Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-05 21:35:29    
Kuotesha mbegu kwenye anga ya juu

cri
    Mwezi Oktoba mwaka 2003, China ilifanikiwa kumpeleka mwanaanga wa China kwenye anga ya juu. Ndoto ya kusafiri kwenye anga ya juu waliyo nayo wachina ilitimizwa. Chombo cha safari kilichosafiri katika anga ya juu, yalifanyika majaribio mengi ya kisayansi, kuotesha mbegu ni mojawapo katika majaribio hayo. Leo tunawaletea maelezo kuhusu kuotesha mbegu kwenye anga ya juu.

    Kuotesha mbegu ni teknolojia mpya, mbegu za mimea zikipelekwa kwenye anga ya juu, mchakato wa uoteshaji wa mbegu utakuwa na mabadiliko mapya tofauti na ule wa duniani kutokana na hali tofauti ya anga ya juu yenye miunzi mikali, mvutano mdogo, na isiyo na vijidudu. Hatimaye mbegu hizo zikipandwa kwenye ardhi ya dunia, baadhi yao zitaweza kuzalisha aina mpya za mazao ya kilimo.

    Msanifu mkuu wa mradi wa chombo cha kupeleka binadamu kwenye safari ya anga ya juu Bw. Wang Yongzhi anafahamisha:

    "Tulitumia mazingira mazingira maalum ya anga ya juu kufanya majaribio mbalimbali ya kisayansi na kiteknolojia kuhusu sayansi ya maisha, baada ya kukupata mionzi mikali, mbegu zinaweza kutokewa na mabadiliko."

    Kuanzia mwaka 1987, China ilianzisha majaribio ya kuotesha mbegu katika anga ya juu, baada ya hapo kilianzishwa kituo cha utafiti wa uoteshaji wa mbegu kwenye anga ya juu. Zaidi ya miaka 10 iliyopita, China ilitumia satilati 9 na vyombo 5 vya safari ya anga ya juu kupeleka mbegu za aina mbalimbali kwenye anga ya juu, mbegu hizo za aina mia kadhaa ni za nafaka, mboga, maua na kadhalika. Kuotesha mbegu za aina mpya ya mimea katika ardhi ya dunia kunahitaji miaka 8, lakini majaribio hayo yakifanyika kwenye anga ya juu yanahitaji miaka 4 tu. Baada ya kupandwa kwa mbegu hizo kwenye ardhi dunia kwa miaka minne mfululizo, ndipo inapoweza kupata aina mpya bora ya mbegu. Watu waliita mbegu hizo mpya zilizooteshwa kwa njia hiyo kuwa "mbegu za anga ya juu". Hivi sasa China imepata mimea mipya ya aina mbalimbali baada ya kuotesha mbegu kwenye anga ya juu, mimea hiyo ni pamoja na mpunga wa maji, ngano, nyanya n.k.

    Wilaya ya Ci iko kilomita 300 kutoka Beijing, mji mkuu wa China. Katika sehemu hiyo, zimepandwa mboga za aina nyingi ambazo mbegu zao ziliwahi kuoteshwa kwenye anga ya juu. Mwandishi wa habari aliona kuwa, mazingira ya sehemu hiyo ya upangaji mboga hakuna tofauti na yale ya upandaji mboga za kawaida, lakini mboga za sehemu hiyo ni kubwa zaidi. Kwa mfano tango moja iliyozalishwa kwenye sehemu hiyo urefu wake ni zaidi ya mita moja, na uzito wa pilipili hata kuwa na gram mia 8. Fundi wa kilimo wa wilaya hiyo Ndugu Xie Aimin alisema:

    "Ukuaji wa nyanya ambazo mbegu zake ziliwahi kuoteshwa kwenye anga ya juu ni mzuri sana, mimea yake ni mirefu zaidi na zao la pilipili huwa na uzito wa gram mia 3, mbali na hayo ina uwezo mkubwa wa kukinga maradha ya ugonjwa na wadudu. Mboga za aina hiyo hazihitaji kutiwa mbolea za chumvichumvi, ni mboga zisizo na uchafuzi."

