Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-04 19:43:53    
Walemavu Wachina Wengi Wanaojikakamua Wafanikisha Maisha yao Kwa Moyo wa Ukakamavu

cri
    Mwanakampuni ambaye ni mlemavu kutoka mji wa Huhehaote,mkoa ujiendeshao wenyewe wa kabila la wamongolia Bw. Chen Guoyi ana kampuni 6, kila mwaka analipa ushuru wa yuan za renminbi zaidi ya milioni moja kwa taifa.

    Ingawa Bwana Chen Guoyi ni mlemavu lakini amefanya miujiza, alisema kuwa,"Naamini kuwa, watu wenye ulemavu wanaweza kufanya shughuli kama watu wa kawaida wanavyofanya, ikiwa tunajikakamua kwa kujiendeleza tutaweza kupata mafanikio mazuri."

    Mkuu anayehusika wa Shirikisho la walemavu wa mkoa ujiendeshao wenyewe wa kabila la wamongolia alieleza kuwa, chini ya uangalifu wa serikali, maendeleo ya kijamii, na mabadiliko ya mawazo ya walemavu wenyewe, sasa idadi ya walemavu wanaojikakamua kwa kujiendeleza kama alivyofanya Chen Guoyi imeongezeka siku hadi siku. Wanachapa kazi katika maeneo mbalimbali ya jamii, wamesifiwa na kuheshimiwa kutokana na ukakamavu na bidii zao.

    Chen Guoyi mwenye umri wa miaka 49 alilemaa mkono wa kushoto alipozaliwa. Kuanzia utotoni, yeye aliweza kuvumilia zaidi kuliko watu wengine wa kawaida. Uchungu na hali ya kujifunga iliwahi kumtenganisha na jamii ya watu. Bwana Chen Guoyi alisema kuwa, "Nilikuwa karibu kupoteza matumaini ya maisha yangu".

    Sera ya serikali ya China ya kuwapa kipaumbele walemavu katika ajira ndiyo ilimpa fursa ya kujikakamua. Mwaka 1971, Bwana Chen Guoyi alikuwa mwalimu wa kiwanda cha kutengeneza matanki ya mji wa Huhehaote,maisha yake yalibadilika kuanzia hapo. Ili kufanikisha maisha yake,Chen Guoyi alijifunza mwenyewe masomo ya chuo kikuu, baada ya jitihada zake bila ya uvivu waktik akiwa na umri wa miaka 17, hatimaye alipata diploma ya chuo kikuu cha walimu cha mkoa ujiendeshao wa kabila la wamongolia.

    Mwaka 1988, Chen Guoyi alifungua kampuni yake ya kwanza, alitia mkataba wa kuendesha kiwanda cha kutengeneza vinywaji katika shule ya sekondari ya 31 ya mji wa Huhehaote. Baadaye alijishughulisha tena na kazi ya ujenzi, uuzaji wa nyumba, mkahawa, hatimaye alipata mafanikio makubwa katika shughuli za biashara. alipofanya shughuli za biashara, alipata uungaji mkono na msaada mkubwa kutoka kwa idara mbalimbali za serikali. Chen Guoyi alisema kuwa:"kuendesha kampuni si kama tu kunaweza kutimiza matumaini yangu ya kimaisha,bali pia kunaweza kuisaidia serikali katika kuongeza nafasi za ajira kwa walemavu wengi." Yeye alifanya juhudi kwa awezevyo kuwapatia nafasi za ajira walemavu wengi zaidi katika viwanda na kampuni zake.

    Mkuu wa baraza la walemavu la mkoa ujiendeshao wa kabila la wamongolia Bwan Pan Runhui alifahamisha kuwa, sasa mkoa huo una walemavu wapatao laki 9 na elfu 64. Miongoni mwao, walemavu laki 6 na elfu 9 wako vijijini na mbugani,wengine wako mijini.

    Mwaka 2003,mkoa ujiendeshao wa kabila la wamongolia uliandaa masomo ya kiufundi kwa walemavu elfu kumi hivi ili kuwapatia ajira, walemavu walioajiriwa wa mkoa huo walifikia asilimia 78.3. Mkoa huo pia umeanzisha data ya walemavu wenye sifa nzuri, mwaka 2003, walemavu 60 waliorodheshwa kwenye data hiyo.

    Mwaka jana, mchoraji mlemavu wa kike Tang Xiaoqi alifanya maonyesho ya michoro yake chini ya msaada wa shirikisho la walemavu la mkoa ujiendeshao wa kabila la wamongolia. Mawaidha ya kumsifu kutoka kwa watazamaji yalimpa moyo zaidi.

    Kwa jumla sasa wako walemavu milioni 60 hivi nchini China, ambao wanachukua asilimia 5 ya idadi ya jumla ya watu wa China. Chini ya sera ya serikali ya China ya kutoa kipaumbele walemavu katika kuwapatia ajira, kiasi kikubwa cha walemavu wameajiriwa katika idara mbalimbali, wengine wamejishirikisha katika biashara ndogo ndogo.

    Kama mfanyakazi wa ofisi ya hifadhi ya haki katika shirikisho la walemavu la mkoa ujiendeshao wa kabila la wamongolia Bw. Gao Qing alivyosema kuwa, hali ya walemavu wa China imeboreshwa siku hadi siku kwa kulinganishwa na ile ya zamani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-04