Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-27 16:45:53    
Mavuno mazuri ya peach

cri
    Wasikilizaji wapendwa, kifuatacho ni kipindi cha nchi yetu mbioni. Mipichi iliyopandwa kwenye maeneo makubwa ya wilayani Pinggu, kiunga cha Beijing imechanua maua.

    Kwenye kando ya barabara moja yenye mipichi mingi, mwandishi wetu wa habari alikutana na mkulima Wang Zeshun na kuwa na mazungumzo naye. Mkulima huyo alisema kuwa alitumia wadudu wa tutu kula wadudu waharibifu wa mipichi, na alipata mavuno mazuri bila kutumia madawa ya kuua wadudu waharibifu. Alisema, "Mimi ninatumia wadudu wa tutu kula wadudu waharibifu wote waliko katika mipeach yangu, hivyo sikuwa na haja ya kutumia madawa. Mapichi niliyovuna mwaka huu ni mazuri na matamu ambayo yalipendwa sana na wanunuzi."

    Mkulima Wang Zeshun amepanda mipichi zaidi ya mia tano. Alisema kuwa hapo zamani familia yake ilililma zao la ngano peke yake, lakini hakupata mavuno mazuri kutokana na kwamba ardhi ya huko haina rutuba, hata alijitahidi sana, lakini pato lake lilikuwa chini ya Yuan za Renminbi elfu kumi kwa mwaka, sawa na dola za kimarekani 1220. Siku moja, mtaalamu alikwenda shambani kuwaambia kuwa ardhi ya huko inafaa kwa kupanda mipichi. Kutokana na mapendekezo ya mtaalamu, alipanda mipichi ambayo ilizaa mapichi katika mwaka uliofuata ambayo yalimletea pato la zaidi ya Yuan elfu 70, baada ya

    kuondoa gharama ya Yuan elfu 20, faida ilikuwa Yuan zaidi ya elfu 50, alishauriana na mkewe kuwa wataendelea kushughulikia zao la mapichi.

    Mke wa Wang Zeshun anaitwa Wei Jinfeng, ambaye alizaliwa katika sehemu ya kaskazini mwa China, licha ya kwamba anazungumza na watu kwa haraka, anafanya kazi chapuchapu pia. Alisema kuwa sasa anafurahi sana kushughulikia miti ya matunda. Wakati anapoangalia maua ya mipichi iliyochanua maua, na kuona matunda kuwa makubwa siku hata siku, alifurahi mno, alisema kuwa kushughulikia mipichi kumewalatea pato kubwa, na kuleta uwezekano kwao kupanga shughuli zao binafsi. Alisema, "Sitaki kufanya kibarua kwa watu wengine. Kwani kufanya kibarua, sina budi kufuata saa niliyopangwa, tena pato siyo kubwa. Baada ya kuuza mapichi yetu, ninaweza kushughulikia biashara ya kuuza mboga. Mwaka huu kwa uchache kabisa tutapata Yuan za Renminbi elfu 80 hadi 90"

    Alisema kuwa baada ya kushughulikia uzalishaji wa matunda ya mapichi, maisha ya familia yake yalikuwa mazuri mwaka hata mwaka. Sasa wameshanunua nyumba, na amekuwa na uwezo wa kuwasomesha watoto wawili katika shule ya sekondari.

    Mkewe Wang alielekezea kwa kidole banda kubwa lililofunikwa kwa nguo ya plastiki akisema kuwa baada ya kuwa na pato kubwa, familia yake ilijenga banda kubwa ili kuzalisha mapichi katika majira mengine, hatua ambayo inawaletea pato kubwa zaidi, hivi sasa mapichi iliyozaa mipichi yao ndani ya banda, yamekomaa.

    Katika banda hilo kubwa, mwandishi wetu wa habari alikutana na vijana kadhaa waliofika huko kutoka Beijing ili wachume mapichi wao wenyewe kutoka katika mipichi. Mgeni mmoja aitwaye Zhang Chunhai alisema kuwa walifanya matembezi huko katika majira ya Spring kwa lengo la kuchuma mapichi ili jamaa zao wapate kuyaonja. Bw. Zhang alisema, "Leo tunafurahi sana, zamani tulinuanua mapichi sokoni na hatukuwahi kuchuma mapichi sisi wenyewe kutoka katika mipichi, kwa hiyo tumefurahi kwelikweli. Hali ya namna hiyo ni vigumu kupatikana kwetu mjini, tena hewa ya kiungani ni safi zaidi kuliko mjini."

    Kila mwaka familia ya Wang Zeshun inapokea wageni wengi waliotoka mjini kuchuma mapichi katika majira hayo, ambayo mapichi yanaweza kuuzwa kwa bei nzuri sana, kuuza kilo moja ya mapichi wanaweza kupata Yuan za Renminbi 60, tena wanunuzi walikuwa wengi. Wakati mwingine hata katika usiku ambao watu wa familia yake wamelala, walikuja watu kugonga hodi kwa kutaka kuchuma mapichi. Hivi sasa kila ifikapo wiki endi au siku kuu, wakazi wa mjini wanapenda kwenda sehemu za viungani wakitaka kujiburudisha kwa mazingira ya asili, kuangalia maua na kuchuma mapichi.

    Hewa safu ya sehemu ya nje ya mji, maua na matunda yaliyoko katika mipichi yanawafurahisha wakazi wa mjini; fedha za wakazi wa mjini zimetunisha pochi za wakazi wa vijijini, kweli hayo ni mambo yanayowanufaisha watu wa mjini na vijijini. Mwandishi wetu wa habari aliambiwa kuwa nusu ya mapichi ya mkulima Wang Zeshun huchumwana wageni kutoka mjini; katika mwaka uliopita, fedha waliyopata wakulima wa matunda kutokana na matunda yaliyochumwa na wageni zilikuwa 15% ya jumla ya pato lao.

    Kijiji alichoko Wang Zeshun kinajulikana kwa kijiji cha Yuzisha, kijiji hicho kina koo zaidi ya 60, ambazo zote zimepanda mipichi baada ya kuona ufanisi wa upandaji wa mitunda, na mapato yao yamekuwa makubwa mara kadha kuliko yale ya hapo awali. Jirani ya Wang Zeshun Bw. Wang Xihe alisema kuwa baada ya kupanda mipichi 200, maisha ya familia yake yamekuwa tofauti kabisa na ya zamani.

    Wang Zeshun alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa licha ya kuendeleza mambo ya utalii kwa kutumia upandaji wa miti ya matunda, wakazi wengine wa kijiji hicho wameanza kupanda mipichi midogo iliyopandwa katika vyungu vidogo ambayo inapendwa na watu wengi na inauzwa sehemu ya mbali ikiwemo Hongkong. Makada wa kijiji hicho walisema kuwa pato lao kutokana na mauzo ya mapichi lilifikia dola za kimarekani laki kadhaa katika mwaka uliopita.

Idhaa ya Kiswahili 2004-04-27