    Mtaalamu alifahamisha kuwa, mbegu zikioteshwa kwenye anga ya juu, mimeya yake huwa na uwezo mkubwa wa kukinga na madhara ya ugonjwa na wadudu, mazao huwa na sifa nzuri na ongezeko la utoaji wa mazao hayo huzidi kwa 30% kuliko mimea ya kawaida. Hivyo, kupanda mboga na nafaka ambazo mbegu zao ziliwahi kuoteshwa kwenye anga ya juu kunazingatiwa zaidi na wataalamu wa kilimo wa China. Walisema kuwa, China ilitumia 7% ya ardhi ya dunia kutatua suala la lishe ya wachina wanaochukua 22% ya idadi ya watu wa dunia, sababu muhimu ni kutegemea njia ya kuongeza utoaji wa mazo ya kila hekta. Hivi sasa katika hali ya ufundi wa jadi, uwezo wa utoaji wa mazao ya kila hekta umekuwa chini sana, ikitaka kudumilisha maendeleo endelevu ya kilimo na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi, huenda kutegemea teknolojia ya kuotesha mbegu bora kwenye anga ya juu ni njia nzuri kwa utatuzi wa masuala hayo.

    Baada ya kufanya juhudi kwa miaka mingi, nafafa na mboga za aina mbalimbali ambazo mbegu zao ziliwahi kuoteshwa kwenye anga ya juu zimeanza kuuzwa kwenye soko. Kwa mfano mahindi yenye rangi mbalimbali, pilipili tamu zote zimekuwa chakula cha kawaida kwa watu wa China.

    Meneja wa Kampuni ya mbegu ya wilaya ya Ci Bibi Li fen alifahamisha akisema:

    " Wafanyabiashara wa sehemu mbalimbali wa China walikuja sehemu yetu kufanya ukaguzi kuhusu upandaji wetu wa mboga ambazo mbegu zao ziliwahi kuoteshwa kwenye anga ya juu, wana hamu kubwa kwa mboga na hizo na wote wamenunua mboga hizo."

    Kwa kutegemea njia ya kuendeleza upandaji wa mboga ambazo mbegu zao ziliwahi kuoteshwa kwenye anga ya juu, kampuni ya Bibi Li ambayo ilianzishwa kwa miaka 2 tu ilipata mafanikio makubwa, sasa wanataka kukuza zaidi uzalishaji wao mboga. Hivi sasa kampuni hiyo si kama tu ilianzisha vituo viwili vya kuotesha mbegu mkoani Hebei, bali pia ilianzisha shughuli zake mkoani Shanxi, Jiangsu na sehemu nyingine. Meneja Lifen alisema kuwa, shughuli zake zitafanyika katika nchi za nje. Kwa kuwa kuotesha mbegu na kupanda mimea ya aina hiyo kumeleta ufanisi mzuri wa kiuchumi, hivi sasa thuluthi mbili za mikoa ya China inafanya shughuli husika. Marekani, Russia, Bulgaria, Philippine na nchi nyingine zinashirikana na China katika nyanja hizo.

    Ofisa wa kituo cha utafiti wa uoteshaji wa mbegu kwenye anga ya juu cha China Bwana Sun Yongcheng aliainisha kuwa, China imeona ipasavyo umuhimu wa kuotesha mbegu kwenye anga ya juu. Alisema:

" China imeamua kurusha satlaiti moja inayotoa huduma kwa uoteshaji wa mbegu kwenye anga ya juu, baadaye itakamilisha mradi wa uoteshaji wa mbegu kwenye anga ya juu kutokana na eneo tofauti ya kimaumbile na aina tofatui za mimea. China itaweka mkazo kuotesha mbegu zitakazoleta ufanisi mzuri wa kiuchumi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-05