Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-28 17:16:53    
Wazazi wa China wazingatia kuwaelimisha watoto wao

cri
Miaka ya 70 ya karne iliyopita, China ilianza kutekeleza sera ya mpango wa uzazi wa majira. Sera hiyo iliichangia jitihada ya China ya kupunguza idadi ya watu. Hivi sasa hapa nchini hasa katika miji mikubwa, familia nyingi zina mtoto mmoja tu. Hivyo wazazi wa China wanazingatia sana kumwelimisha watoto wao hata kabla yao kuzaliwa, bila kujali kutumia nyakati nyingi na gharama kubwa. Wazazi wa China wanataka watoto wao kuwa watu wenye elimu na uwezo mkubwa watakapokuwa watu wazima.

    Hivi sasa wanawake wajawazito nchini China, wanapenda kuwaelimisha watoto wao hata kabla yao kuzaliwa, huwa wananunua vitatu vya kuwapa watoto elimu, CD za muziki na kaseti za hadithi kwa watoto wao.

    Wachina wanazingatia elimu kwa watoto tangu zamani. Miaka mingi iliyopita, wachina walisema kuwa, uwezo na akili ya mtu mmoja iliweza kujulikana tangu alipokuwa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu. Hivyo, mama wajawazito waliwaburudisha kwa muziki, kuwasomea hadithi na kuzungumza na watoto ambao bado wakiwa ndani ya matumbo yao. Mbali na hayo, wakati mama anapokuwa na mtoto anapaswa kuangalia vitendo vyake. Kwa mfano anapaswa mwangalifu kwa vitendo vyake, kwa mfano anapaswa kutazama vitu vizuri au mandhari nzuri ya kuvutia na kuwa mchangamfu daima. Mara mtoto azaliwapo, wazazi wake huwa wanawanunulia vitabu, kaseti, CD na vitu vingine vinavyohusu elimu ya Kichina, Kingereza, muziki n.k. Baadhi ya watoto wanapelekwa na wazazi wao katika shule ya kukuza uwezo uliojificha wa watoto wao ili kuongeza uwezo wao katika maeneo mbalimbali.

    Watoto walipokuwa wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitatu, huwa wanapelekwa katika shule ya vichekechea kujifunza elimu mbalimbali zikiwa ni pamoja na muziki, upigaji picha, Kingereza, uchezaji wa ngoma na wushu.

    Watoto wanapokuwa na umri wa miaka 6 husomeshwa katika shule za msingi na kuanza kipindi cha miaka 12 cha kupewa elimu ya lazima. Katika kipindi hiki, wazazi wachina pia wanaingia katika kipindi muhimu. Si kama tu watoto wamekuwa wakisoma shuleni, bali pia wazazi walipaswa kusoma vitabu ili kuwasaidia watoto wao kuongeza elimu na kupata matokeo mazuri katika mitihani mbalimbali. Pindi watoto wanapokubwa na matatizo wazazi waweze kuwasaida kuyatatua. Mbali na hayo, wazazi wataendelea kuwapeleka watoto kujifunza elimu nyingine katika shule maalumu za Kingereza, hisabat ya Olimpiki,na kemikali ambapo wazazi huchoshwa zaidi kuliko watoto wao.

    Kipindi chashule ya msingi nchini China kina muda wa miaka 6, lakini kabla ya watoto kuhitimu kutoka shule ya msingi, wazazi wanaanza kuwa na wasiwasi kuhusu shule za sekondari. Kwa kuwa, watoto wakisoma katika shule moja nzui ya sekondari wataweza kuingia chuo kikuu chenye sifa nzuri. Lakini kusoma katika shule nzuri ya sekondari kunahitajika kusoma kwa bidii pia kufanya mitihani mingi, hivyo ili kufaulu katika mitihani hiyo, wazazi wanapaswa kwapeleka watoto wao katika mafunzo mengine mbalimbali na kuongeza elimu katika nyakati za mapumziko na wikendi. Mbali na hayo, wazazi huwa wanatafuta waalimu wa nje waje nyumbani mwao kufundisha watoto. Gharama hiyo ni kbuwa ambayo kwa mwalimu wa shule ya msingi ni Yuan 60 kwa saa, na mwalimu wa shule ya sekondari ni Yuan mia moja kwa saa. Aidha, kuna baadhi ya wazazi ambao wanawapeleka watoto wao kusoma masomo ya ziada nyumbani kwa walimu ili walimu waweze kusimamia masomo ya watoto kila wakati.

    Kuna wazazi wengine ambao wana uwezo wa kutosha kuwapeleka watoto wao kusoka katika nchi za nje. Hivi leo katika vyuo vikuu vya nchi mbalimbali duniani kuna wanafunzi wa China.bibi Wangjun anakaa katika mji wa Chengdu, mkoani Sichuan, kusini magharibi ya China, mwaka uliopita alimpeleka binti yake kusoma Uingereza, kila mwaka anahitaji Yuan laki 1.5. Bibi Wang alisema kuwa kusoka katika nchi za nje ni bora kwa maendeleo ya mtoto wake, kwanza anaweza kuongea Kingereza, hivi leo, wazazi wenye wazo kama bibi Wang ni wengi sana nchini China.

    Watoto wakisoma katika vyuo vikuu, wazazi wao huwa hawapati kupumzika. Wanatambua kuwa wakitaka kupeleka watoto wao kusoma katika vyuo vikuu vya nchi za nje kama wazazi wengine wanavyofanya, basi wanaanza kujinyima katika matumizi yao ili nao waweze kuwapeleka watoto wao kusoma katika nchi za nje. Watoto hawa wanapaswa kujizatiti katika mambo mengi yakiwa ni pamoja na kufannikiwa mtihani wa TOEFL,kampyuta na masomo mengine kabla ya kwenda nchi za nje.

    Kutokana na mchango mkubwa wa wazazi kwa elimu za watoto, uwezo na sifa za watoto wa China zimeinuka sana. Hususan katika miji mikubwa, watoto wameanza kuoongea lugha ya Kingereza, kutembelea mtandao wa Inter-net, kutumia kompyuta tangu walipokuwa watoto wadogo. Watoto hawa wana sifa nyingi, pia wana uwezo mkubwa wa kujitegemea wakati wanapokabiliwa na matatizo. Lakini wataalamu wengi wanasema kuwa hali hiyo ya wazazi kuzingatia kupita kiasi elimu kwa watoto inaleta matatizo. Kwa mfano, baadhi ya watoto siku zote wanasoma tu, na kupuuza kujenga afya za miili zao. Vilevile kuna watoto ambao hawataki kujifunza kitu kipya kutokanana na kuwa na wasiwasi wa kujifunza; wataalamu wanaona kuwa njia ya kuwaelimisha watoto katika nchi za nje siyo kwamba kunafaa kwa watoto wote wa China. Hivyo, kabla ya kupeleka watoto kusoma nchi za nje, ni bora kwa wazazi kufikiri kwa makini.

    Matokeo mazuri ya masomo ya watoto bila shaka nimuhimu sana, lakini wazazi hawawezi kuzingatia tu masomo ya watoto peke yake. Watoto wangepata maendeleo katika pande mbalimbali zikiwemo akili, afya, tabia nzuri n.k.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-28