Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-03 17:53:53    
Kituo cha kimatanfa katika anga ya juu

cri

    Kituo cha kwanza cha kimataifa kilichojengwa katika anga ya juu kwa ushirikiano na nchi 16 zikiwemo Marekani, Russia, Japani na Canada, kilianza kujengwa katika mwaka 1998. kituo hicho ni mradi wa ushirikiwano wa kwanza kwa ukubwa katika eneo la sayansi na teknolojia ya usafiri wa anga ya juu duniani, na pia ni kituo cha kwanza cheney binadamu ilichojengwa na nchi nyingi kwa ushirikiano.

    Mpango wa ujenzi wa kituo cha kimataifa cha anga ya juu ulitolewa na Marekani mwanzoni mwa miaka 80 ya karne ya 20, ambao hapo baadaye ulishirikiwa na shirika la usafiri wa anga ya juu ya Ulaya, Canada na Japani kwa nyakati mbalimbali. Tarehe 1 Novemba mwaka 1993 shirika la usafiri wa anga ya juu ya Marekani ilisaini mkataba na shirika la usafiri wa anga ya juu ya Russia ambalo lilikuwa pekee lenye uzoefu wa usafiri na kusafirisha vitu vikubwa katika anga ya juu, zikiamua kujenga kituo cha kimataifa katika anga ya juu katika msingi wa kituo cha anga ya juu kijulikanacho "Amani". Tarehe 29 Januari mwaka 1998, wawakilishi wa nchi 15 huko Washinton, Marekani walisaini mikataba ya kujenga kituo cha kimataifa katika anga ya juu pamoja na nyaraka 3 za kumbukumbu za pande mbili, zikitarajia kumakilisha ujenzi wa kituao cha anga ya juu kwa muda wa miaka 9 na kukamilisha ujenzi kasisa mwaka 2006.

    Usanifu wa kituo cha kimatafa katika anga ya juu ulitumia muundo kama mabehewa yaliyo tundikwa kwenye boriti, yaani boriti ni kitu cha msingi, mabehewa mengine kama ya kuongezea nguvu ya hewa na huduma yalitundikwa kwenye biriti hilo kubwa. Muundo wa namna licha ya kuweza kuongeza uimara wa kituo kilichojengwa katika anga ya juu, bali pia unachangia kufanya kazi vizuri kwa matawi ya mfumo, zana za majaribio ya kisayansi, zana za upimaji, kujizatiti kwa wanaanga kabla ya kutoka katika mabehewa na kufanya matengenezo angani.

    Hivi sasa, katika kituo cha anga ya juu, ujenzi wa mabehewa 6, mkono mrefu wa mtambo na betri ya sola umekamilishwa. Baada ya kukamilishwa kabisa ujenzi wake, kituo hicho cha kimataifa chenye uzito wa tani 500, kitakuwa na maabara 6, behewa moja la makazi, mabehewa matatu ya viunganisho pamoja na mifumo ya kudumisha uwiano, umeme, huduma na uchukuzi. Uongozi na udhibiti wa kituo hicho ya anga ya juu, zitakuwa za Marekani na Russia zamu kwa zamu ambapo Marekani inatakiwa kujenga kituo cha kimataifa kwa kutumia ndege zilizopelekwa katika anga ya juu kwa maroketi, wakati Russia ina;ekeka watu na mizigo kwa vyombo vya usafiri katika anga ya juu.

    Baada ya kukamilishwa ujenzi wake, kituo hicho cha kimataifa kitakuwa kama "mji wa anga ya juu" unaowawezesha binadamu kukaa kwa muda mrefu. Katika hali ya kawaida kituo hicho kina nafasi ya kukaa kwa muda mrefu kwa wanaanga 7, na kinaruhusu wanaanga 15 kufanya shughuli za uchunguzi juu yake, hivi sasa kituo hicho kinaweza tu kutumiwa na wanaanga watu kufanya uchunguzi kwa muda mredu.

    Hivi sasa, ujenzi wa kituo hicho cha kimataifa umekabiliwa na matatizo. Tokea mwaka 2001, Marekani ilipunguza kwa kiwantgo kikubwa bajeti ya usafiri wa anga ya juu, shirika la usafiri wa anga ya juu la Marekani nalo lilitangaza kupunguza mpango wa ujenzi wa kituo cha kimataifa na kuacha ujenzi wa mabehewa mawili ya kituo. Ajali ya "Colombia" iliyotokea mwaka jana ilifanya ndege ya usafiri wa anga ya juu ya Marekani kusimamisha kwa muda usafiri wake, jamba ambalo limeathiri ujenzi wa kituo cha kimataifa. Russia kutokana na uhaba wa fedha za bajeti ya usafiri wa anga ya juu, hali ambayo inafanya watu kuwa na mashaka juu ya uwezo wa nchi hiyo kumaliza kazi ilizogawiwa katika ujenzi wa kituo na kuhakikisha wanaanga 7 kufanya kazi kwa muda mrefu ndani yake.

    Hivi karibuni, wataalamu wa Russia walisema kuwa endapo China itafanikiwa kurusha angani chombo cha Shenzhou No. 5 chenye binadamu ndani yake, huenda China itaalikwa kushiriki katika ujenzi wa kituo cha kimataifa cha anga ya juu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-03