibuni mpango wa utafiti wa mwezi wa vipindi vitatu ambavyo viwili vya mwanzo ni kuchora ramani ya mwezi, kuchukua mawe ya mwezi na kuyaleta duniani kupimwa, ili kujua mahali na kiasi chake madini za huko. Na katika kipindi cha tatu ni kujenga kituo mwezini mnamo mwaka 2010.

Aidha, Ulaya, Japan, India na China zilitoa mipango ya utafiti wa mwezi. Kutokana na mpango uliowekwa, chombo cha kwanza cha uchunguzi wa mwezi kilichorushwa hivi karibuni na Ulaya kijulikanacho kwa "Smatr-No. 1" kitaanza kutekeleza jukumu lake la kufanya uchunguzi kwa mwezi baada ya miezi 15. Japan itarusha angani chombo cha uchunguzi wa mwezi mwaka ujao ambacho kitaweka chombo cha kupimia mtetemeko wa ardhi kwenye mwezi ili kujua muundo wake pindi unapotokea mtetemeko wa ardhi, wakati chombo cha kijulikanacho kwa "Jini la mwezi" chenye kamera inayoweza kupiga picha safi na kuzunguka mwezi, kinatarajiwa kurushwa angani katika mwaka 2005.

    Idara ya utafiti wa anga ya juu ya India imetangaza kuwa itarusha setilaiti yake ndogo mwaka 2005 na kurusha angani chombo chake cha kwanza cha usafiri wa anga ya juu chenye binadamu ndani yake mwaka 2008. Idara ya usafiri wa anga ya juu ya China imeeleza kuwa mpango wa urushaji wa chombo cha uchunguzi wa mwezi unatekelezwa bila matatizo.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-26